Uwezekano wa vifurushi TV na simu kufanana?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,681
1,698
Ukweli inauma na ni muda mrefu nimekuwa nawazia jambo hili kuwa MATUMIZI YA VIFURUSHI VYA KING'AMUZI KUWA SAWA NA VYA SIMU?

Nimekuwa nafikiria hivi hasa kutokana na TANESCO wanavoupiga mwingi siku hizi hakuna cha kiangazi wala masika.

Kifurushi cha simu kinaisha pindi tu utumiapo aidha kwa kutumia sauti maana ya kupiga au kutuma ujumbe, kama hufanyi hivo kifurushi chako hakitumiki.

Kifurushi cha TV kinakwisha licha ya kutokuwasha hiyo TV kwa maana usiku na mchana au umeme haupo (mgao) mzigo unasoma tu.

Ingesaidia pakawa na Chama cha kuwatetea wenye ving'amuzi hapa nchini vilevile.

Nawasilisha na inauma kwa kweli.
 
Una hoja ila hujaiandika kwa utulivu tu...

Umacholilia wewe hapa ni tuwe na pay per view kwa contents za TV ambazo ni programs za kawaida, iwe kama LUKU (lipa kadiri unavyotumia)
 
Una hoja ila hujaiandika kwa utulivu tu...

Umacholilia wewe hapa ni tuwe na pay per view kwa contents za TV ambazo ni programs za kawaida, iwe kama LUKU (lipa kadiri unavyotumia)
Shukran mkuu kwa kunielewa maana jana umeme wameuchukua saa mbili asubuhi, wakaturejeshea saa kumi na mbili jioni halafu wakauchukua tena saa moja na nusu usiku na kuturejeshea saa tano usiku. Sasa jana pesa imeliwa hivihivi.
 
Pay per view zitakuwa gharama sanaaa,
Utasikia ili uangalie kipind fulan ni 1000/-, match ya simba 2000/- kwa mwezi simba acheze mara 6, ni 12,000/- hio,
Bado vipind vingine,

Tupambane tuwe na umeme wa uhakika ila sio ppv, hii ni ngumu
 
Walete PPV... hii itasaidia kupunguza machannel ya hovyo wanayotulundikia maana hayata uzika kabisa. Tena hii itawafanya wawekeze zaidi kwenye content creation.
 
Back
Top Bottom