vichekesho bongo mmefulia????

ASIKARI

Member
Oct 17, 2012
92
19
nilikuwa napenda sana kuangalia komedi za nyumbani..nilikuwa nafurahi na kucheka sana. kingwendu, bambo, muhogo mchungu, senga mzee majuto nk.
nachoshangaa ni kuwa siku hizi hawa wachekeshaji huwa hawanichekeshi pale ninapo angalia cd zao..sioni nn wanafanya.
je nisuala mradi wawe sokoni ama???? siamni kama naweza angalia komedi nikiwa na stress zangu then ikiisha hakuna kilicho pungua.
WITO ANGU KATIKA WAIGIZAJI WA TASNIA YA UCHESHI...CHONDE CHONDE EMBU KUWENI WABUNIFU WA VICHEKESHO JAMAN.
NA SIO SUALA LA KUTUJAZIA CD MADUKANI
 
Nunua za wanaochekesha mkuu tatizo liko wapi?wabongo tunapnda kulala mika xna.
 
Mimi nikiangalia Comed za bongo Stress ndio zinazidi kupindukia!
 
Original comedy kama wakitulia ndio wenye uwezo wa kuchekesha hasa Joti na siyo hao Zilipendwa, amebaki Mzee Majuto peke yake.
 
Hah sitaki shida nina collection ya Charlie Chaplin, Basket mouth zinanitosha........
 
Na kwa huu ujio wa VINGAMUZI nikiangalia vichekesho vya wenzetu CITIZEN yaani tunachofanya ni aibu tupu......Ila kwa upande wa Televisheni nawatupia lawama wamiliki wa hivi vituo, Hawako tayari kununua UBUNIFU wanataka uje BURE kwa kuwalazimisha hao wasanii wao wafanye wanachoweza na ndio tunachoona kinachofanyika kwenye TV zote za bongo, Wasanii nao wanaishia kufanya kile wanachoweza na kamwe tusitarajie wataenda zaidi ya hapo. UBUNIFU NI GHARAMA jamani. Wamiliki wa vituo wajipange, watafute SCRIPT za vichekesho kwa gharama, Anachofanya BAMBO na wengine ndio wamegotea hapo....
 
ebana kuna vichekesho vinaonyeshwa chanel 5 kila jumatano saa 3 kamili usiku...dah ebana hawa jamaa wanajuwa....kuna mshkaji anaongea kama Yesu ni nooma....
 
hamumjui Kinyambe wa vituko show nyie,yule ni Mr bean iseee.hata asipozungumza utacheka tu
weeee! kinyambe ni another level! yaani huwa siku izi nikiona cd ina picha ya kinyambe tu lazma ninunue maana mambo yake tu yatakuvunja mbavu.
kwa mfano siku moja alikuwa kwa rafiki yake mida ya usiku halafu huko nje mvua inanyesha kinoma. yule rafiki yake akamwambia alale hapo ili asinyeshewe maana sehemu ya kulala ipo. kinyambe alishuruku kupewa sehemu ya kulala na akamuona rafiki yake ni mtu safi sana. sasa cha kushangaza ni kuwa yule rafiki yake alipoenda chumbani kuweka mazingira ya kitanda sawa, kinyambe alikimbia mpaka kwake halafu akarudi akiwa amenyeshewa kishenzi. jamaa lipomuuliza kwa nini amenyeshewa akamwambia alienda kufunga mlango maana palikuwa wazi! can u imagine!
 
ebana kuna vichekesho vinaonyeshwa chanel 5 kila jumatano saa 3 kamili usiku...dah ebana hawa jamaa wanajuwa....kuna mshkaji anaongea kama Yesu ni nooma....

So unafurahia Yesu kuigizwa,Yesu amekuwa kichekesho?Hivi mtume muhamad akiigizwa wale jamaa zetu patakalika kweli?Me huwa naangalia vichekesho vyao,wanafurahisha but yule anayemuigiza Yesu anaomba sh. mia aache aisee inaweza mletea matatizo
 
The issue ni hivi wale jamaa hata hata nyumba zao za Ibada huwezi kuta zinachezewa chezewa kipumbavu pumbavu kama nyumba za hawa wengine.

makanisa yamekuwa ni majumba ya ibada, sambamba na majumba ya kurekodia movie.
Ukishindwa kujiheshimu mwenyewe basi hakuna atakaekuheshimu.

So wacha wamuigize hata anakula vitumbua bila kulipa.
wao wenye nabii wao wameshindwa kumjengea heshima...
 
Na kwa huu ujio wa VINGAMUZI nikiangalia vichekesho vya wenzetu CITIZEN yaani tunachofanya ni aibu tupu......Ila kwa upande wa Televisheni nawatupia lawama wamiliki wa hivi vituo, Hawako tayari kununua UBUNIFU wanataka uje BURE kwa kuwalazimisha hao wasanii wao wafanye wanachoweza na ndio tunachoona kinachofanyika kwenye TV zote za bongo, Wasanii nao wanaishia kufanya kile wanachoweza na kamwe tusitarajie wataenda zaidi ya hapo. UBUNIFU NI GHARAMA jamani. Wamiliki wa vituo wajipange, watafute SCRIPT za vichekesho kwa gharama, Anachofanya BAMBO na wengine ndio wamegotea hapo....

Tom na Jerry zinakufaa kupunguza stress... Jarib.
 
Back
Top Bottom