Uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign - Sheria ya Ardhi ni ya Mwaka 1999 na Sio 1995

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi
Naangalia TBC mubashara uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign,
Screen Shot 2023-02-15 at 12.16.39 PM.png
Screen Shot 2023-02-15 at 12.16.52 PM.png
Screen Shot 2023-02-15 at 12.21.12 PM.png
Screen Shot 2023-02-15 at 12.21.26 PM.png

Katika ufuatiliaji wa uzinduzi huu mubashara kupitia TBC, kukatokea jambo fulani,
kuna kiongozi mmoja mkubwa ambaye pia ni mwanasheria mbobezi na mbobevu akiwa live Mubashara kupitia TBC, ameitaja sheria ya Ardhi No. 4 ya mwaka 1999 na Sheria ya Ardhi ya Vijiji No. 5 ya mwaka 1999, kiongozi huyo amesema ni sheria za mwaka 1995!.

Silitaji jina la kiongozi huyo kwasababu I know it's just a slip of a tongue, bandiko hili linaulizia Watanzania tuendelee kuvumilia hizi slips of a tongue kwa wanasheria wetu mpaka lini?. Jee unajua kuwa besides a slip of a tongue kuna a slip of a pen?, hadi slip of sheria hadi a slip of katiba?.

Viongozi wetu ni binadamu na sio malaika hivyo wanayo haki ya kukosea ikiwemo a slip of a tongue, lakini kwa mwanasheria mbobezi mbobevu kusema sheria ya Ardhi ni ya mwaka 1995!, hili sio dogo!.

Naendelea huku nikiwasisitiza wale wenye access na TBC fuatilieni...

  1. Hizi slips of a tongue kwa wanasheria wetu wabobezi na wabobevu haziishii kwenye ulimi tuu, katiba yetu ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume na katiba ni sheria batili!, lakini wanasheria wetu hawa hawa wabobezi na wabobevu wamefanya slip of a pen, wakatunga sheria batili ya uchaguzi inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT!.
  2. Sheria hiyo batili ikaingia Bungeni mwetu na Bunge na wanasheria wetu wabobezi na wabobevu wakapitisha sheria batili hiyo hivyo wao kutunga sheria batili kinyume cha katiba!.
  3. Na baada ya Bunge kuitunga, rais wetu nae wa wakati huo akaisaini sheria batili hiyo na kuanza kutumika!, na mpaka leo sheria batili hiyo bado ipo na inaendelea kutumika!.
  4. Mchungaji Mtikila (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi) akafungua shauri Mahakama Kuu ikaitangaza sheria hiyo ni batili ifutwe kwasababu iko kinyume cha katiba!.
  5. Serikali ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, na kwa vile sheria hii iko kinyume cha katiba, serikali ikaamua kufanya mabadiliko ya katiba, sheria hiyo batili ikachomekewa ndani ya katiba, hivyo sheria hiyo sasa sio kinyume na katiba ni kimbele na katiba!. Hii ni slip of a tongue kwa katiba yetu!.
  6. Mtikila akafungua kesi nyingine Mahakama Kuu kupinga mabadiliko hayo haramu ya katiba na Mahakama Kuu yenyewe haikuwa na a slip of a tongue!, ikatamka mabadiliko hayo ya katiba ni haramu!.
  7. Serikali ikakata rufaa Mahakama ya Rufani Tanzania nayo ikafanya a slip of a tongue, ikatamka kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, kama Bunge limetunga sheria batili, uwezo wa Mahakama Kuu ni kusema tuu Kuu sheria hiyo ni batili lakini sio kuibatilisha!.
  8. Na kwa vile ubatili huu sasa umechomekewa ndani ya katiba ya JMT, then ubatili huo ni over and above uwezo wa Mahakama na mamlaka ya kuingilia kifungu chochote cha katiba kwasababu Mahakama iko chini ya katiba, hivyo huo ubatili uliochomekewa na Bunge ndani ya katiba lazima uchomolewe na Bunge lenyewe lilichomeka!.
  9. Kwa ufahamu wangu kwa kuvaa viatu vya nia ya mtunga katiba, alidhamiria nini aliposema sheria yoyote unapokweda kinyume cha katiba, sheria hiyo inakuwa ni batili, alidhamiria ubatili huo ni ubatili ni ubatili wa void ab initio!. Unapokuwa na ubatili wa void ab initio, tangu ubatili huo unapotamkwa kuanzia pale pale ubatili huo unakuwa ni ubatili ab initio kuanzia pale pale!.
  10. Mpaka hapa ninapoandika leo, hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu ubatili huu ipo na hakuwahi kubatikishwa, ubatili huu bado upo ndani ya katiba yetu, hivyo tuna ubatili huo umo ndani ya katiba yetu!.

Wanasheria hawa, ndio waliotufikisha hapa!, jee tuendelee kuvumilia hizi slips of a tongue kwa wanasheria wetu manguli wabobezi na wabobevu hawa mpaka lini?.

Ushauri Wangu kwa Kampeni Hii
Mimi kama mtu wa habari na publicity, kampeni hii ni jambo jema, jambo kubwa na jambo zuri, tatizo ni Watanzania wengi hawajui haki zao, hivyo nashauri, watekelezaji wa kampeni hii, waandamane na media kila waendapo, media itangaze kila kinachofanyika, sio tuu ili kuhamasisha watu wajitokeze kwa wingi, bali pia kutoa fursa ya kutoa elimu ya sheria na elimu ya haki kwa Wananchi.

Mimi kwa upande wangu, mara moja moja nitakuwa nawarusha kwenye kipindi changu hiki
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=nCGmC4ZFaUcLXiN-
Karibuni
Paskali
 

Attachments

  • Screen Shot 2023-02-15 at 12.20.28 PM.png
    Screen Shot 2023-02-15 at 12.20.28 PM.png
    84.4 KB · Views: 4
Mkuu sheria zetu zinabadilika kila mara, utashi wa raisi anaweza kubadilisha sheria yoyote hata vifungu vya katiba. Usimlaumu huyo jamaa maana kwa jinsi sheria za tanzania zinavyobadilishwa hovyo hovyo hata computer haiwezi kukumbuka
 
Wanabodi,

Naangalia TBC mubashara uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign, kuna kiongozi mmoja mkubwa ambaye pia ni mwanasheria mbobezi na mbobevu akiwa live Mubashara kupitia TBC, ameitaja sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ni sheria za mwaka 1995! Japo I know it's just a slip of a tongue, kwasababu Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji ni sheria za mwaka 1999!

Viongozi wetu ni binadamu na sio malaika hivyo wanayo haki ya kukosea ikiwemo a slip of a tongue, lakini kwa mwanasheria mbobezi mbobevu kusema sheria ya Ardhi ni ya mwaka 1995!, hili sio dogo!

Naendelea huku nikiwasisitiza wale wenye access na TBC fuatilieni

P
Hahah tufatilie nini ikiwa wazungumzaji hawajui hata mwaka ulioanzishwa the Land Act Cap 113?labda alikuwa anarefer land policy
 
Labda ilianzishwa 95 ikaja kupitishwa 99.. ndio nmemuelewa hivyo
Sheria inatajwa kwa mwaka iliopitishwa!, na sheria japo zipo nyingi, lakini hazifanani, sheria ya Aridhi No. 4 ya mwaka 1999 na sheria ya Aridhi ya Vijiji No 5 ya mwaka 1999, ni sheria muhimu sana, a slip of a tongue kuuita sheria ya Ardhi ya mwaka 1995, can be tolerated kwa watu wa kawaida!, not kwa kiongozi, mwanasheria mbobezi, mbobevu!.

Hata katiba, inatajwa kwa mwaka wake katiba ya JMT ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, akitokea kiongozi akasema katiba ya JMT ya mwaka 1975, it's awkward!.
P
 
WHO IS THAT? HUWA SIANGALII TBC, HAINA MAANA KUIANGALIA MAANA HAWATASEMA UKWELI. ONA HUYO SASA ETI 1995! NDIO ZAO SI SLIP OF A TONGUE! :D :D :D :D
GT don't discuss people!, hapa nazungumzia a slip of a tongue!.
Angalia TBC ndio TV yako unayo igharimia!.
P
 
Mkuu sheria zetu zinabadilika kila mara, utashi wa raisi anaweza kubadilisha sheria yoyote hata vifungu vya katiba. Usimlaumu huyo jamaa maana kwa jinsi sheria za tanzania zinavyobadilishwa hovyo hovyo hata computer haiwezi kukumbuka
Duh...!.
P
 
You can't be serious, tuangalie TBC, labda kama wanaonyesha mpira.
Kwenye marekebisho ya sheria ya habari, tutapendekeza Watanzania tuanze kukatwa Radio Levy kama SDL, watu mkatwe, mchangie, mjisikie ni redio au TV yenu, hata msipoitazama au kuisikiliza, then its ok maana hela yako tunatumia.
P
 
Kwenye marekebisho ya sheria ya habari, tutapendekeza Watanzania tuanze kukatwa Radio Levy kama SDL, watu mkatwe, mchangie, mjisikie ni redio au TV yenu, hata msipoitazama au kuisikiliza, then its ok maana hela yako tunatumia.
P

Pendekezeni tukatwe hata laki kwa siku, lakini hatutakuwa na muda kusikiliza wala kujivunia huo uchafu.
 
Back
Top Bottom