Uwezo wa Roma Mkatoliki kutunga na kuandika nyimbo za harakati za kisiasa na utawala ni mdogo mno

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Huyu kijana anauwezo mdogo wa kutunga na kuandika nyimbo kufikisha ujumbe wa aliokusudia. Badala yake amejikita kwenye hisia, mihemko na nadharia. Ila ukikaa na kusikiliza hakuna ujumbe unaoleweka.

Hawa vijana wangejifunza kwa majabali ya muziki waliotangulia akina marijani rajabu na wengine. Nimepata muda wa kusikiliza wimbo wa Roma mkatoliki sijaona cha maana wala meseji za kueleweka zaidi ya upayukaji tu. Nashangaa Kwanini watu wamehamaki wakati ni wimbo wa kawaida tu uliojaa hisia kuliko uhalisia

Mimi nilikuwa mfuasi wa nyimbo za Mr.Sugu, Profesa Jay, Solo thang na Afande Sele kwenye upande wa nyimbo za kufoka foka

Hawa wanamuziki wasasa sio wabunifu ni muda sasa tuwachoke
 
We mwenye uwezo mkubwa yako uliyotunga iko wapi?! Na siyo kila nyimbo iwe na ujumbe unaoeleweke nyingine hazitakiwi kueleweka ila kwa utaemuhusu unaeleweka tu mbona. Wasanii kibao wanatuimbia nyimbo hazina ujumbe wala nn na tunasikiliza itakuwa Roma. We endelea kusikiliza hao watu wako achana na hawa wa sasa
 
Mkuu tukiacha ushabiki je kuna nini cha ziada tumejifunza kwenye Huu wimbo
We mwenye uwezo mkubwa yako uliyotunga iko wapi?! Na siyo kila nyimbo iwe na ujumbe unaoeleweke nyingine hazitakiwi kueleweka ila kwa utaemuhusu unaeleweka tu mbona. Wasanii kibao wanatuimbia nyimbo hazina ujumbe wala nn na tunasikiliza itakuwa Roma. We endelea kusikiliza hao watu wako achana na hawa wa sasa
 
Mubaraka mwinshehe ndio kaimba wimbo Mtaa wa saba na sio marijani

Nyie vijana msiwe mnakurupuka
Marijani Rajabu wa Mtaa wa Saba na Jogoo la Shamba, yule wa Moro Jazz...:D:D:D:D
''Tuyaache hayo vipi Korosho za Mtwara'' By anaitwa Roma
 
Back
Top Bottom