Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,604
- 1,704
1. Zakumi naona unataka kutimiza ule usemi wa kibaguzi kuwa ukitaka kumficha kitu muafrika (maana ndivyo alivyo) weka kitu katikati ya kitabu. Unataka mimi ndio nikueleze hizo haki za raia wakati zipo kwenye Katiba. Na Katiba iko kwenye mtandao. Acha uvivu wa kufikiria na kusoma. Ndio maana Mwanakijiji anakasirika mnapotaka awatafunie na awamezee kila kitu. Kama huwezi hata kui-google hiyo Katiba basi sema nikitumie kwenye barua pepe yako. Uraia si kwa ajili ya mercenary (mamluki)!
2. Ndjabu nimekuambia hilo suala ni dhana nzito. Wewe unasema kuwe na sheria za kuwasaidia wazawa dhidi ya wageni. Wazawa gani unawaongelea? Kina Mzee wa Vijisenti? Na Mzee wa Kiwira? Hao kina Americanus wenye ngozi nyeusi? Nasema hivi: Mzawa ni mtu mwenye asili ya eneo fulani au ambaye amejiasilisha katika eneo hilo, analipenda kwa dhati, yaani raia mwema na mzalendo halisi. Kwa mantiki hii Joe Slovo ni mzawa wa Afrika Kusini kuliko wale 'impimpi' waliowasaliti kina Mandela na Sisulu. Ndio, Remmy Ongala ni mzawa wa Tanzania kuliko mafisadi wa EPA, BOT, Buzwagi, Radar na Richmond! Nchi inatakiwa iwe na sera nzuri ya kulinda raia wake wema dhidi ya raia wasio wema na wageni wasiotutakia mema katika nchi hii!
3. FMS naona unamkana Nabii Mkuu wa Uzawa, sasa kama ni sera nzuri mbona hamuwi manabii wake wakuu muone jinsi itakavyowatokea na ninyi puani maana ukitaka kuchimba uasili wa kila mtu , je, nani atasimama? Au umesahau kuwa hata Nyerere mlianza kusema kuwa ni Mburundi sijui Mrwanda? Na Mkapa naye si mlishaanza kusema kuwa ni Mmozambiki? Tena na Karume si mlidai kuwa ni Mmalawi?