Uzinzi si jambo jema, nimekosa cha kumshauri huyu ndugu

Trubetzkoy

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
298
542
Habari!

Picha linaanza kwa kumuangazia bwana X ambaye kutokana na tabia yake ya uzinzi imekuwa ni kawaida kwake kutamani kila mwanake anayekatiza mbele ya macho yake. Hali hii imemfanya awe na orodha ndefu ya wanawake alioshiriki nao tendo la ndoa na mara nyingi akishamnyandua mwanamke huwa hamrudii tena mwanamke huyo.

Ilitokea siku moja jamaa alimnyandua binti fulani na kama ilivyo kawaida yake baada ya mnyanduo jamaa akakata mawasiliano na huyo binti japo walikuwa wakionana mara kadhaa ila hakukuwa na stori zaidi ya salamu.

Miezi takribani kumi baada ya kukutana kimwili jamaa anapigiwa simu na yule dada, dada anadai amejifungua na mtoto ana umri wa wiki moja kwahiyo binti anachohitaji ni jamaa apendekeze mtoto apewe jina gani.

Taarifa hii si tu ilimshitua jamaa bali ilimkasirisha pia. Alipouliza hili linawezekanaje na kwanini binti hakutoa taarifa ya ujauzito wake badala yake amekaa kimya kipindi chote cha ujauzito na amekuja kutoa taarifa mtoto kashazaliwa, binti anadai ooh! niliogopa kukwambia nilihisi pengine ungeniambia nitoe na mimi kutoa mimba siwezi naogopa. Jamaa akachanganyikiwa akamwambia binti kwa sasa siwezi kukujibu chochote kwa sababu taarifa imekuwa ya ghafla sana.

Baada ya hapo jamaa akaamua kufanya ujasusi na hatimaye aligundua kuwa miezi michache baada ya kukutana kimwili na yule binti, binti aliolewa na mshkaji mwingine na kipindi chote hicho muoaji hakujua kuwa mkewe ni mjamzito. Muoaji amekuja kushtuka tumbo limeshakuwa kubwa na hapo hapo wakaongozana kwenda hospitali ambapo ilibainika mimba imeshakuwa kubwa na kwamba muda wowote binti angeweza kujifungua.

Jamaa(mume) baada ya kupata maelezo hayo ya kitabibu ilibidi aitishe wana ukoo kwa ushauri zaidi. Haikupita wiki moja binti akajifungua. Mume wa binti hakuweza kumsaidia binti kwa chochote badala yake alimfungashia kila kilicho chake na kumtimua.

Ndugu yangu (mzinzi) baada ya kupata taarifa hizo za kijasusi aliweka msimano kwamba huyu mtoto sitahusika naye kwa lolote, lakini ulipopita mwezi mmoja tangu kuzaliwa mtoto, mzinzi alitumiwa picha ya mtoto ambaye mama yake na ndugu wengine walidai kuwa mtoto kafanana naye(kafanana na mzinzi). Mzinzi alipotazama picha, kwa kiasi fulani mtoto kafanana naye. Sasa kaja kuniomba ushauri kwamba je, katika mazingira kama hayo amkubali mtoto au abaki na msimano wake wa awali?

Naomba mnishauri ili nikamshari mwana.
 
Kama Kuna kitu wanaume inabidi tukae na tupeane somo ni kuhusu watoto.. Unawezaje kujifikiria kumkubali au kumkataa mwanao?

Wanaume wa zamani walikua wanasita kukubali watoto kwa sababu vipimo vya kuthibitisha ilikua shida, sasa hivi vipimo vipo, mechi umepiga vizuri, unapata wapi ujasiri wa kukataa damu yako? Ngoswe.
 
Akubaliane na matokeo. Kama ameshakwisha kuoa, amjulishe mwenzake na kumtaka radhi kwa hiyo ajali.

Baadae sasa atoe huduma kwa huyo mzazi mwenzie. Mwambie asipende kukataa watoto hata iwe nini maana mtoto au watoto ni baraka.

Yeye ni baraka; asimkoseshe mwingine kuwa baraka katika maisha yake.
 
Akubaliane na matokeo. Kama ameshakwisha kuoa, amjulishe mwenzake na kumtaka radhi kwa hiyo ajali.

Baadae sasa atoe huduma kwa huyo mzazi mwenzie. Mwambie asipende kukataa watoto hata iwe nini maana mtoto au watoto ni baraka.

Yeye ni baraka; asimkoseshe mwingine kuwa baraka katika maisha yake.
Asante kwa ushauri, naendelea kupokea ushauri then nitampelekea achukue ule utakaokuwa unamfaa
 
Habari!

Picha linaanza kwa kumuangazia bwana X ambaye kutokana na tabia yake ya uzinzi imekuwa ni kawaida kwake kutamani kila mwanake anayekatiza mbele ya macho yake. Hali hii imemfanya awe na orodha ndefu ya wanawake alioshiriki nao
Amkubali mwanae, amtunze vema kabisa Kwakumpa mahitaji yote muhimu. Mtoto Hana kosa.
 
Kama Kuna kitu wanaume inabidi tukae na tupeane somo ni kuhusu watoto.. Unawezaje kujifikiria kumkubali au kumkataa mwanao?

Wanaume wa zamani walikua wanasita kukubali watoto kwa sababu vipimo vya kuthibitisha ilikua shida, sasa hivi vipimo vipo, mechi umepiga vizuri, unapata wapi ujasiri wa kukataa damu yako? Ngoswe.
Nasikia hivyo vipimo ni ghali sana kiasi kwamba si kila mtanzania anaweza kupata hiyo huduma
 
Back
Top Bottom