VIDEO: Mahojiano na Mh. Zitto Kabwe katika Makutano Show

Heshima Kwako Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya shida,
Afisa muandamizi wa matatizo ya ghafla.
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimaskini.
Mweka-hazina wa Dhambi.
Mratibu wa uoga.
Raisi mstaafu wa mapenzi na udanganyifu wa hapa na pale.
Katibu mkuu wa madeni.
Balozi wa vishawishi.
Kiongozi wa malengo yasiyotekelezeka!
Nakusalimu tu..Za jioni Mheshimiwa?..!
[/QUOTE]

Makutano show, wala usikwazike na wadau kama hawa. Lazima wawepo ili dunia iweze kwenda. Yaani kwenye ecosystem, tunawahitaji sana maana baada ya kusugua sana ubongo na pilika za kutafuta rizki, unacheka kidogo ukikutana na watu hawa....
 
Makutano yanaelekea kuwa mazuri. Maoni ya Mhe Zitto yana mantiki yanafikirisha. Nichangie katika mojawapo ya aliyoyanena: nimependa hoja yake ya kuUTAKAKA urais vs kuOMBWA kuwa rais! Kwa maoni yangu vyote viwili vinaweza kuwa na faida na hasara - inategemea na mambo mengine mengi. Historia inaweza kuwa mwalimu wetu mkuu (headteacher).

Bila kwenda mbali sana Mzee Ruksa aliombwa kuwa Rais na Bwana wa Ukweli na Uwazi aliombwa kuwa Rais - matokeo ya kazi za waheshimiwa hawa tunazijua. Mhe JK, kwa upande wake, aliUTAKA SANA urais mwaka 1995 lakini alishauriwa asubiri hadi 2005. Kwa bahati mbaya, pamoja na kusubiri miaka 10 akisubiri kuingia Ikulu, hakuna ushahidi wa kutosha kwamba alitumia kipindi hicho kujenga 'ajenda' ya urais wake kwamba ungekumbukwaje hata baada ya kizazi hiki, yaani kutengeneza 'legacy'.

Kwa hivyo aliingia Ikulu bila dira [hapa ninaomba tutofautishe dira (vision) na kaulimbiu (slogans)] kiasi kwamba hata baada ya kuwa madarakani muhula wa kwanza (2005-2010) Mheshimiwa alisahau au kuogopa kuwashawishi wenzake waingize suala la mabadiliko ya katiba katika iIani ya uchaguzi wa 2010! Ilikuwa ni baada ya uchaguzi alipokumbushwa na umma umuhimu wa kufanya mchakato wa mabadiliko hayo!!!

Mhe. Zitto ninajua kwamba unafahamu vizuri kwamba 'legacy' haianguki kama mvua (yaani kuja kwa kudra ya Muumba) bali hubuniwa nakusukwa (kama ukuta wa nyumba) kwa kuzingatia hali na mahitaji ya kisiasa, kiuchumi, na kijamii yaliyopo na yanayoweza kutabirika.

Nina imani kwa vile umesisitiza dhana ya kuUTAKA urais basi utakuwa unajiandaa kuingia Ikulu na ajenda kuntu ya kuboresha maisha ya Watanzania na sio kwenda huko kama mtalii. Utangazaji nia kuUTAKA urais uende sambamba na kututangazia 'ajenda kuntu' ili tuijadili.

Tunakutakieni kheri katika azma yako.
 
Hata la Dodoma sio mbaya, tuna majina mazur. Anyway kama wenzangu mmelikubal sawa, ila inaonekana amelicopy Kenya kwenye kipindi flan ambapo huenda likamletea shida hasa pale watu watakapo anza kuchanganya story za kule na huku kwenye mambo tofauti. BIG UP

Ok,kile kinachoitwa makutano junction?
 
Hebu wasiliana na jamaa wa ARUSHA MAMBO.

Huyu jamaa sijui yupo Arusha au wapi ila mara nyingi anaunga vipindi vya TBC na hasa Bunge na kuviweka ONLINE kama Radio maana huwa tunasikia tu sauti ila hatupati picha.

Jamaa yupo pia hapa Jamiiforums na kwenye FACEBOOK: http://www.arushamambo.com ,

Contact: Info@Arushamambo.com

Soma hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/290629-arusha-mambo-live-bunge.html
Kwa sasa ni redioni na maswali yanasomwa hewani lakini ikifikia hatua ya kwenda kwenye TV hapana shaka yatapita maswali/maoni yenu.
 
makutano junction (kenya) Makutano show (Tanganyika) ... wabongo kwa ku-copy
 
makutano junction (kenya) Makutano show (Tanganyika) ... wabongo kwa ku-copy

Kama ni kizuri hakuna shida. Isitoshe Makutano junction ya Kenya na hii ziko tofauti kwa maana ya muktadha. By the way nini kipya duniani kwa sasa? Badala ya kukosoa au kuchangia kuboresha unaanza kukandya!
 
UKIWA MVIVU WA KUFIKIRI UTAONA HAKUNA JIPYA, Ubunifu utatofatiana daima, hapa ni JF siyo FB Ibambasi
 
UKIWA MVIVU WA KUFIKIRI UTAONA HAKUNA JIPYA, Ubunifu utatofatiana daima, hapa ni JF siyo FB Ibambasi

Ok, mwaswali mawili tu; niambie wewe ndio Fina na unataka kuwa na kipindi chenye muktadha wa "Makutano", ni ubunifu gani unafikiria ungeufanya? Pili, FB na mada hii vina uhusiano gani?
 
Ok, mwaswali mawili tu; niambie wewe ndio Fina na unataka kuwa na kipindi chenye muktadha wa "Makutano", ni ubunifu gani unafikiria ungeufanya? Pili, FB na mada hii vina uhusiano gani?
mkuu namashaka na uelewa wako,pole unatakiwa kuwa FB kwa vichwa maji wenzio, ama umesha ndungai?
 
mkuu namashaka na uelewa wako,pole unatakiwa kuwa FB kwa vichwa maji wenzio, ama umesha ndungai?

Sijui hata kama maswali uliyaelewa. Nimekuuliza lakini kila mara unakimbilia kujificha nyuma ya FB. Nakuuliza tena, ni ubunifu gani ambao Fina au wewe ungeuleta ikiwa ungetaka uwe na kipindi chenye muktadha wa "Makutano"?
 
Hata la Dodoma sio mbaya, tuna majina mazur. Anyway kama wenzangu mmelikubal sawa, ila inaonekana amelicopy Kenya kwenye kipindi flan ambapo huenda likamletea shida hasa pale watu watakapo anza kuchanganya story za kule na huku kwenye mambo tofauti. BIG UP

Kile ni MAKUTANO JUNCTION japo ni maana moja lakini limeunganishwa kwa pamoja pia ile kama tamthilia flani
 
Back
Top Bottom