Vigogo wauza unga wakamatwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,140
Na Makongoro Oging’, UWAZI
DAR ES SALAAM: WALE vigogo wanaosadikiwa kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ‘unga’ nchini wameanza ‘kutumbuliwa majipu’ kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuanza kuwakamata, Uwazi linakupa zaidi.

Kwa mujibu wa vyanzo vyetu ndani ya jeshi hilo, vigogo wengi wanaojihusisha na biashara hiyo walikamatwa wiki iliyopita katika maeneo ya Kinondoni, Ilala na Temeke, Dar baada ya wengine wengi kukamatwa siku za nyuma kutokana na kudaiwa kuingiza unga nchini kwa nyakati tofauti.

Hycenth.

Imedaiwa kuwa, baadhi ya vigogo hao wanamiliki majumba na magari ya kifahari na kufuatia taarifa zilizowataja kuwa ni wauza unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia baadhi ya mali zao, kama magari na nyumba na kufanya uchunguzi wa uhalali wake.

Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser VX, Jeep, Mercedes Benz, Toyota Altezza, Toyota Harrier na mengine mengi ambayo wahusika walikuwa wakitanua nayo mjini huku vijana wengi wanaotumia unga wakizidi kuwa mateja.

Habari za uhakika kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa, kesi za baadhi ya watuhumiwa zinaendelea kuunguruma mahakamani huku kukiwa na madai kwamba, baadhi ya watuhumiwa walisaidiwa kutoroka nchini na hivyo kuruka dhamana.

DCI AZUNGUMZA NA UWAZI
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Tanzania, DCI Diwani Athuman alikiri kufanikiwa kuwakamata watu wengi wanaojihusisha na biashara ya unga kufuatia msako mkali unaofanywa na jeshi hilo nchi nzima kwa kushirikiana na kitengo cha kupambana na kudhibiti madawa ya kulevya nchini na taasisi mbalimbali za serikali.

“Tumechukua hatua hii ili kukisambaratisha kikundi cha watu wanaojihusisha na biashara hii haramu na ninawaomba wale wote wanaojihusisha ambao hatujawakamata wajue tutawafikia na hakuna atakayepona. Naomba ushirikiano wa wananchi kuendelea kuwafichua,” alisema DCI Athuman.

WALIOTOROKA KUFUATILIWA
DCI aliongeza kusema kwamba, wale waliokimbilia nje ya nchi lazima watafuatiliwa na kutiwa mbaroni na kazi hiyo pia imewajumuisha polisi wa kimataifa (Interpol) na akasisitiza kuwa, watakamatwa na kurejeshwa nchini kukabiliana na kesi zao.

WALIOKAMATWA WAKITOROKA
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya jeshi hilo vinasema kwamba wapo wauza unga waliokamatwa wakati wakitoroka na wamenyang’anywa hati zao za kusafiria.

NZOWA AZUNGUMZA NA UWAZI
Naye Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Kupambana na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, SACP Godfrey Nzowa alipoulizwa kuhusiana na zoezi hilo la kamatakamata za watuhumiwa wa kuuza unga alikiri kuwa lipo na linaendelea vizuri.

IMG_3361.jpg
Shoaib.

“Tunashirikiana vizuri na vyombo vingine vya dola. Hakika Rais Magufuli amefanya biashara hii haramu iishe hapa nchini. Anawachukia watu hawa kama mimi ninavyowachukia. Suala hili ni mtambuka,” alisema Nzowa na kuongeza kuwa, wapo waliofikishwa mahakamani na baadhi yao wameshafungwa jela za ndani na nje ya nchi.

TAKWIMU ZA MIAKA 6
Kamanda Nzowa aliweka wazi takwimu ya ukamatwaji wa watuhumiwa hao kutoka mwaka 2009 hadi mwaka huu na orodha hiyo inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.

Steven Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gramu 1,800), Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu 1,007.4), Dhoulkefly Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu (heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000). Huyu alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.

IMG_3380.jpg
Ben.

Wengine ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza (cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu 286). Huyu alikuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin Jalal.

Kamanda Nzowa akaendelea kuwaanika, Jack Vuyo, (heroin gramu 42,000). Huyu alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete. Simon Eugenio Fadu (cocaine gramu 8,000), Assad Aziz, (heroin gramu 50,000). Alikuwa na Isamil Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.

Leila-wa-Kenya.jpg
Leila.

Wengine kwenye orodha hiyo ni, Anna Jamaniste Mboya, (cocaine gramu 1,140 amefungwa miaka 20 na faini shilingi milioni 148), Fredy William Chonde ‘Willy’ (heroin gramu 175,000), Abdul Ghan na Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani walipewa dhamana kinyemela na wakatoroka. Walikamatwa wakiwa na cocaine gramu 804.7), Chukwudu Denis Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria) (cocaine gramu 81,000).

Aidha, wapo Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo, (cocaine gramu 1,530), Kadiria Said Kimaro (heroin gramu 1,365.91), Abdallah Rajab Mwalimu (cocaine gramu 716.5), Mwiteka Godfrey Mwandemele (cocaine gramu 1,112), Abbas Kondo Gede (cocaine gramu 1,112), Mwanaidi Ramadhan Mfundo (cocaine gramu 5,000). Alikuwa na Sara David Munuo, Antony Karanja, Benny Ngare, Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha Said Kungwi, Rajab Juma Mzome na John William Mwakalasya.

IMG_3355.jpg
Wengine ni Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000). Alikuwa na Aziz Juma Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa na Hamidu Kitwana Karimu.
Ramadhan Athuman (heroin gramu 3,000). Alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed Kichaa na Issa Abdulahman. Rashid Ally Mtopea (heroin gramu 12,000). Alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam.

Maurine Amatus Lyumba, John Adams Igwenma, Mnigeria (cocaine gramu 830.19), Upendo Mohammed Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis sativa gramu 1,000). Alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi Malven Kalu Oko (Wanigeria) (heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine gramu 3,882.92), Alberto Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroin).

madawayakulevya.jpg
Wengine ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne, Mnigeria, (gramu 1,245.96 za heroin), Kwaku Safo Brobbey, Mghana (gramu 13,781.78 za heroin), Princewill Ejike Mnigeria (gramu 981.12 za heroin).

Mary Mvula, Mzambia (gramu 391.51 za cocaine), Waziri Shaban Mizongi, (gramu 2,013 za heroin). Alikuwa na Santos Joseph Mpondela, Kelvin Kelven Mwazeni.

Wengine ni Emmanuela Adom, Mghana (gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omar Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed Said, (gramu 9,857.54 za bangi). Alikuwa na Abdullatif A. Fundikira.

157.jpg


Mfano wa magari wanayomiliki.

Aliendelea kuwataja, Marceline Koivogui, Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin Cheleh Swen, Mliberia (gramu 1,509.35 za heroin). Alikuwa na Benjamin Obioma Onuorah wa Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za cocaine), Josephine Mumbi Waithera, Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine).

Iddi Juma Mfaume (gramu 563.25 za heroine), Amina Kassim Ramadhan, (gramu 1,980.11 za heroine), Vivian Edigin, Mnigeria (gramu 797.56 za cocaine), Hadija Tambwe, (gramu 33,507.04 za cannabis), Sasha Farhan, Mnyeke Sativa na Mychel Andriand Takahindangeng, Muindonesia (gramu 3,932.44 za cocaine).

Toyota_Prado_GXL_102.jpg
Wengine ni Kristina Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen Basil Ojiofor, Mnigeria (gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, (gramu 1,793 za heroin), Khamis Said Bakar, (gramu 1,793 za heroin).

Kundi la mwisho ni Tabia Omar au Neema Omar (gramu 994.97 za heroin), Masesa au Habiba Andrew Joseph, (gramu 1,037.9 za heroin). chanzo.GBP
 
Sijamwona kigogo hapo...alafu heroin nyingi sana tz,nimeona habari ya Chanel ten mnaijeria kakamatwa na Heroin kg 8 kama sikosei,anataka kutoka nayo nje ya nchi.
 
Hao ndio vigogo mbona wanatuchezea akili,kutufanya watoto....

Nini maana ya tafsiri kigogo?? Kwa taarifa yako hiyo biashara ya unga hufanywa na watu wakawaida sana ambao wanahela nyingi sana wako mtaani huko na mwisho wa siku wakaiweka serikali mkononi kwa kununua baadhi ya viongozi wasiowaaninifu. Ila kwa biashara hiyo hayo majina ni kweli kuna vigogo wa biashara hiyo mfano huyo mama anaitwa LEILA ni hatari sana anamiliki plaza kadhaa pale nairobi, shikuba sijui ameindikwa jina gani hapo naye ni kigogo kwenye hiyo biashara,, choji naye ni hatari hapo... Hakuna kiongozi mwenye network ya unga bila kupitia kwa hao akina CHONJI maana hao ndio huijua hiyo biashara huko ilikotoka na soko lake kwa wazungu...
kwa taarifa yako huyo mama LEILA hata obama alimtaja kwenye moja ya taarifa zake za madawa ya kulevya, amebebesha unga mpaka baadhi ya mawaziri wa serikali ya kenya... PITA mitaa ifuatayo kwa kuuliza hayo majina kwenye mitaa hii temeke,ilala,kinondoni,magomeni na manzese ndio utawajua hao watu kwanini ni vigogo...hao unaowahisi ni wanafunzi tu na wengi wao wamefundishwa biashara na moja ya hao watu, ushahidi wa kuwatia mkononi ni vigumu maana wako mbali na ushahidi kwakutokaa kwao front,, ili kumkamata mtu kama Chonji, shikuba serikali imefanya kazi maana ni watu hatari sana na ndio mizizi kwa taarifa yako, CHONJI amelea sana baadhi ya vijana wa Radio fulani na kuwapa jeuri mjini maana inaonekana alikuwa akiwapa kazi, pia ndiye aliyemfundisha kazi giant mmoja maarufu sana..
 
Waandishi wa habari wa tanzania ni shida sana,,,, umetuwekea picha za magari ya kwenye mtandao, baada ya kupiga picha ya hayo magari ya wahusika na kutuwekea,, hao watu wengi kwa taarifa yako walikamatwa kwenye utawala uliopita na taarifa zake zipo siku nyingi humu JF.. tunataka upadates ya hizo taarifa na sio blah blah za udaku wenu... Fanyeni kazi
 
Mbona mwenye kiupele cheusi uson hajakamatwa? Wangeanza na huyo.

Halafu waandishi wa Tz hovyo kabisa wame download picha za magari kwenye mitandao ndio wanatuwekea humu?? Halafu mwandishi anakalsha kengere zake na kusema alteza nayo gari ya kifahari. Shenzy kabisa
 
Haapo hamna kigogo mkuu hao ni ma supervisor tuu wa kawaida vigogo bado
 
Wana habari wanapotosha ili wauze magazeti ili hali wanajua hawa sio vigogo, watanzania tunataka kusikia mapapa wakikamatwa
 
Ndiyo ktk list hapo ya waliyokamatwa ni mama leila tena alikamatwa miaka 5 nyuma!
Ila bado kuna vigogo wako mitaani wanajiachiaa
Wale ma main supplier wa kino,na ilala na tmk wapo tu na hawajagusswaa

Ovaaa
 
Back
Top Bottom