Valentine's day: Mungu huwaunganisha wapendanao kwa namna ya kipekee sana......

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,161
33,028
Habari za muda huu ndugu jamaa na marafiki wapendwa hapa jamvini........

Leo nimekumbuka kisa cha rafiki yangu mmoja........

Miaka kadhaa nyuma baada ya rafiki yangu kupambana na usafiri wa umma hatimaye Mungu alimjaalia akapata kipando Cha miguu miwili(piki piki) Tulilipokea kwa furaha huku nikimsisitiza awe makini barabarani kwa maana kuna ajali nyingi sana za piki piki.......

Baada ya masiku mengi kupita huku rafiki yangu akifurahia usafiri wake ambao kwa kiasi kikubwa umemrahisishia sana maisha na kipindi chote alikuwa hajaoa......Siku moja jioni nilipokea simu yake, aliniambia amepata ajali, amemgonga mtu na kumvunja mguu maeneo ya Tabata........nikalazimika kukodi piki piki ili kuwahi eneo la tukio maana kwa namna alivyokuwa ANAONGEA nilihisi usalama wake upo hatarini........

Nilipofika pale nikamkuta amemgonga Binti ambaye alikuwa anapitia pembeni ya barabara.......na alikuwa na Hali mbaya..... Tukampeleka yule binti hospital na piki piki ikapelekwa polisi..... Tulifaniikiwa kukamilisha taratibu za matibabu na jamaa aliahidi kumuhudumia yule binti mpaka atakapo pona.....

Kwa kifupi zile pirika pirika za kumuhudumia, kumjulia hali pale kwao mpaka kupelekea binti kupata nafuu.....ikapelekea wawili hawa kuzama penzini.....na baada ya binti kupona kabisa ikaanza mipango ya ndoa....... Na mpaka leo hii mwaka wa sita wanaishi pamoja kwa amani na ndoa yao imejaa furaha.....

Happy Valentine's day wapendanao wote........

1644567736481.png
 
imenisisimua, very touching and lovely,,May God continue showering blessings on their marriage.
 
Sasa Valentine's iliwakutanishaje?alimgonga siku hiyo?
Hapana sikumaanisha kwamba valentine ndio imewaunganisha.....Bali nimekumbuka historia yao nzuri ya chimbuko la penzi lao.....bahati nzuri kumbukumbu zangu zimewiana na muda wa valentine......
 
Back
Top Bottom