neno ni upanga
Senior Member
- Jun 28, 2022
- 189
- 725
Habari wapendwa!
Watu wengi wanacheza na dhambi ni kwa sababu hawajui jinsi mbinguni kulivyo! Leo nitawatazamisha jinsi mbinguni kulivyo baada ya hapo utaamua mwenyewe kuendelea na dhambi au kwenda huko
Kutokea uso wa nchi hii kwenda juu kuna mbingu ya tatu, isiyoonekana kwa macho ya nyama, hiyo ndio mbingu nataka kuielezea hapa!( Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
2 Wakorinto 12:2)
Hizi ni sifa za hii mbingu
1: ni makao ya Mungu
2: hakuna usiku ;(
Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.
Ufunuo 22:5)
3: hakuna maumivu, wala kilio, wala maangaiko ya aina yoyote(
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Ufunuo 21:4)
4: Chochote kilicho mbinguni kinaishi milele (nao watatawala hata milele na milele.
Ufunuo 22:5D
5: mbinguni kuna malaika wasio na idadi (Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,
Waebrania 12:22
6: mbinguni kuna magari yasio kuwa na idadi (Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu; Bwana yumo kati yao kama katika Sinai, Katika patakatifu.
Zaburi 68:17)
7: mbinguni barabara zake ni za kioo kiangavu (Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu. Ufunuo 21:21)
8: mbinguni kuna majengo makubwa sana na mengi sana (Na ule mji ni wa mraba, na marefu yake sawasawa na mapana yake. Akaupima mji kwa ule mwanzi; ulikuwa kama maili elfu na mia tano; marefu yake na mapana yake na kwenda juu kwake ni sawasawa.
Ufunuo 21:16
Note: kujua hesabu hii fanya hivyi
1mile =1.6093km
1500mile=?
= 1500mile×1.6093km/1mile
=2413.93km
Maanake jengo moja mbinguni urefu wake kwenda juu ni sawa na kutoka Lusaka Zambia kwa kupita mbeya mpaka nairobi Kenya!
9: mbinguni majengo yake yamejengwa kwa Vito vya thamani ya hali juu! madini ya thamani (Na misingi ya ukuta wa mji ilikuwa imepambwa kwa vito vya thamani vya kila namna. Msingi wa kwanza ulikuwa yaspi; wa pili yakuti samawi; wa tatu kalkedoni; wa nne zumaridi; wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa kenda yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.
Ufunuo 21:19-21
10: mbinguni kuna matunda ya kila namna na yenye Ladha nzuri isiyolinganishwa na chochote hapa duniani( katikati ya njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. Ufunuo 22:2
11: mbinguni kuna kila aina ya chakula unachokijuq cha hapa duniani na kisichokuepo hapa duniani( Naye akaniambia, Andika, Heri walioalikwa karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu.
Ufunuo 19:9
12: mbinguni kuna aina mbalimbali za juice kuliko za hapa duniani
13: mbinguni kuna mito mizuri ya kuogelea na inayotiririsha maji ya uzima
14: mbinguni kuna wanayama mbalimbali na wazuri wa kupendeza
15: mbinguni kuna bustani nzuri sana na yenye hewa nzuri kuzidi hizi za duniani unazozijua wewe!
16: mbinguni kuna miji mikubwa mbalimmbali na nyenye kujengwa kwa almasi na dhahabu tupu!
Hizi ni sifa chache kati ya sifa za mbinguni ambazo zijazieleza, kutokana uzuri na furaha ya mbinguni, muda wote watakaoingia mji huu watakuwa wanamsifu Mungu kwa kuwaokoa kutoka kwenye moto wa jehanum na kuwaleta kwenye raha ya milele
Utafika mbinguni kama wewe ni mtakatifu na umemwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako.
Yesu anasema"
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.,Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.Yohana 14:1-4
Muendelezo soma: SEHEMU YA 2: Uhalisia wa Kuzimu (Reality of Hell)