VIJANA CHADEMA wamvaa RPC Kamuhanda kwa uongo, uzushi, wakumbusha mauaji ya Mwangosi

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,071
BARAZA LA VIJANA LA CHADEMA (BAVICHA) IRINGA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Iringa limesikitishwa na kitendo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda kujivika jukumu la kupachika raia vyeo ambavyo haviko kwenye utaratibu wa CHADEMA wala BAVICHA ilili kutimiza lengo la kujaribu kukipaka matope CHADEMA na BAVICHA.

Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa zilizotolewa na Bwana Kamuhanda, RPC wa Iringa na na kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Bwana Athanas Mongo (mtuhumiwa wa ujambazi) ni Kamanda wa Vijana wa CHADEMA Mkoa wa Iringa ni uongo na uzushi wenye hila za makusudi za kujaribu kuharibu taswira ya BAVICHA na CHADEMA kwa umma.

Bwana Mongo anayetuhumiwa kwa ujambazi si Kamanda wa BAVICHA Mkoa wa Iringa na wala Muongozo wa Mabaraza ya chama unaosimamia mabaraza yote likiwemo BAVICHA kwa upande mmoja na Katiba ya CHADEMA kwa upande mwingine haina na wala haitambui cheo ambacho RPC Kamuhanda kamvisha bwana Mongo.


Tunavyojua sisi hicho ni cheo kinachotumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Sasa labda RPC Kamuhanda ni mzoefu wa kukariri vyeo vya CCM. Yeye anajua hilo.

Mongo ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA na asiyekuwa na cheo chochote ndani ya BAVICHA wala CHADEMA. Ni Mtanzaniamwenye haki ya kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa. Kutuhumiwa kwake kwa masuala ya uhalifu hakupaswi wala hakuwezi kuhusiswa na CHADEMA wala BAVICHA.

BAVICHA tunamuonya RPC Kamuhanda kuacha mara moja tabia ya kukurupuka na kutokuwa makini katika utendaji kazi kiasi cha kuingilia na kujaribu kubaka Katiba ya CHADEMA na Kanuni za BAVICHA ili tu kukidhi haja yake ya kuipaka matope CHADEMA baada ya kushindwa hila hizo kwenye tukio la mauaji ya Mwandishi wa habari, marehemu Daudi Mwangosi kule Nyololo.


Bila shaka ni ukurupukaji na kukosa umakini kama huu, ndiyo uliosabisha RPC Kamuhanda akakiuka misingi ya utawala bora kama ilivyoelezwa na Ripoti ya Uchunguzi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala juu ya mauaji ya Mwangosi.


Uchunguzi huo wa THUB ambacho ni chombo cha serikali chenye majukumu ya kikatiba na kisheria kuhusu masuala ya haki za binadamu ulibaini kuwa RPC Kamuhanda mnamo tarehe 02/09/2012 alikiuka Sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11(a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeye hakuwa “Officer In-charge” wa polisi wa eneo husika. Kwa maana hiyo amri aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri hiyo. Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.


Kwa mantiki hiyo, ukiukwaji huo wa sheria uliofanywa na RPC Kamuhanda, ulipelekea tukio la Nyololo ambapo Mwandishi wa Habari Mwangosi aliuwawa na Jeshi la Polisi.


Kimsingi baada ya taarifa hiyo ya uchunguzi uliofanywa na chombo cha serikali, unaoonesha kuwa utendaji mbovu wa Kamuhanda, RPC huyo pamoja na polisi wenzake walioshiriki katika tukio la Nyololo kumuua mwandishi wa habari, kisha wakaanza kufanya propaganda za kuipaka matope CHADEMA ili kuwanusuru wao, alipaswa kuwa amejizulu au amefukuzwa kazi na kushtakiwa mahakamani kutokana na tukio hilo la mauaji ya Mwangosi, kama ambavyo CHADEMA imeshauri mara kadhaa, ikiwemo kuandika barua kwa Rais Jakaya Kikwete.

Imetolewa na leo tarehe 10/04/2013 Mkoani Iringa na:

Joseph Nzala Lyata
Mwenyekiti BAVICHA
Mkoa wa Iringa



Sent from my iPad
 
safi.....kazi nzuri mr mwenyekiti mungu akuongezee busara na awape upofu wote wanaokwenda kinyume na ukweli amen
 
Mongo ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA na asiyekuwa na cheo chochote ndani ya BAVICHA wala CHADEMA.


hapo kweny bold naomba ufafanuzi sijaelewa
 
Kumbe huyu RPC hakushtakiwa kwa mauaji ya Mwangosi???

mkuu nani wa kumshitaki mteule wa rais??? sahau hilo mkuu, tuliyataka wenyewe 2010.

kama ulikuwa hujui chukua maneno haya hapa ( VYOMBO VYOTE VYA USALAMA NCHI HII VIPO KUILINDA SISIEMU NA UTAWALA WAKE HATA KAMA WATAVUNJA SHERIA)
 
mimi mwenyewe nilivyoiona hiyo habari juzi nilijua tu, kuwa jamaa kabugi step. tutasikia mengi ya matukio ya mauaji na ujambazi kuhusishwa na CDM. baada ya kufeli udini na ukabila.
 
Mongo ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA na asiyekuwa na cheo chochote ndani ya BAVICHA wala CHADEMA.


hapo kweny bold naomba ufafanuzi sijaelewa

Nyabhingi

Hujaelewa kitu gani hapo. Sentensi imekamilika na inaeleweka.
 
Dah bongo bana bwana Kamuhanda yupo ofisini bado?

Si angalau wangemrudisha makao makuu wampangie kazi zingine? kama wanavyofanyaga.
 
Kama babu yenu ameweza kumkana mjukuu wake (Ludo), ndiyo itakuwa nyie wajukuu kumkana mjukuu mwenzenu?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kumbe huyu RPC hakushtakiwa kwa mauaji ya Mwangosi???

Benaire

Jamaa anatamba tu mtaani. Inasemekana karibu atarudishwa HQ ili astaafu vizuri na kula pensheni yake na stahili zake zingine zote ambazo kimsingi hakustahili.

Si yeye tu, hata hawa hapa chini kwenye picha, hawajashtakiwa. Hata aliyeshtakiwa hadi leo ni mauza uza tu. utafikiri walitoa uhai wa kuku vile. Serikali inayochezea uhai wa binadamu, tena raia wake kiasi hiki, ni serikali iliyopoteza uhalali wa kuongoza. It will hunt them.
 
Mongo ni mwanachama wa kawaida wa CHADEMA na BAVICHA na asiyekuwa na cheo chochote ndani ya BAVICHA wala CHADEMA.


hapo kweny bold naomba ufafanuzi sijaelewa

Nini ambacho haujaelewa? Mimi ni mwanachama hai wa CCM nina kadi na nalipa ada zote kila mwaka, lakini SINA CHEO CHOCHOTE NDANI WA UVCCM WALA CCM! umeelewa sasa? vyuo vya kata bhana!
 
Back
Top Bottom