kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Tunasubiri vifo ili turushe helkopta kuangalia kiwango cha uharibifu na idadi ya waliokufa badala ya kunusa mapema hatari na dalili vifo.
Kwa kilichotokea Hanang ni matokeo ya mipango mibaya ya watanzania wenzetu tunaowalipa kwa kazi ya kutulinda na majanga. Kuna idadi kubwa ya watanzania ambao wameruhusiwa kujenga chini na juu ya milima, mabondeni, kwenye njia za maji na wanyama.
Watu hawa wamepewa vibali vyote ama vya kujenga, au kuingiza umeme na maji kwenye nyumba zao bila kupewa onyo la aina yoyote wala elimu ya namna ya kuishi kwenye maeneo hayo.
Maswali:,
1. Je, baada ya maafa ya Katesh, watu waendelee kujenga na kuishi kwenye maeneo yao yaleyale yaliyokubwa na janga au wahamie kwingine?
2. Je, Tanzania hakuna watanzania wanaoishi kwenye maeneo yanayofanana na maeneo ya Katesh?
3. Je, kuna mifumo gani ya kutaarifiana kama ving'ora kama likitokea janga?
Kinga ni bora kuliko kiba hii tunayoiona.