Uzinduzi wa Tawi la CCM Helsinki - Finland

Kibunango

Platinum Member
Aug 29, 2006
8,420
2,271
WanaCCM na Wapenzi wa CCM nchini Finland wanatarajia kufungua tawi la kwanza nchini Finland katika mji mkuu wa nchi hiyo Helsinki. Wananchama, Wapenzi na Washabiki wa CCM wote katika Finland na nchi jirani mnakaribishwa katika tukio hilo adhimu litakalofanyika katika siku ya Ijumaa ya tarehe 25.06.2010

Kwa habari zaidi tafadhali gonga hapa

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Kibunango,
Naona umehamia Finland. Anzisheni matawi hadi Azerbaijan. Kigumu chama chenu.
 
Kaka kibunango ni mwenyeji wa miaka mingi mno Tampere na Helsinki....Ndio vigogo wa huko...walinipa mapokezi mazuri sana miaka fulani

Omarilyas
 
Kamanda Jasusi:
Kama upo ukanda huu wa Kaskazini karibu sana kwenye uzinduzi wa tawi hili la CCM.

Maendeleo ya Wananchi yataletwa na Wananchi wenyewe.
 
Kaka kibunango ni mwenyeji wa miaka mingi mno Tampere na Helsinki....Ndio vigogo wa huko...walinipa mapokezi mazuri sana miaka fulani

Omarilyas
Mkuu Omarilyas:
Karibu tena Helsinki... Tupo Pamoja!
 
Kibunango karibu tena JF. Nakumbuka uliaga kuwa hatutakuona tena. Karibu. Jukwaa lile lingine bado linahitaji msaada wako!:A S-rap:
 
Nilikuwa bado natafakari nchi ya kwenda kutafutia maisha na wengi walinishauri nikajaribu Scandinavia hasa Finland, lakini kwa hali hii, naona maisha huko ni magumu kuliko Bongo, ukishaona vijana wa kibongo wanapeleka siasa za CCM majuu kuna ujumbe mmoja tu unaoweza kuuona; nchi hiyo ni ngumu na njia pekee ya kujikwamua ni kuingia kwenye utapeli wa kisiasa. Najua wengi hawatakubali conclusion yangu, lakini jaribuni kuangalia timu nzima ya tawi la CCM-UK halafu mniambie ni wangapi wameenda shule na wanafanya kazi za kueleweka....katika hali hiyo hiyo ningemuomba Kibunango anisahihishe kama katika timu hiyo ya CCM-Helsinki kama kuna wajumbe wenye muelekeo wa kimaisha hapo Finland....sidhani kwa sababu kama wangekuwepo wasingejiingiza humo.
 
Shukrani Mkuu, ama kwa hakika sikusema kuwa sitaonekana tena, zaidi kwa habari adhimu kama hii ya uzinduzi wa tawi la chama tawala, nimeona nawajibika tena kuitoa hapa JF, eneo muhimu kwa watumiao forums.
 
Nilikuwa bado natafakari nchi ya kwenda kutafutia maisha na wengi walinishauri nikajaribu Scandinavia hasa Finland, lakini kwa hali hii, naona maisha huko ni magumu kuliko Bongo, ukishaona vijana wa kibongo wanapeleka siasa za CCM majuu kuna ujumbe mmoja tu unaoweza kuuona; nchi hiyo ni ngumu na njia pekee ya kujikwamua ni kuingia kwenye utapeli wa kisiasa. Najua wengi hawatakubali conclusion yangu, lakini jaribuni kuangalia timu nzima ya tawi la CCM-UK halafu mniambie ni wangapi wameenda shule na wanafanya kazi za kueleweka....katika hali hiyo hiyo ningemuomba Kibunango anisahihishe kama katika timu hiyo ya CCM-Helsinki kama kuna wajumbe wenye muelekeo wa kimaisha hapo Finland....sidhani kwa sababu kama wangekuwepo wasingejiingiza humo.
Kamanda, conclusion yako kwa mtazamo wangu wa wengine waishio hapa Finland nadiliki kusema ni butu. Zaidi karibu sana Finland!

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Yeyote anayeshabikia CCM, anashabikia ufisadi na ulaji...hakuna lingine zaidi. Wanaoshabikia CCM kwa sasa sijawasikia hata siku moja wakiongea hoja ambazo zitasaidia kumkomboa Mtanzania. Hoja yao kubwa ni kulinda maslahi ya CCM (pamoja na yao), na kujenga dynasties ambazo zitawalinda wazazi wao pindi watakapokuwa hawapo katika madaraka. CCM badala ya kuwa Chama cha kuleta mapinduzi kwa wananchi, kimekuwa chama cha kuleta mapinduzi kwa mabepari, mabepari tawala na vibaraka wao. Ni wakati sasa vijana, hasa wasomi kusimama kidete, bila kuwa na woga au kujali maslahi yao binafsi, na kutetea wananchi na taifa la Tanzania. Tusipofanya hivyo tunajikuta tunatawaliwa na kunyonywa daima na vizazi vijavyo vitokanavyo na uongozi mbovu wa sasa.
 
Yeyote anayeshabikia CCM, anashabikia ufisadi na ulaji...hakuna lingine zaidi. Wanaoshabikia CCM kwa sasa sijawasikia hata siku moja wakiongea hoja ambazo zitasaidia kumkomboa Mtanzania. ...
"Maendeleo ya Wananchi yataletwa na Wananchi wenyewe." Kauli hii inatosha kutoa tongotongo kwenye jicho lako.
 
Umesema sawa kabisa. Kweli tumejaa matongotongo, sio katika macho yetu tu, hata katika kumbukumbu zetu. Usemi huo ulioutoa umenakili kutoka kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye kwangu mimi ni kiongozi bora kuliko wote waliotokea Tanzania mpaka sasa. CCM imesahau maadili ya chama yalivowekwa wakati wa uongozi wa Mwalimu na kukumbatia udhalimu usio kifani. Kila mtu anaweza kunukuu hoja mbali mbali zilizotolewa na Mwalimu, na kuzigeuza kwa faida yake, lakini ukweli unabakia palepale...udhalimu ambao CCM unawafanyia wa Tanzania hauna kifani. Kuna haja ya wananchi kufuta tongotongo zetu na kuacha kuwashabikia watu ambao ndio chanzo cha mauti yetu, (I mean literally, mauti yetu!!)
 
CCM ni sehemu ya kuwezesha wenye nia ya kuendelea kufikia lengo yao. Ndio maana nikasema kuwa maendeleo ya mtu yanatokana na fikra zake binafsi. Uwezi kuja hapa na kulaumu eti CCM inashindwa kuleta maendeleo!

Karne hii inaangalia zaidi mawazo ya chini, ambayo ni ya wananchi. Siku za kuwapangia maisha wananchi zimekwisha! Ni wajibu wa kila mwananchi kujua anataka nini!

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
 
Na kweli CCM inasikiliza maoni ya wananchi. Bongo tambarare. Hongereni sana.
 
CCM ni sehemu tu ya kuleta maendeleo kwa wananchi. Ila ni wajibu wa kila mwananchi kujua nini atahitaji ili kuendelea.
 
MABADILIKO YA UKUMBI NA TAREHE

KUTOKANA NA SABABU NJE YA UWEZO WETU TUMERUDISHA NYUMA SIKU MOJA YAANI ALHAMISI BADALA YA IJUMAA AMBAYO NI SIKUKUU MUHIMU HAPA FINLAND (MID-SUMMER-JUHANNUS) KUTAKUWA NA SHIDA YA USAFIRI. PIA KUTOKANA NA KUPOKEA EMAILS NYINGI ZA WASHIRIKI KAMATI YA MAANDALIZI IMECHUKUA UKUMBI MKUBWA NA WA KISASA PALE PALE KATIKATI YA JIJI LA HELSINKI-RAVINTOLA KAISANIEMI (THE HOME OF AFRICAN NIGHT) KAISANIEMENTIE 6.

TAREHE: ALHAMISI 24.6.2010
MUDA: 18.00pm -23.30pm
BAADA YA MKUTANO: KUTAKUWA NA BURUDANI YA NYIMBO ZA KINYUMBANI TU NA DJ. ALTUNEZ.
KWA WALE WANAOJISIKIA KUJA KUFAHAMIANA NA WATANZANIA WENZAO, TUTAKUWA NA MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA BAR KUWA WAZI KWAAJILI YA VINYWAJI BAADA YA MKUTANO 21:00.

NB: WANAWAKAMATI WANAFANYA MAWASILIANO NA BALOZI WETU WA SWEDEN AU MWAKILISHI WAKE ILI AWEZE KUWA MGENI RASMI KWAAJILI YA UFUNGUZI.

:mmph:Je huyo Balozi au Mwakilishi wa serikali ya Jamhhuri ya Muungano wa Tanzania anayekuja kutoka Sweden katika uzinduzi wa tawi hilo anatumia fedha za Jamhuri au za CCM?
 
Nilikuwa bado natafakari nchi ya kwenda kutafutia maisha na wengi walinishauri nikajaribu Scandinavia hasa Finland, lakini kwa hali hii, naona maisha huko ni magumu kuliko Bongo, ukishaona vijana wa kibongo wanapeleka siasa za CCM majuu kuna ujumbe mmoja tu unaoweza kuuona; nchi hiyo ni ngumu na njia pekee ya kujikwamua ni kuingia kwenye utapeli wa kisiasa. Najua wengi hawatakubali conclusion yangu, lakini jaribuni kuangalia timu nzima ya tawi la CCM-UK halafu mniambie ni wangapi wameenda shule na wanafanya kazi za kueleweka....katika hali hiyo hiyo ningemuomba Kibunango anisahihishe kama katika timu hiyo ya CCM-Helsinki kama kuna wajumbe wenye muelekeo wa kimaisha hapo Finland....sidhani kwa sababu kama wangekuwepo wasingejiingiza humo.
Du shule na ccm vina uhusiano gani????kwani wanachama wa ccm wanahitajika kuwa na elimu ipi???
 
Back
Top Bottom