Uwajibikaji: Nyerere kiongozi pekee aliyeonesha ukomavu kwenye uwajibikaji Tanzania

mavumbi

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
596
326
Mwaka 1982 mwalimu aliambiwa na wana CCM kwenye Mkutano wa Halamashauri Kuu ya CCM kuwa mzee hali ni mbaya.

Walimwambia tumefikia mahali rushwa imeshamiri kiasi kwamba Daktari anapokuwa thieta na mgonjwa wa upasuaji, anauliza wanandugu wazi Bahasha yangu iko wapi?

Hamjui kamshahara kenu ka serikali ni aibu? Mwaka 1985 bila woga wala kuhofia kukosolewa, akaachia ngazi - ee ngoja wengine nao wajaribu.

Mwaka 1994, Waheshimiwa John Malecela na Horace Kolimba walipo jichanganya kwenye misimamo ya kitaifa Mwalimu aliwaambia bila kumung'unya maneno, Wajibikeni, na wazee hao walijikuta wakisambaratishwa ingawa ilikuwa ni aina ya kuwafukuza kazi!

Kabla ya hapo, ni mwalimu ndie aliyemwambia Mwinyi ajiuzulu baada ya kashfa kubwa ya vikosi vya usalama akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Ilitumika Diplomasia tu kusomeka amejiuzulu mwenyewe
Mwaka 2007 Edward Lowassa alifukuzwa Wabunge Dodoma na kumpa wakati mgumu Bwana JM Kikwete, kunda upya serikali.

Mfano wa hovyo wakati wa JPM Rais wa 5 wa Tanzania ni pale Waziri wa Ujenzi Mhe Kamwelwe alipoulizwa, na Rais, kwa ewe Mhe Waziri je unasemaje kuhusu aibu hii ya kubomoka kwa Kalvati tu, kwenye Barabara kuu ya Dar - Dodoma - Kanda ya Ziwa? Wote tulisikia majibu yake maana yalikuwa live! Ewe Mhe Rais Naomba unisamehe..."

Na kwa 'uungwana wa JPM', akawawajibisha walio chini yake, akamwacha waziri ambaye mfumo ulihakikisha harudi tena Bungeni!

Hohoho! Ndio uwajibikaji Tanzania. Hakuna, tuombe aje mwingine wa kama Nyerere!
 
Kwamba na Sa100 na katelephone wawajibike kwa AJALI ya precesion air!!?

Utasubiri Sana, NYERERE alienda na ile CCM,wanaotamba Sasa ni wanamtandao wanahakikisha chakula hakikosekani tumboni!!

Mungu IBARIKI NCHI YANGU TANZANIA!
 
Back
Top Bottom