EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Mkuu unachoona kwenye video ni trela tu, picha lenyewe mwombe Mathias aandike asiweke video... Alikuwa eneo la tukio
Mkuu kabla ya haya kutokea kuna mtu toka maeneo hayo aliniambia kuwa baada ya kuwa mbunge alishauri kisiwa kimoja kilichopo Muleba Kaskazini kihamishiwe Mwanza. Wananchi hawakuridhika na hili. Hii issue nao imeandikwa na gazeti la Mtanzania leo.
Mbunge azomewa mkutanoni Muleba
Na Arodia Peter
MBUNGE wa Muleba Kaskazini (CCM), Charles Mwijage, ameanza kuonja shubiri ya kisiasa baada ya kuzomewa na kurushiwa mawe akiwa kwenye mkutano wa hadhara juzi jioni katika Mji mdogo wa Izigo ulioko Kata ya Izigo wilayani Muleba, Mkoa wa Kagera. Shuhuda wa tukio hilo, aliliambia MTANZANIA kwa njia ya simu jana, kwamba vurugu hizo zilianza wakati Mwijage alipowasili katika eneo hilo ambapo alipokewa kwa mabango mbalimbali yaliyokuwa na maneno ya kutorodhishwa na uongozi wake.
Pamoja na hayo, shuhuda wetu alisema vurugu hizo zilichagizwa na risala ya wananchi waliyoiandaa kwa ajili ya mbunge huyo ambapo alishutumiwa kwa hatua yake ya kukataa kuwa na Katibu katika ofisi yake ya ubunge iliyopo eneo hilo la Izigo. Shutuma nyingine ni hatua ya mbunge huyo kupendekeza katika vikao vya wilaya kuwa Kisiwa cha Goziba kiondolewe Muleba Kaskazini na kupelekwa Mwanza jambo ambalo linapingwa na wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwa litapunguza mapato ya wilaya yao kwa kuwa kisiwa hicho kina wavuvi na samaki wengi.
Alipozungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mwijage alikiri kuzomewa na kurushiwa mawe na wapiga kura wake ingawa alisema tukio hilo lilitokea kwa kuwa baadhi ya wananchi hawaelewi vipaumbele vyake. "Pamoja na mkutano wangu kuvurugwa, bado nitaendelea na mipango yangu ya kuhakikisha wananchi wanajikwamua kiuchumi kwa kuanzisha Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) pamoja na ufugaji wa nyuki na samaki.
Kutokana na vurugu hizo, taarifa kutoka Muleba zinasema kuwa, kilichomtokea mbunge huyo ni matokeo ya mgawanyiko wa Chama Cha Mapinduzi na makovu ya uchaguzi mkuu uliopita kwenye kura za maoni. Taarifa hizo zinasema kuwa kitendo cha Mwijage kukataa kutumia ofisi ya mtangulizi wake, Ruth Msafiri, kimetafasiriwa vibaya na kimekuwa ni kichocheo cha wananchi kugawanyika na kuwa makundi mawili.
Mbunge azomewa mkutanoni Muleba