DOKEZO Uwanja wa Ndege wa Zanzibar una huduma mbovu, mtalii anazongwa na watu wenye uniform na wasio na uniform utadhani mwizi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Huduma za kuingia na kutoka Zanzibar zipo tofauti Sana na huduma za viwanja vingine vya ndege Duniani. Nadhani mentality ya wizi au Rushwa umepelekea serikali ya Zanzibar kujaza taasisi nyingi zinazosumbua wageni kinyume kabisa na nchi nyingi.

Nadhani uwanja una camera, ingetosha data zinazokusanywa na immigration zikawa shared kwenye taasisi nyingine kupunguza mzunguko wa wageni uwanjani.

Jambo jingine wengi wa maafisa wasiovaa uniform uwanjani wanaonekana wazi kukosa ueledi kwenye kazi katika viwanja vya ndege; sisi tuna kampuni ya utalii, ambapo wageni wetu wengi wanalalamika kuwa mistreated na maafisa kanzu uwanjani hapo. Mistreatment inaanzia kwenye taratibu za kuingia au kutoka, passport inakaguliwa zaidi hata ya mara tatu sijajua kama Kuna silaha au kitu Gani ndani ya pasport.

Kiutaratibu wageni wetu wengi tunawaombea visa wakiwa nje kupitia huduma ya online visa na tunafanya hivyo tukiamini kwamba tumewapunguzia usumbufu lakini wakifika uwanjani treatment it's like wezi au watu wenye tishio la kiusalama. Mgeni mwenye online visa anahitaji kupekuliwa pasipoti yake?

Tukiamini akishahudumiwa tayari anaruhusiwa kuingia nchini kw sababu taarifa zake zinakuwa serikalini tayari; je tunachokagua mara kumi kumi ni kipi? Mgeni anatumia ten to fifteen minutes kuzunguka uwanjani for what. Tupunguze huduma zisizo na logic, tuwape watendaji wetu exposure waone huko nje huduma zipo vipi, tuondoe maafisa wasio na uniform ambao wanatafsiriwa kama wapelelezi na kama tunataka watumike basi wavae uniform Kwa sababu kukaguliwa na MTU asiye na uniform kunatisha wageni wakiamini wamehojiwa na majasusi.

Tusitoe as if tunahudumia wageni, hii IPO pia wanapotaka kuondoka nchini badhi wanazuiliwa even kupanda ndege bila kuelezwa sababu ni Nini? Mnakwamisha biashara Kwa kujaza watu wasio na sifa za kutoa Huduma viwanjani, uwanja wa Ndege huduma za kipolisi za kazi gani?

You have to rethink mpunguze watoa huduma, acheni taasisi Moja kama Uhamiaji Tena waliopo kwenye madirisha ndio watoe huduma siyo kusambaza watu wanaosumbua wageni bila kazi ya maana uwanjani Ili tu waonekane nao Wana kazi. Fanyeni utafiti wa huduma zenu je zinaendana na matakwa ya Kimataifa?

Zinaboost utalii? Zimamfanya mgeni ajisikie kurudi?
 
siyo kusambaza watu wanaosumbua wageni bila kazi ya maana uwanjani Ili tu waonekane nao Wana kazi
Ukweli ni kuwa ZNZ hakuna ajira.
CCM na serikli yake iliwaahidi vijana fulani wasaidiae kuingia madarakani CCM ili wapewe ajira.
Sasa kila kichchoro kinachoonekana kama Opportunity kinatumiwa kuwekwa hawa (Janjaweed) ili kuwapoza wasije wakaleta rabsha dhidi ya serikali.
Siasa, ndiyo inatawala pale na si kanuni za kiuchumi wala kiusalama.
 
Ukweli ni kuwa ZNZ hakuna ajira.
CCM na serikli yake iliwaahidi vijana fulani wasaidiae kuingia madarakani CCM ili wapewe ajira.
Sasa kila kichchoro kinachoonekana kama Opportunity kinatumiwa kuwekwa hawa (Janjaweed) ili kuwapoza wasije wakaleta rabsha dhidi ya serikali.
Siasa, ndiyo inatawala pale na si kanuni za kiuchumi wala kiusalama.

Uko sahihi kabisa, Zanzibar siasa ndio kila kitu. Na hayo ndio madhara ya kuingia madarakani bila ridhaa ya umma, kwani unakuwa na kundi kubwa la kuliridhisha kinyume na utaratibu.
 
Aende Entebe yaani askari wanalinda eneo mpaka ya pale pa kuondokea. Wanamatch na bunduki zso yaani hawasimami Mahali pamoja. Huyu akienda mbele yule wa kule anaanza nae kuja upande wa pili wanakutanika katikati. WAPO MACHO WAKATI WOTE MPAKA ZAMU YAO IISHE.
 
Wewe hujawahi kusafiri nje ya nchi, yaan Dk 10 au 15 uone nyingi?? Nenda Ethiopia hapo, Ulaya pia ukaguzi ni mkubwa kuliko unavyodhania wewe. Sema wao wameadvance kwenye teknolojia.
 
Ukweli ni kuwa ZNZ hakuna ajira.
CCM na serikli yake iliwaahidi vijana fulani wasaidiae kuingia madarakani CCM ili wapewe ajira.
Sasa kila kichchoro kinachoonekana kama Opportunity kinatumiwa kuwekwa hawa (Janjaweed) ili kuwapoza wasije wakaleta rabsha dhidi ya serikali.
Siasa, ndiyo inatawala pale na si kanuni za kiuchumi wala kiusalama.
Umenena kweli
 
Msafiri kutumia hata zaidi y nusu saa airport ni kawaida duniani. Kikubwa ni kuwe na utaratibu unaoeleweka .
Kitendo cha wageni kuhangaishwa kiholela na wafanyakazi wasio na uniform na vitambulisho waljvyovaa wamevigeuza usiweze kusona jina ndio tatizo.

Kama kuna utaratibu mzuri mgeni ataona kabisa kuwa amechelewa kwa sababu labda ya wingi wa watu au sababu nyingine.
 
Back
Top Bottom