Uzi maalumu wa kuwa enzi marafiki wa ukweli ambao hatuwezi kuwasahau kamwe!

vanus

JF-Expert Member
May 27, 2017
1,148
2,841
Katika harakati za maisha tunakutana na watu wa kila namna, ni bahati sana kukutana na rafiki wa ukweli ambae yupo tayari kujitoa kwa hali na mali.

Kama ni mpenzi wa miziki ya Hip hop utasikia wasanii wakiwataja marafiki zao walio kufa au ambao bado wapo hai, na wengine wakitengeneza kumbukumbu za picha kwenye cheni za dhahabu kuonyesha appreciation, au kama ni mpenzi wa social network lazima utakuwa ushakutana na neno Real G au my G! hao ndo watu ambao naongelea mimi.

Rafiki ambae hata mkigombana haweki kinyongo wala kisasi moyoni, baada ya dakika kadhaa maisha yanaendelea.

Rafiki ambae kutoa msaada kwako ni swala la kufumba na kufumbua macho

Rafiki ambae ni mtu wa karibu sana kwako ni zaidi ya ndugu kwako, yupo tayari kukutetea madhaifu yako mbele ya watu.

Kupitia uzi huu tuwa enzi marafiki wa ukweli au Real G's ambao wanaishi kwenye mioyo yetu, haijalishi tupo nao mbali au tayari wamekufa.

Ingependeza kama tungeelezea namna tulivyokutana na hawa marafiki zetu wa ukweli na kutoa appreciation.
 
Kipindi nasoma advance level nilikuwa, nalala kwenye bweni lenye mchanganyiko wa O-level na A-level tulikuwa tunalala na madogo.

Nilikuwa mtu wa gambe ila weekend tu, shule haikuwa na fence hivyo swala la kutoroka kwenda ambiance/kona bar ilkuwa ni swala rahisi sana.

Kuna mwamba mmoja wa form 6 Alikuwa ni mtu wa tungi sana na mgomvi sana ila kwa muonekano wa nje amekaa kibishoo sana huwezi kumzania ni mtu wa matukio, hakuwa rafiki yangu wala hatukuwa na mazoea ya karibu.

Siku moja amerudi bwenini kalewa sana, yupo tungi si mchezo akawasha taa ya bweni kibabe kila mtu akakereka ila tukavunga kwasababu ya ugomvi wake

akasogea karibu na madogo wa form 1 akaanza kuwaamsha kwa vibao eti waende wakasome wakati muda huo ni saa 8 kasoro usiku, aliwapiga sana madogo vibao wakaanza kulia.

uvumilivu ulinishinda sana nikamwambia achana na madogo walale na usirudie tena kuwapiga, mwamba baada ya kusikia hivyo akanisogelea mpaka kitandani kwangu akaniambia kwani wewe unatakaje?

Mimi sinaga maswala ya kuanza kusutana hapo hapo nikarusha ngumi, mwamba akavua t-shirt kuashiria yupo tayari kwa mapambano.

asee tulipigana sana pale bwenini, pigana sana watu walikuja kuamua lakini wapi unaekuja kuamua ukikaa kizembe unakutana na ngumi au teke, tulipigana sana pale bwenini wanafunzi wote wakakimbia nje wakawa wanachungulia kwa dirishani

Baada ya president wa shule kuja kutuamua tukaachana na ugomvi wale wanafunzi wote wakarudi bwenini.

yule mwamba akinifata tena pale kitandani kwangu akaniambia njoo nje man tuongee wala sikuwaza nikajua game inaendelea leo mpaka asubuhi.

kufika nje jamaa akaniambia fanya kama unasahau yalitokea ni pombe tu, nikamwambia naelewa sana kamanda usijali yamekwisha.

jamaa akaondoka usiku ule bwenini akaenda town kunywa pombe, hakulala pale bwenini usiku huo.

kesho yake mida ya mchana jamaa alirudi shuleni na kuku wa kukaanga na ndizi rost akanikabidhi akaniambia wewe ni ndugu yangu kula, sikuamini kama yule mshikaji mgomvi anaweza kufanya kitu kama kile.

Tokea hiyo siku tulikuwa marafiki wakubwa sana pale shuleni, tukawa tunaitwa wanajeshi wawili.

Yule mwamba alikuwa ananikubali sana mpaka leo hii, tumefanya mambo makubwa sana mengi siwezi elezea yote.

Tumeishi vizuri sana na huyu master kuna kipindi kwao alifukuzwa kwa ajili ya pombe na matumizi mabaya ya pesa.

Nikamvuta mpaka mbezi kwa mama mdogo wangu tukawa tunaishi nae nyumba ya wanaume kwa siri maana bi mdogo ni mnoko sana, nikawa naiba chakula tunakuja kula wote na mwanangu.

Leo hii jamaa ana maisha yake safi bado tunasaidiana na kukutana mara kwa mara.

Ishi sana Real G!
 
Ishi sana Real G Nick!
Hongera sana
 
naam wapo watu waliocha kumbukumbu nzuri kwenye maisha yetu hatukua na nasaba nao isipokuwa tumekutana katikati ya utafutaji wa maisha, wakawa sehemu ya maisha yetu na kuwa sababu ya kupunguziwa uzito kwenye magumu na changamoto tunazokutana nazo pasipo kutarajia wao kupata chochote kwetu, hao tunaweza kuwaita kwa lugha rahisi marafiki wema.
mwenyezi Mungu awe nao kila siku watu wa namna hio, nami najitahidi kadri ninavyo weza kuwa rafiki mzuri kwa yoyote niliyejaliwa awe hivyo, ingawa ni vingumu kulingana na mfumo wa maisha na ule udhaifu wetu binadamu wa ubinfsi lakini natumaini kati ya watu kumi niliokutana nao hawatakosekana watatu ambao nimekuwa kumbukumbu nzuri kwao, najitahidi walao nifike nusu.
 
Nina tatizo flani linanifanya napata seizures kama mtu mwenye kifafa.

Sasa kuna jamaa nilikutana nae chuo, tunasoma kozi moja.

Urafiki wetu sio ule wa kuwa karibu, wala hatuendani na tunaonana mara chache.....

Ila nikipata seizures yeye ndo anajitolea kuwa karibu, kunipeleka hospitali.... Kanishauri mambo mengi ya msingi tu.

Yaani ni rafiki wa shida tu.

Huyu siwezi kumsahau.
 
umenikumbusha mwanangu mmoja kipindi icho nasoma yeye aliishia njiani akaingia mtaa aka fight sana kiasi chake alijipata jamaa alikuwa ana ni backup sana kipindi icho maisha yalikuwa tough sana ata kushika jero ilikuwa mtiti alikuwa mwanangu wa ukweli lakini arifariki ghafla tu walimkuta chumbani kwake ameanguka kutoka kitandani yupo chini aisee nili humia sana
Rest in peace my real G
 
Kuna mwanangu mmoja yupo Norway kwa sasa ni zaidi ya ndugu

Namkubali sana, tumepitia mabalaa makubwa sana lakini hatujawahi kuchokana wala kununiana
 
Back
Top Bottom