Uwajibikaji wa Vyombo vya habari wa Tanzania Media Fund Mlimani City

Zitto... Kuna uvumi mwingi sana ktk blogs na nyingine zinatumika ktka media bila kupata ushahidi
 
Mgamba: Wikileaks ichukuliwe kama sehemu ya chanzo cha habari, na siyo kwamba ni habari yenyewe
 
Mgamba+++ wikiliki ni chanzo cha habari na ukipata lazima utafute balance na kuwpa nafasi wengine mfano Hosea na Us embassy kupata uhakika... Ethics ktk online media inakua na tatizo
 
Mgamba: Lazima tuwe makini sana na matumizi ya new media, lazima ichukuliwe kuwa ni chanzo cha habari
 
Zitto, trust ni tatizo sana ktk jamii yetu, kuna ripoti kwamba 78pc ya Watanzania hawaaminiani na DSM ni 80pc na kwa DSM 9 out of 10 hawaaminiani... Mara ingine uzushi kabisa naandikwa uongo... Nadhani Watanzania wanapenda zaidi habari za uzushi.... Naamini sana mediÀ zetu... Nadhani ni vyema wakapata nafunzo zaidi waandishi wetu
 
Zitto: Siyo kwamba siamiani vyombo vya habari, naviamini sana na mara nyingi nimekuwa nikipewa nafasi kubwa, lakini kuna wakati nazushiwa, inawezekana Watanzania wanapenda sana habari za uzushi na hilo naweza kulisemea, lakini nimeamua kutumia new media kwa kuwa nawafikia wananchi kwa muda mfupi zaidi na kwa haraka.
 
Mchangiaji mmoja anasema...social media inatoa changamoto kubwa kwa media houses maana wanakuta habari ishasomwa sana ktk social media
 
Simbeye... Taaluma ktk social media, print and electronics na wao wabadilike maana mambo uanabadilika sana
 
Lazima tuzingatie maadili hata kama tuko ktk online... Tuwape mafunzo waandishi wetu
 
Mgamba... Tunachangamoto kubwa sana, new media na electronics, TV na Radio maana ukifika mwanza saa moja usiku unakuta mambo yashashomwa
 
Mgamba (Mhariri Guardian): am Addicted to social media, namaliza muda wangu mwingi sana kwenye kompyuta nikisoma, kuiandika na kuchangia baadhi ya mijadala kwenye facebook, twitter, blog na maeneo mengine ya mtandao huo wa kompyuta
 
Zitto: Vijijini electronics wanapata haraka, twitter na new media unaweza kupata popote kwa kutumia mobile na baadae itafika wakati hadi vijijini wataanza kutweet
 
Zitto... Bada ya kuweka ktk tweeter nimepata maoni na taarifa nyingi kutoka kwa wataalamu kuhusu ukwepaji kodi na hii inasaidi sana kuuliza maswali TRA na hii ni kupata taarifa na inajenga trust maana ni moja kwa moja ni Zitto
 
Mjadala umeisha lkn mkutano unaendelea... Taarifa zaidi baadae
 
Maamuzi mazito... Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Habari hajaonekana... Zitto anapewa jukumu la kuwa mgeni kukabidhi vyeti na baadae mgeni rasmi akifika atatoa hotuba
 
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambaye alikuwa akitarajiwa kufika kwenye kongamano hili la wadau wa vyombo vya habari lililoandaliwa na Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) hadi sasa hajafika na imeamuliwa na uongozi wa TMF kuwa Zitto Kabwe ambaye amewasili ndiye anachukua baadhi ya majukumu ya mgeni rasmi. Tuendelee...
 
Mgeni rasmi kaingia wakati mambo yanamalizika, imeamuliwa kuwa atahusika sasa kufungua maonesho ya picha na baada ya hapo msosi na kuondoka
 
Mkuu wa TMF, Abdu Simba anasema TMF ijayo itakuwa na mengi mazuri kwa ajili ya neema ya vyombo vya habari, nchi na watu wake
 
Naibu Waziri ndiyo anaingia sasa, amefuatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo. Sasa atakuwa na kazi moja tu kubwa kufungua maonesho ya picha
 
Back
Top Bottom