Uzee sasa basi, wamerekani wagundua dawa

Yuko mzee mmoja Tanzania tajiri sana asie na wajukuu mwenye kupenda dogodogo mwenye kumiliki vyombo........ akisikia hii habari jioni anakodi ndege na kwenda kuinunua hata kama haijaingia sokoni. nimtaje nisimtaje ?

Mbona kama namjua? ni wa ccm?
 
Baada ya kufanya majaribio kadhaa yenye mafanikio kwa kuwawekea panya wazee damu ya panya wadogo, na hali ya uzee kuondoka, wamerekani wako tayari muda wowote kuanzia sasa kufanya majaribio hayo kwa binadamu. chanzo; BBC

hao ni waandishi wa habari ndio wamesema hivyo.

Ukienda deep kwenye biology ya mwili wa mwanadamu utagundua kwamba damu uliyokuwa nayo mwaka uliopita sio hiyo uliyokuwa nayo leo. Chembe za damu zinatengenezwa kwenye bone marrow continuously. Chembechembe za damu na chembe nyingine za mwili wa binadamu huwa zinakuwa replaced mara kwa mara wakati binadamu anapokuwa hai, maana yake ni kwamba kila siku cells zinakufa na kutolewa nje ya mwili na kila siku mwili unatengeneza chembe mpya.

Hapo labla hao wazee wawe wanawekewa damu za watoto kila wiki, kitu ambacho hakiwezekani.
 
Haya sasa,tusubiri tuone!hivi dawa ya ukimwi walishaipata?
 
ni kumkufuru mungu tu hiyo

kaka maswala ya mungu subhana mapana sana ,usipendelee kukufurisha watu kwa mambo ambayo yako kimya,kipindi mtu wa kwanza ametua mwezini wazee walisema ivyo ivyo,lakini kwenda kule tumepata elimu kubwa sana kwani kumezidishia watu imani rejea surat Qamar,uone alichoeleza mungu na walichoona watu waliofika mwezini,maswala mengine ni ya kielimu alafu hao hawarudishi akili ikawa kama ya ujana bali wanaondoa makunyanzi katika mwili.
 
Kweli mwisho wa dunia umekaribia sema muda na siku ndio siri aliyonayo Mwenyezi Mungu.
 
Watutafutie na body spare parts
Kifai umechelewa wapi? Mbona biashara au organ donation ya figo, maini, ngozi, n.k ni kitu cha kawaida sana siku hizi kwenye nchi zilizoendelea? Especially kama mtu amekufa kwa ajali ya gari madaktari wanawahi kung'oa viungo kabla havijapoa. Hapo ni zaidi ya artificial transplants: metal, plastic, n.k. Anzia hapa Skin, bones and tissue for sale: How the dead are being used for grisly trade in human body parts | Mail Online

Watutafutie na body spare parts

cc: mshana jr mrangi bategereza SUM IBM2014 prototypeman, ...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom