Elections 2010 Vick Kamata akamata ubunge wa viti maalum!

Mwenye kufahamu tafadhali atoe darasa - Viti maalum ni kwa ajili ya CCM au na vyama vingine? Endapo kikitokea chama tofauti na CCM kikawa na wabunge wengi kuliko CCM hao kina mama na dada zetu waliopita viti maalum bado watakuwa wabunge? Kuuliza si ujinga
 
Ikitokea Chadema wakapita na kushinda uchaguzi mkuu then itakuwaje> Please assist kwa hawa viti Maalum:A S-heart-2:
 
Mwenye kufahamu tafadhali atoe darasa - Viti maalum ni kwa ajili ya CCM au na vyama vingine? Endapo kikitokea chama tofauti na CCM kikawa na wabunge wengi kuliko CCM hao kina mama na dada zetu waliopita viti maalum bado watakuwa wabunge? Kuuliza si ujinga

Itakuwa imekula kwao! But kwa ninavyoijua CCM, hata sheria itapindishwa ilimradi wawemo!
:shock::shock:
 
Hivi tayari kuna washindi au wa ccm mnajipongeza kuvuka mstari wa kwanza; angalia post zenu; hakuna sema anaweza pita kura za maoni ila iso ubunge; una matatizo wewe maana baada ya hapo itategemea kama chama kitashinda kwa asilimia ngapi
 
Ajabu mimi natamani kujua waliokuwa wakishindana ili nijue failures ni kina nani...
 
hivi viti maalum vya ubunge bora vipewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na bila kubagua chama gani wanatoka kuliko kupandikizana bila kunufaisha taifa kwenye kitu chochote zaidi ya kunufaisha matumbo yao.
 
Naomba kueleweshwa... hivi ni kupata ubunge viti maalum au kufuzu kuwani bunge viti maalum?!!
 
Kama Rita Mlaki (kitu ya muzee aliyepita) kapewa Ubunge viti maalumu baada ya kuchemsha ubunge wa kuchaguliwa pale Kawe sichangai na huyu Vicky Kamata ( kitu ya muzee....) akipewa ubunge wa viti maalamu na baadaye uwaziri wa wizara ya iliyokuwa ya Sitta...
 
Ati kuna Watu wamewahi kunyetisha juu ya nasaba:A S-heart-2: za huyu mdada na Mzee wa nyumba tetu. Hii imekaaje??
 
2j2e2xs.jpg
 
'mama wa Kawe ' naye yuko juu!

wa UWT Taifa Mh. Sophia Simba.



Mmoja wa washindi waliochaguliwa,Bi. Ritah Mlaki akishangilia mara baada ya kutangazwa kuwa mmoja wa washindi watano katika Matukio mbalimbali yaliyofanyika jana jijini kwenye uchaguzi wa Wagombea kupitia UWT kwenye mkutano Mkuu Maalum Wa uchaguzi Mkoa wa Dar es salaam uliofanyika kwenye ukumbi wa PTA katika viwanja vya Sabasaba.

Katika uchaguzi huo wajumbe wa UWT waliwachagua wawakilishi wa makundi mbalimbali kwa ajili ya VITI MAALUUM, Mwenyekiti wa UWT Mkaoni Dar es salaam Zarina Shamte Madabida alikuwa mshindi wa kwanza. na kufuatiwa na Ritah Mlaki, Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na Mlezi wa Chama mkoa wa DSM Abdulrahman Kinana, na kuhudhuriwa na MWenyekiti wa UWT Taifa Sophia Simba.


Mgombea wa Viti Maalum Janeth Masaburi akiomba kura kwa wanachama.


Wanachama wakigawiwa karatasi kwa ajili ya kupiga kura.

(picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)​
 
Ila nimeupenda huu utaratibu wa viti maalumu kugawanywa kufuatana na mikoa na makundi maalum ndani ya chama, Chadema iige mfano huu.
 
Back
Top Bottom