Kwa kuwa mwandishi, nilijua naweza kutimiliwa anytime naweza kupata zawadi ama kupanda ngazi wakati wowote, kwanza nawajibika na sera ya gazeti na kila chombo kina policy.. Hatuko juu ya sheria, ukiona umekosea lazima uombe radhi na kuwajibika kwa wasomaji wako
Je, munawaheshimu wasomaji wenu? English paper ukikosea unarekebisha lakini magazeti ya Kiswahili yanarudia sana, anatoa mfano wa Tanzania Daima kwamba Magufuli amejiuzulu ama Sitta na Mwakyembe wameshughulikiwa na cabinet wakati hakukua na kikao siku hiyo
Simbeye anasema kuiwajibisha serikali lazima uwe na sababu, lazima kuwe na kitu cha kuiwajibisha serikali, lakn kama hakuna kitu unadhoofisha serikali bila sababu. Ktk media lazima kuwa objective.
Ichikaeli Maro wa Daily News anasema lazima kama media house unakosea uombe radhi na kurekebisha... Lazima tuwape nafasi wanaotuhumiwa tuwasikilize na wao
Mwandishi mmoja anasema: ni mentality ya editors, hawako acountable kwa umma kama yule wa Daily News alikua anawajibika kwa watawala wakati wa uchaguzi na si kwa umma, tumeona Mkurugenzi wa TBC alikua anawajibika kwa umma na tumeona yaliyomkuta.... Anashangiliwa
Mohamed Tiba anasema, kwa uzoefu wake ktk media, nimesoma magazeti, sijaelewa kama ni kuwajibishana ama ni vita kati yao na hii imenishtua maana tumeona media zinajenga uaduia miongoni mwao na ni tishio kwa uhuru wa habari na hatuoni vikifanya kazi pamoja
Wamiliki ni tatizo, hawawalipi vizuri waandishi na hapo wanalazimika kupata nauli na wApo wanaopenda waendelee kuteseka na njaa ili wapate nafasi ya kuwatumia
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.