Uwindaji haramu Tanzania: Ni nani yupo nyuma ya waarabu hawa?

Hizi picha na video ni za mwaka juzi ndio ikapelekea wakafungiwa sasa sina hakika kama wamerudi tena ama la! Ila kwa hizo pich sio za sasa.....ila mamlaka ifanyie kazi
 
Mkuu waarabu ndio zaidi wenye kufanya haya mambo ya kikatili kwa wanyama wetu kuliko hata wazungu. Wazungu wao waliyafanya hayo sana kipindi Tanganyika wanaitawala.
hii kesi ya tumbili 61 juzijuzi tu munaijuwa ??
n00b umetufunguwa macho....
tum%2Cbiliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.jpg
 
Kuna member mmoja hapa aliwahi kuleta takwimu za sensa ya tembo kwenye hifadhi moja ya taifa, kwa kweli inaonesha baada ya miaka kumi au Kumi na tano ijayo hatutakuwa na tembo Tanzania.
Na vijiji vilivyo karibu na sehemu wanayowinda tembo,
Kila siku nyama ni ndovu usubuhi nchana na jioni
tamu balaa
supu nyekunduu
nyama ina nyuzinyuzi
 
Hilo suala la uwindaji wa kitalii wengi wetu hatuliewi vizuri. Kampuni za uwindaji zinalipia kuua wanyama katika maeneo waliyopewa na inaruhusiwa kisheria. Tatizo la kukiuka baadhi ya taratibu anayepaswa kubeba lawama ni PH (Professional Hunter) ambaye huambatana na wawindaji ambao anapaswa kuwa-guide. Hakuna tatizo kama ambavyo inajaribu kuelezwa na baadhi yetu. Mgogoro wa kampuni hiyo ya waarabu na ile ya wamarekani ulipaliliwa na aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu ambaye inadaiwa alikuwa anatumiwa na wamarekani kuwakomoa waarabu ambao hulipa pesa nyingi zaidi na husaidia zaidi jamii katika maeneo yanayozunguka eneo lao la uwindaji. It's not a big deal!
 
Wanasindikizwa mkuu, wakati mwingine hunting party inakuwa na maafisa wawili wa Serikali kuhakikisha kanuni za uwindaji wa kitalii zinafuatwa.
Huu ni unyama ma kutisha... Kwanini wawindaji waliopewa leseni wasisindikizwe na maafisa wanyama pori ili kuhakikisha wanyama waliolipiwa ndio wanaowindwa na ukatili haufanyiki?? kwanza sijui kama kuna sheria ya kumruhusu mtoto mdogo wa umri huo kuwinda???
 
Sio kila mtu analipwa, wapo watanzania wenye uchungu na rasilimali za Taifa hili.
Kwa bahati nzuri kwa kiasi ninalifahamu sula hili hapa kuna mgogo wa haki ya uwindaji katiaka eneo husika kati kampuni moja ya kimarekani na kampuni ya greenmile.waziri alitoa haki ya kampuni ya kimarekani kuwinda kuwinda bila kufuta haki hiyo kwa kampuni ya greenmile ambayo ilishinda zabuni ya kuendesha uwindaji.sasa greenmile imeshinda na kurudishiwa haki hiyo.ndio maana kelele zimeanza.na nxio maana nimekuuliza umelipwa kiasigani.
 
Tangu mwanzo inajulikana nani mwenyeji wa hao wawindaji(MAJANGILI).Wakati umefika sasa wa kuangalia upya mikaba yao.Hata waliwaletea mwaka juzi msaada wa magari ya kampeni.Kwa undani aulizwe katibu mkuu wetu ana majibu sahihi.Na hasa suala la Loliondo.
 
Pamoja na uwepo wa professional Hunter, game Scout wa Serikali anakuwepo pia. Alichukua hatua gani alipoona Sheria na kanuni zinakiukwa kwa kiasi kikubwa hivi??? Au wawindaji walikuwa peke yao bila gamescout? It doest matter how much one pays, sheria na kanuni lazima zifuatwe.

Kwenye video wanaoonekana ni MKURUGENZI MTENDAJI na MMOJA WA WANAHISA WA GREEN MILES, iweje useme Professional Hunter abebe lawama?

Hilo suala la uwindaji wa kitalii wengi wetu hatuliewi vizuri. Kampuni za uwindaji zinalipia kuua wanyama katika maeneo waliyopewa na inaruhusiwa kisheria. Tatizo la kukiuka baadhi ya taratibu anayepaswa kubeba lawama ni PH (Professional Hunter) ambaye huambatana na wawindaji ambao anapaswa kuwa-guide. Hakuna tatizo kama ambavyo inajaribu kuelezwa na baadhi yetu. Mgogoro wa kampuni hiyo ya waarabu na ile ya wamarekani ulipaliliwa na aliyekuwa waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu ambaye inadaiwa alikuwa anatumiwa na wamarekani kuwakomoa waarabu ambao hulipa pesa nyingi zaidi na husaidia zaidi jamii katika maeneo yanayozunguka eneo lao la uwindaji. It's not a big deal!
 
Kwa mfano nyani anauliwa ili akafanyiwe nini?Aliwe?Au ni mazoezi tu ya shabaha?
 
Suala hapa ni ukiukwaji wa kanuni za uwindaji wa kitalii na sheria ya wanyamapori unaoonekana wazi wazi na waliokiuka hawajachukuliwa hatua stahiki.

Kwa bahati nzuri kwa kiasi ninalifahamu sula hili hapa kuna mgogo wa haki ya uwindaji katiaka eneo husika kati kampuni moja ya kimarekani na kampuni ya greenmile.waziri alitoa haki ya kampuni ya kimarekani kuwinda kuwinda bila kufuta haki hiyo kwa kampuni ya greenmile ambayo ilishinda zabuni ya kuendesha uwindaji.sasa greenmile imeshinda na kurudishiwa haki hiyo.ndio maana kelele zimeanza.na nxio maana nimekuuliza umelipwa kiasigani.
 
Hizi picha na video ni za mwaka juzi ndio ikapelekea wakafungiwa sasa sina hakika kama wamerudi tena ama la! Ila kwa hizo pich sio za sasa.....ila mamlaka ifanyie kazi

Kwani waliwahi kuondoka? Mbona tuko nao kwenye biashara kama kawaida. Hata baada ya waziri wa maliasili na utalii aliyepita kuwafungia leseni yao hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa. Cha kushangaza zaidi waziri wa sasa akiandika barua zinazohusiana na masuala ya uwindaji wa kitalii Green Miles Safaris wanapata nakala zao.
 
Hivi hakuna utaratibu mwingine tunaweza kuutumia badala ya kulalamika kila siku !???
 
Hawa waarabu HAWAFANYI hivyo bila ya sheria. Wanalipia malipo ya kuwinda kila aina ya mnyama. Sheria yetu ya nchi inaruhusu, kuna kitu kinaitwa ANIMAL CULING ( kupunguza idadi ya wanyama kwa kuwawinda) ndio hapo serekali inatoa vibali na kuruhusu uwindaji.

Hebu angalia hiyo link hapo juu utawaona wamarekani nao wanawinda. Idadi kubwa ya wauwaji wanyama wetu wanaokuja kujinufaisha na uuwaji wa wanyama ni waz unguarded, na wamekuwa wakifanya hivyo zaidi ya miaka 100 na hakuna anayewasema, lakini akifanya mtu mwingine tunawasakama.

Ni bora tukalipinga hili jambo kwa wote wanao kuja kuuwa wanyama wetu kama starehe. Kama ni upunguzaji nasimama waruhusiwe watanzania wenye shida ya kitoweo.

Sheria za uwindaji haziruhusu kupiga mnyama ukiwa kwenye gari, haziruhusu kupiga wanyama wadogo wala haziruhusu kuwagonga na magari. Hoja zimesimamia hapo. Pia haziruhusu mateso ya aina yoyote kwa mnyama aliejeruhiwa, ndio maana ukimjeruhi inabidi umfuatilie ili ummalizie.
 
Inashangaza sana mkuu halafu kuna watu wanawatetea.
Hapo inadhihirisha umekula chochote huna hoja yeyote ya maana.na tena ungekuwa mkweli kufungiwa kwa mwaka mmoja ni adhabu tosha isitoshe kulikuwa na prof hunters na watu wa maliasili.hivi wewe ndio mwenyekujua sana sheria za maliasili kuliko hào walkokuwepo.
 
Back
Top Bottom