Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Companero bora ukiri kwamba hujui unaloongelea. Naona unachanganya na kulinganisha dhana ya "uzawa" na mambo kibao kuanzia Citizenship, Morality, Patriotism, na hata "mapendo ya dhati kwa eneo fulani" (Whatever the hell that means, maana ni kitu ambacho ni very subjective na hakileti maana).
La ajabu zaidi unadai eti "Uzawa" ni sawa na "Uraia Mwema", lakini wakati huohuo unadiriki kusema kuna Wazawa wengine wamewazidi Wazawa wenzao kwa Uzawa wao! Ni wazi kuona hii inapingana moja kwa moja na maana ya msingi ya dhana ya Uraia (kwa mana ya haki na majukumu sawa kwa Raia wote). Huwezi kusema Uraia wa Raia mmoja umezidi Uraia wa Raia mwenzake, au?
NDD:
Companero ana-limit upeo wake katika vitu viwili tu, uzawa na uraia. Labda tuongezee upeo wa mjadala huu kwa kuongeza maana. Kwa mfano:
- Kuna watu asilia (indigenous)
- Kuna wazawa (natives)
- Kuna raia (citizens)
- Kuna wazalendo (Patriots)
- Kuna wakazi wa kudumu (Permanent residents).
Watanzania mke na mume wanapopata mtoto wakiwa na uraia wa Marekani au UK, bado asili ya mtoto yule ni Tanzania.
Watanzania wenye asili ya kihindi waliozaliwa Tanzania, ni wazawa wa nchini Tanzania.
Uraia wa nchi unaweza kupatikana kwa sababu ya asilia, uzawa au kubadilisha.
Uzalendo ni mapenzi ya nchi ambayo yanaonyeshwa katika ulinzi wa interests za nchi.
Wakazi wa kudumu ni wahamiaji wenye uraia wa nchi nyingine.
Kama nimekosea naomba usahihisho wa maelezo yangu hili upeo wetu usiwe limited katika Uzawa na uraia wakati kuna vitu vingi.