Videoder na waptrick zimekuwa hazifanyi kazi siku hizi, kulikoni?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,226
2,839
Kabla ya kuenea simu kubwa "smartphones" nakumbuka nilikuwa nadownload nyimbo zangu kupitia waptrick na siku mojamoja kupitia tubidy. Hata baada ya kuja simu janja nikawa naendelea kuingia waptrick kwenye browser naendelea kuinjoi

Akaja kaka yangu akanitumia file la kudownloadia linaitwa Videoder na hapo nikawa nimeisaliti waptrick kabisa... sasa siku nikaona nyimbo nikidownload kupitia videoder kuna mlolongo mrefu wa kupata wimbo halisi unaoutaka nikasema niingie waptrick nakuta imejaa matangazo kibao mpaka yananizuia nashindwa kuitumia nikaiacha

Siku nyingine tena kujaribu mwendo ni uleule basi nikajisemea bye bye waptrick, nikawakacha mazima nikabaki na videoder yangu. Mara videoder nao wakaanza masharti ya kusign in ndipo udownload nikaona fresh, mara usign in ndipo usearch nikachukulia poa pia, hee majuzi hakuna cha kusign in wala nini haitaki kabisa kufanya kazi upande wa "all" lakini kwenye browser unatumia tu

Tatizo hili lilikuwa kwangu tu kwa wenzangu fresh mara sasahivi wote hatutumii tumehamia vidmate lakini hata hakuna raha kama kwenye videoder. Huku matangazo yanasumbua mbaya napo. Features za vidmate hazikaribii videoder hata kwa mbali

Uzuri wa videoder kwangu ni urahisi wa kuitumia, features zake na uwezo wake wa kudhibiti matangazo wakati wa kuitumia. Uzuri wa waptrick nao ni audio zake (music) ambazo zinakuwa ni orijino kabisa siyo kama ukichukulia kwingine unakuta wimbo umewekwa mambo ambayo wewe huyahitaji

Tafadhali naomba mwenye ujuzi wa kufanya nirudie kutumia videoder na/au waptrick anisaidie!
 
Nadhani ni Playstore ndio hawataki kuiba vitu vya watu kutokana na masharti ya haki miliki
 
Tumia simu za kawaida zisizo smat utainjoi hata kama smat shart ziwe zile za zamani ila kwa hiz smat zetu toleo jipya hupati kitu
 
ukiona program yeyote inayohusika na wizi wa kazi za watu mtandaoni inafanya kazi vizuri tu na haina mqtangazi,ujue haina maisha itafungwa tu.

hata kule site za mauaji kwa saaa kuna video ukiigusa tu unaambiwa hapa mpaka peemium membership otherways pita vileee.
 
Waptrick inafanya kazi nimeingia jana tu nimeshusha ngoma za profesa J , ndio mzee.
Sema ina ads nyingi sana
 
Enzi ya waptrick na wapdam kwenye kiswaswadu changu nilichokuwa nafanya Mungu anajua ,jamaa unimekumbusha mbali mno maana tulikuwa sita zangu pendwa kwa games,videos nk
 
Bila kusahau afmobi af1234
ukiona program yeyote inayohusika na wizi wa kazi za watu mtandaoni inafanya kazi vizuri tu na haina mqtangazi,ujue haina maisha itafungwa tu.

hata kule site za mauaji kwa saaa kuna video ukiigusa tu unaambiwa hapa mpaka peemium membership otherways pita vileee.
halafu zina madhara yake pia kwa simu yako.
 
Fungua waptrick kwa kutumia opera mini na browser zingine tofauti na Chrome.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom