(Video) - Huwezi kuamini hata ukiangalia kwa macho yako mwenyewe!

Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?
viongozi wa serikali ya ccm akili zao zimeganda mkuu na kama wakiendelea kutuongoza nchi itakuwa masikini milele.

hakuna sababu ya kuagiza samaki nje na asante kwa video manake kama usingeweka ningekubishia vibaya sana.hii ni aibu kubwa kwa viongozi wetu,najua hawajali hata kidogo kwa vile wako kwa manufaa yao binafsi na sio taifa.
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?

Mwanakijiji maswali yako yote yana jibu moja '' Sisi na viongozi wanaotuongoza ni mbumbumbu na wajinga''. Hebu niwape tip kidogo, Nyerere alijenga Tanganyika Packers! imekufa, hivi ni kuwa hatuna ng'ombe au hakuna walaji,sasa tunaagiza beef kama zile zile kutoka Brazil!!!!.
Nyerere alijenga Tanzania fisheries, tumeziua na sasa tunaagiza samaki tukiwa na Indian ocean,Tanganyika,victoria,nyasa n.k!!!!!!!
Tumeuza TRL, je ni kuwa hakuna abiria au mizigo? ni ujinga tu, watu wachache wamechukua 10% kuua taifa with impunity.
Alichofanya magufuli ni kuonyesha jinsi gani tulivyokolea usingizi, labda angekuwa na wenzake wawili watatu angefanikiwa lakini angalia cabinet akina SS!!!!!!!!!!!!!!!.
Inasikitisha sana, tuwaeleze watz tunahitaj nchi yetu,tuchukue nchi yetu! there is a window of opportunity, let us try something different! the status quo will never solve our problem. Ni jukumu letu soote kutoa elimu ya umma, tuwaambie wananchi hizi jezi na vitenge vya kijani/njano kw miaka 50 havijatusaidia!
 
......sisi CHADEMA tutaliangalia hilo kwa jicho la tatu na nne na kulikomesha mara moja. Vitu kama vibiriti, tooth pick, nyanya, matunda ya aina zote, vegetables za aina zote, juice za aina nyingi, plastic houseware, nyama, samaki, kuku toka nje tutaviwekea kodi kubwa na kutoa nafuu ya kodi ya mitambo na malighafi ya kutengenezea hizo bidhaa. Hawa CCM ambao kila kukicha wahindi na wafanyabiashara wakubwa wanakimbilia ubunge they never think of mkulima mmatumbi wa nchi hii.

Kaka nashahuri kuwa mutoe kwanza kodi kwenye mitambo then after 2/3 yrs ndio muongeze kodi kwenye hizo imported goods maana na wasiwasi kuwa bei itapanda kwa kuwa kuna uwezekano wavuvi wa ndani hawatoshelezi soko.
 
Nchi hii imekosa wazalendo kiasi cha kusikitisha sana.Washauri wa maswala ya uchumi na biashara za kimataifa kwa wakuu wa nchi hii haijulikani wanafanya nini.Mambo haya yanaendelea kuongeza upungufu tu kwenye fedha za kigeni; na kwa sababu, option waliyonayo wataalamu wetu ni devaluation ili ku cope na Current Account deficit(Balance of Payments) basi shillingi yetu itaendelea kuporomoka ukiilinganisha na dollar ya Marekani; wafanya biashara tulionao ndani wataendelea kupandisha bei kiholela kwa kisingizio cha kuporomoka shilling yetu, bei za mafuta zitaendelea kupanda na huko vijini kwetu wazee watendelea kutokwa na jasho la ugumu wa maisha. Wakati huu wa uchaguzi watahongwa 5,000 au 10,000 ili wawarudishe wabaya wao kwenye madaraka na waendelee kutokwa na jasho la the created ugumu wa maisha.
Siamini kwamba uingizwaji kiholela wa vitu kutoka nje ni kwa bahati mabaya.I am convinced it is a planned process for the benefit of the few.Ni nani mwenye uchungu na nchi hii alazimishe option ya protectionism kwa faida ya wengi?

Waziri wako wa fedha anakuambia ni kwa sababu ya ukame na mtikiso wa soko la dunia, najiuliza hivi sisi huko duniani tunauza nini? mimi nachojua ni kuwa tunauza madini kwa wingi thats all na hizi hela za madini sijuhi kama zinaingia Tanzania na sio Canada/Australia.
 
Tunaagiza samaki kwa sababu hatuna samaki, au tunaagiza samaki kwa sababu hatuna uwezo wa kuvua samaki? au tunaagiza kwa sababu tusipoagiza tutakuwa kama hatuna uwezo wa kuagiza?

Inawezekana tunaagiza kwa sababu tunataka "vionjo tofauti" - Unajua kwa mfano japokuwa tuna process samaki ( kupata minofu) bado eneo hilo lina utata. Fikiria kuna wenye kupenda sushi - iwe tuna, salmon etc. Na kama ujuavyo yahitaji kuliwa ikiwa mbichi. Inawezekana "ubora" kwa maana ya utengenezaji katika hali itakayoruhusu kuliwa ikiwa mbichi na salama bado ni utata.
Tungefafanua uagizwaji/uagijazaji huu unafanyika kwa kila aina ya samaki au kwa baadhi na kwa sababu maalumu? Haitaingia akilini mtu kununua samaki aina ya Sato, Sangara, red snapper etc kutoka nje ilhali wamejaa tele hapahapa nchini.
 
.......Unashangaaa samaki!!! Hii ndio TZ bana kila kitu imported hadi chu.pi. Tena kuna wale samaki kibua wanatoka south Africa ni watamu aiseee hadi basi.
 
Inawezekana tunaagiza kwa sababu tunataka "vionjo tofauti" - Unajua kwa mfano japokuwa tuna process samaki ( kupata minofu) bado eneo hilo lina utata. Fikiria kuna wenye kupenda sushi - iwe tuna, salmon etc. Na kama ujuavyo yahitaji kuliwa ikiwa mbichi. Inawezekana "ubora" kwa maana ya utengenezaji katika hali itakayoruhusu kuliwa ikiwa mbichi na salama bado ni utata.

Inawezekana kuna ukweli.. lakini kwa kuagiza zaidi kutoka nje ndio tunawapa uwezo watu wetu kuimprove utamu wa hawa wa kwetu..

Tungefafanua uagizwaji/uagijazaji huu unafanyika kwa kila aina ya samaki au kwa baadhi na kwa sababu maalumu? Haitaingia akilini mtu kununua samaki aina ya Sato, Sangara, red snapper etc kutoka nje ilhali wamejaa tele hapahapa nchini.

Lakini kama Sato na Sangara wanapewa majina ya kichina si ndo hivyo hivyo..
 
Inawezekana tunaagiza kwa sababu tunataka "vionjo tofauti" - Unajua kwa mfano japokuwa tuna process samaki ( kupata minofu) bado eneo hilo lina utata. Fikiria kuna wenye kupenda sushi - iwe tuna, salmon etc. Na kama ujuavyo yahitaji kuliwa ikiwa mbichi. Inawezekana "ubora" kwa maana ya utengenezaji katika hali itakayoruhusu kuliwa ikiwa mbichi na salama bado ni utata.
Tungefafanua uagizwaji/uagijazaji huu unafanyika kwa kila aina ya samaki au kwa baadhi na kwa sababu maalumu? Haitaingia akilini mtu kununua samaki aina ya Sato, Sangara, red snapper etc kutoka nje ilhali wamejaa tele hapahapa nchini.
Bibie, Sijui kama umeitazama hiyo video na una ujuzi wa kuwatambua samaki. Hakuna samaki kati ya hao hapo ambaye hatuna nchini na hata iwe kutengeneza Sushi, kinachothaminiwa ni ujuzi wa kumtengeneza samaki huyo ili apate kulika akiwa mbichi.. haijalishi ni samaki gani.

Kisha labda nikupe ukweli zaidi ni kwamba samaki anayeingizwa zaidi Tanzania ni Tuna fish ambaye ukiuliza wataalam watakwambia kwamba Kila (All) tunafish wana bacteria ndani ya nyama zao na kama hawakuwa handled correctly husababisha scombroid poisoning, sasa nambie hapo Bongo wanapotengeneza hizo sushi ya Tuna ambaye kaingizwa nchini pasipo kupimwa itakuwaje?.

Bibie, huu uroho na ulimbukeni wa kuiga ndio utakuja tumaliza vibaya sana..
 
hili li nchi linahitaji kiongozi ataketawala kidikteta japo mwaka mmoja watu wachapwe fimbo na kupigwa risasi kwa wanopindisha sheria ndo mambo yataenda sawa, hii tabia ya kuchekeana chekeana kwenye maswala muhimu yanayohitaji umakini na uwajibikaji ndo maana nchi inapelekwa shimoni. inauma sana enyi wenzangu wadanganyika
 
Back
Top Bottom