Uzembe wa Askari kulenga shabaha na kupoteza risasi 49 unaposingiziwa ushirikina

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
6,162
8,822
Nilimsikiliza Msemaji wa Polisi, Mwanamama akiwa anazungumzia tukio hili kana kwamba kulikuwa na miujiza na si uzembe wa Wahusika.

Ni aibu sana kwa karne hii kama bado tuna ujinga wa kuabudu vitu ambavyo havipo halafu hapohapo tunataka tupate Vijana wa kuleta mapinduzi ya sayansi na teknolojia.

Hatuwezi kufika kokote kwa ujinga wa aina hii, na ukweli ni kwamba Askari hao hawakuwa na uwezo. Na huenda hata kwenye matukio ya Ujambazi Polisi hupoteza risasi nyingi mpaka kufanikiwa kumlenga Muhusika.

Huyo/hao Askari waliohusika kupoteza silaha zote hizo wahakikiwe uwezo wao wa kutumia silaha kwa ufanisi...huenda Askari wetu ni legelege kiasi cha kutumia silaha huku wakiwa wanatetemeka kwa kumuogopa Fisi.

Tukiendelea kuendekeza haya mambo ya kijinga tutakuza taifa la Wanaume 'Mashoga' na kutafuta visingizio. Taifa tunahitaji Wanaume wenye balls (Men with balls)

MEN WITH BALLS

Kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki,

Utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
 
kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki, utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
Haya ndio mambo ninayoyapinga.

Jamani tuache ujinga Watanzania hakuna maajabu yoyote...risasi ni risasi haina majadiliano na imani ya Mtu...ikilengwa kwa malengo ikampata muhusika ataanguka tu.

Hata kwa Wenzetu inatokea Mtu anapigwa risasi na akaweza kukimbia eneo la tukio, na yupo anayepigwa na kuanguka hapo hapo...ila Wenzetu kwa kuwa wanatumia akili watatafuta sababu, ni huenda labda tu risasi haijafika sehemu hatarishi mwilini na sio miujiza.
 
kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki, utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
Kama Jamii hatuwezi kukubaliana na Excuse kama hizi..., Ukishakubali hili tu utakubali lolote lile...., Mwanao kushindwa mtihani na kusema alipigwa upofu wa ghafla..., mpangaji wako kukosa rent na kusema pesa imeyeyuka ghafla..., Serikali kushindwa kutimiza ahadi na kusema kodi zote walizokusanya zimegeuka na kuwa moshi..., mlinzi wako kuacha kulinda akijua kwamba atakwambia alishangaa kapata uzingizi wa pono....
 
kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki, utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
Fisi kukwepa ni jambo moja na uwezo wa Muhusika kulenga shabaha ni jambo lingine.
 
Haya ndio mambo ninayoyapinga.

Jamani tuache ujinga Watanzania hakuna maajabu yoyote...risasi ni risasi haina majadiliano na imani ya Mtu...ikilengwa kwa malengo ikampata muhusika ataanguka tu.

Hata kwa Wenzetu inatokea Mtu anapigwa risasi na anaweza kukimbia eneo la tukio, na yupo anayepigwa na kuanguka hapo hapo...ila Wenzetu kwa kuwa wanatumia akili watatafuta sababu na huenda risasi haijafika sehemu hatarishi mwilini na sio miujiza.
Wewe ni mbumbumbu sana na hauijui dunia. kalaga baho.
 
kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki, utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
Peleka huyo Fisi wenu kwa huyo Mwanaume niliyeweka clip hapo juu uone anavyotumia risasi moja tu Fisi chali.
 
kuna mengi huyajui, hao askari wanakutana na mambo mengi sana, mengine hadi wao wenyewe wanaenda kwa waganga ili kutimiza. kuna majambazi mengine hata ukiyalenga risasi haziingii na yanakusogelea yakunyang'anye bunduki, utafanya nini kama sio kutoka nduki...hahaha, risasi 49 kulenga na fisi anakwepa sio kitut rahisi, ushirikina upo, kama hauamini kuna siku utakunyorosha hadi urudi hapa useme kweli upo.
Kama ushirikina upo na huwa unafanya kazi kwa nini huwa hatuutumii kuchukua kitu kama kombe la dunia la mpira wa miguu?
 
Isiyokuwasha hujailamba. Hujajua nini kilitokea mpaka zikatumika risasi zote hizo. Tungesikia story kutoka ka Askari na mashuhuda ndipo tungeweza kusema neno.
Mashuhuda na askari wamesema fisi alikuwa anakwepa risasi! Wewe uliona wapi mnyama anayekwepa risasi? Kwa mtu mwenye utaalam kidogo tu na mambo ya bunduki na risasi atakucheka sana akisikia unasema eti fisi anaweza kukwepa risasi.
 
Hivi risasi 1 ni bei gani jamani halafu fisi mbona sio lazima kumuwinda kwa bunduki
Zina gharama lakini kwa kuwa tunaendekeza uzembe basi Askari anaweza kutoa kisingizio chochote akakubaliwa.

Na ishu hapa wala sio gharama ya risasi, ila kwa risasi 49 huyo Askari hafai kutoa ulinzi, tuseme unataka kutembea Porini ukaambiwa usinikizwe na Askari kama huyo si utashambuliwa na Wanyama?.
 
Back
Top Bottom