Video: Nyerere akiri alikuwa Dictator

kweli lugha ni tatizo watu wanashindwa kutofautishisha " ". Kama kuna mwalimu wa kiswahili atusaidie. FFox kwa taarifa yako kwenye UDA ilikuwa mwanafunzi hawezi kuachwa kituoni. Wazo la JK sorry JKN kuanzisha KAMATA na UDA lilikuwa zuri tu
1. Basi liliweza kuondoka kituoni kwa muda maalum bila kujali kuwa limejaa au halijajaa na kama UDA ingeendelezwa vzr tungekuwa na
suluhisho la usafiri
2. Nauli za mabasi zisingekuwa zinapanda hovyo kama ilivyo sasa kwani hakuna bei ya kueleweka ya nauli
3. FYI kama kiwanda cha TIPPER kingekuwa kinafanya kazi hadi sasa sidhani kama kungekuwa na bei ya holela ya mafuta
4. Nyerere alikuwa haogopi mtu kama alivyomzuia JK na EL kugombea 1995 na kama alivyosema wazi kuwa CCM si mama yake anaweza kujitoa Kama binamu ndio kuna makosa atakuwa alifanya lkn ikumbukwe kipindi chake kilikuwa na misukosuko mingi
5. JKN aliheshimika sio kwa raia wake tu hata nchi za nje nakumbuka alipowa Kiwanja na Hati miliki China na ndipo tulipojenga ubalozi wetu kitu ambacho hakuna nchi yeyote ambayo imepewa kiwanja China
6. Ni yeye ambaye aliweza kupokea maandamano ya wanafunzi tena waliokuwa wanaenda ikulu kupinga yanayofanywa na serikali kutaka waziri mkuu ajiuzulu na akayapokea sijui kama hili limeshafanyika kwa raisi yeyote kama sio kuishia kudundwa na na FFU sasa hapa sijui dikteta ni Nyerere au waliomfuatia
7. Kipindi chake kuna watu walikuwa wanajitahidi kumjengea maadui kama ilivyofanyika kwa baba mdogo wangu wakati huo walipokuja watu kumuambia kuwa Nyerere amepanga kumuua hivyo aondoke kama Kambona alivyoondoka babamdogo aligoma kwakusema kuwa hana kosa hivyo bora afie hapa na hakuna lolote lililomtokea mpaka anafikwa na mauti miaka 6 iliyopita
8. kama ishu ni vijiji vya ujamaa ile ilikuwa haina budi kufanyika kwani ingekuwa ngumu kusambaza huduma za jamii kama watu wasingewekwa pamoja sehemu inayoeleweka
9. Ni Nyerere huyu aliyeanzisha elimu bure bila kujali umepata daraja langapi kigezo tu ni kuwa na sifa ya kudahiliwa na ukishajiunga chuo hela ziko pale zinakusubiri utasoma mpaka utamaliza ila kwasasa ni ngumu mtoto wa shule ya kata kupita division 1 form VI ili aweze kupata mkopo hivyo watoto wengi wa masikini watakosa elimukwani ningumu masikini kulipia hata 300000/= achalia mbali 3000000/=
10. Ni JKN huyu aliyekuwa anatoa matibabu bure tofauti na sasa unachangia lakini dawa zinaoza MSD na mahospitalini hakuna dawa sina mengi ya kusema ila JK sorry JKN alikuwa zaidi ya maraisi tz na Africa na Hata Mandela hawezi kukamata huyu jamaa kama utawalinganisha sema tu vyombo vya habari vimemkweza Mandela mno kwani JKN kachangia mambo mengi sio Tz tu bali Afrika kwa ujumla. Hehehe nafikiri ndugu FFox sorry mheshimiwa FFox umenipata kwani nchi haiweza kutengeneza hata jembe yote tunaagiza toka nje jamani hata kiberiti au taa ya kandili
 
Hivi hiyo elimu bure na matibabu bure walikuwa wanafaidika wa tz wangapi namaanisha tulikuwa na hosipitali/ vituo vya afya vingapi na tulikuwa na shule ngapi?
 
Pengine alikuwa na nia NZURI ila Strategy au execution of the Strategy ilikuwa Mbooovu kupita maelezo. Nia njema ikitekelezwa hovyo, hata wema wake huwa questionable
 
Pengine alikuwa na nia NZURI ila Strategy au execution of the Strategy ilikuwa Mbooovu

Hakuwa na watu. Na kwakuwa alikuwa dictator watu wakanyamaza wakajifanya waumini wa siasa zake. Alipoondoka tu wakaanza kufanya vitu vyao.
Hapo kwenye BOLD nakuunga mkono.
 
Neno DIKTETA mnalitumia vibaya humu JF. Sifa mama za dikteta zinafahamika na Mwalimu hakuwa nazo hata chembe:
-Dikteta haondoki, haachii madaraka kwa namna yoyote ile. Bila shaka mmewaona akina Gadaffi, huyu wa Syria, Huyu wa Korea Kaskazini aliyefariki juzi na aliyemtangulia, mlimwona Sadam kule Iraq,...Hawa mtawafananisha vipi na kwa lipi na Mwalimu?
-Dikteta hana mrithi mwingine zaidi ya wanae wa kuzaa. Hakuna mtoto wa Mwalimu amewahi kuwa hata Naibu Waziri.
-Dikteta hana vikao vya CHAMA. Hivi vikao unavyoona vinaendelelea ndani ya CCM na hata vyama vingine ni mfumo aliouacha Mwalimu. Sekretarieti, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu (wengine wanaita Baraza Kuu), Mkutano Mkuu,...
-Dikteta ananyonga kwelikweli. Mwalimu alishindwa kusaini watu waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe wengi tu. AHM alinyonga wengi kuliko Mwalimu.
 
si kila wakati udikteta ni mbaya hasa kwa taifa ambalo bado ni changa
Wachache wanaielewa dhana hii Matunge. Wanadhani kujenga nchi yenye MAKABILA, DINI, MATABAKA mengi kiasi hiki ni lelemama. Kusimamia KATIBA au SHERIA kunataka "udikteta" wa aina fulani hivi.
Ntakupa mfano mmoja dhahiri ambao kama Mwalimu angekuwa Rais wa JMT asingeukubali. Mabadiliko ya hivi karibuni ya KATIBA ya Zanzibar. Baadhi ya vipengele vinakinzana wazi na KATIBA ya JMT. Na katiba ya JMT iko wazi juu ya hili.
 
Back
Top Bottom