Uzalishaji mdogo wa testosterone husababishwa na nini?

kayuguyugu

Member
Oct 30, 2013
30
30
Naombeni kujua hili tatizo la uzalishaji mdogo wa homoni za testosterone husababishwa na nini na tiba yake ni nini?
 
Kitaalamu hio hali inaitwa ''Male hypogonadism''

Inawezekana ikasababishwa na vitu vifuatavyo (baadhi)
1. Kutumia dawa kali au vitu vyenye kileo kikali (kinywa au kuvuta)
2. Mtu kuwa na korodani moja au shida ya mishipa ya fahamu kutoka kwenye ubongo
(Hapa unakuta korodani moja inafanya kazi au moja haikushuka toka utotoni)
3. Majeraha ya ndani (kuumizwa kwa kitu chochote kwenye viungo zalishi)
4. Umri (kadiri mtu anavyoukaribia uzee, uzalishaji nao unapungua)
5. Magonjwa kama Kansa na HIV/AIDS (inaona na ya juu kwenye matumizi ya dawa kali)
6. Kitambi kikizidi sana nacho kinachangia
7. Stess zikizidi pia zinachangia. (Stess za akili na kuuchosha sana mwili mfululizo)

Matibabu: (Epuka hayo hapo juu)
1. Jitahidi kupunguza stress (msongo wa mawazo)
2. epuka kuwa na uzito ulipitiliza au kuwa na uzito mdogo zaidi yako. (Njia rahisi hapa, jipime ujue una Centimita ngapi, ukipata toa 100, kitakachobaki ndio uzito unaoshauriwa usiuvuke. ukiuvuka unakua umezidi uzito, mbele zaidi unakuwa na kitambi. Mfano Mimi nikiwa CM 184, nikitoa 100 nabakiwa na 84, hivyo katika uzito wa kawaida nisizidi kilo 84. Nikizidi hapa ni changamoto ya kuelekea kwenye kitambi, hivyo natakiwa nichezee labda 75 hadi 85 hapo.

Vinginevyo tumia MBI index= (uzito in Kg)/(urefu in meters*Urefu in meters) . utakachopata kikiwa kati ya 18.5 hadi 24.9 Upo kweze uzito wako wa kawaida. Ikipungua 18.5 uko underweight (ikizidi 24.9 hadi 30 ni overweight, ikifika 30 na zaidi upo obese.

3. Angalia sana ulaji wako. Punguza sana vyakula vya mafuta na wanga; Zingatia sana matunda yenye na vyakula vya protini na madini ya zinki (Samaki, mbegu za tikiti na Maboga)
4. Fanya mazoezi fanya mazoezi fanya mazoezi.

Usijali sana mtiriko wangu, sijawa na muda wa kutosha, japo kwa uchache natumai utajifunza kitu.

Tized
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom