Uvivu kazini na kutegeana kazi

cold water

Senior Member
Oct 6, 2021
175
618
Bora ofisi uwe peke ako kuliko kuwa wengi ofisi moja,kuna watu ni wategezi wa kazi jamani hapa ofisini kwangu tupo watatu,kiongozi mmoja tu katika sisi wafanyakazi watatu, yeye kiongozi kazi yake kuhakikisha mambo yanakaa sawa na huwa hafanyi usafi kiujumla,huyu mwingine sasa sijawahi muelewa sio kiongozi lakini hataki kujishughulisha kwenye mambo ya usafi, nimeripoti kazini mwezi wa NNE lakini,tangu mwezi huo wa nne hadi leo hii Mimi ndo nimekua mfanya usafi kila iitwayo Leo nisipofanya panaachwa kama palivyo nimechoka.

Lakini ukiangalia ni majukumu yetu sote kwasababu hakuna aliyeajiliwa kwaajili ya usafi by then kazi zetu tunafungua SAA 2:00 asubuhi hadi SAA 9 jioni, most of the time utamsikia tu nimechoka leo blah blah nyingi utakuta tumeingia tu ile asubuhi analalamika kuchoka.

Au siku iyo ataenda huku mara aende kule anazunguka zunguka tu yani kupeleka masaa, sasa sikuiyo kiongozi wetu hakufika kazini tuliingia wawili ilikuwa majira ya saa saba siku iyo akaniambia hapa tupeane masaa ya kupumzika yeye ataondoka saa saba mchana atarudi saa nane na nusu akifika iyo saa nane na nusu na Mimi nirudi nikapumzike lakini ukiangalia hapo Mimi napumzika nusu saa tu kutimia ile saa 9:00 yeye toka saa saba mchana hadi saa 8:30 jamani dah nachokaga sometime kazi za kutegeana.
 
Back
Top Bottom