UVCCM Morogoro wampinga Malecela


LOWASA NA JK2.jpg
 
This is funny,

Unapinga watu kutoa matamko huku wewe ukitumia njia hiyo hiyo kutoa matamko?


Kama Makonda amekiuka kanuni,kwani wewe usipeleke kwenye vikao vya chama?Wewe umefuata katiba ipi iliyokuruhusu kumshutumu Makonda na Malecela hadharani?

Je ukiambiwa na wewe umuombe msamaha Mzee Malecela utaona umeonewa?


Yaani kada wa muda Mrefu wa UVCCM ndiyo anaweza kweli kuja hadharani kwa hoja dhaifu na za aibu namna hii?Hii ndiyo hazina ya CCM? Kweli hii chama hakiwezi kuunda serikali bila mawaziri mizigo na in the near future tutarajie the worst.

Unasema makonda kadanganya,je ukiulizwa ni lini Lowassa alistaafu U-waziri mkuu utatujibu kwa weledi na kutuondolea mashaka juu ya kauli na dhamira yako?

-Hivi,hili Tamko ni lako Binafsi kama mwenyekiti wa hilo tawi au la taasisi unayowakilisha?

Kama uko kwenye mawazo yangu Ben. Mtoa lawama anatumia njia ile ile iliyotumiwa kimakosa (kama anavyodai) kutoa maoni yake. Nae ni kiongozi wa taasisi hiyo hiyo. Inachekesha na kuhuzunisha sana. Nilitegemea angepeleka malalamiko yake haya kwenye hivyo vikao anavyotaka yapelekwe ili kutumia busara na kanuni za CCM. Amenukuu taratibu za rufaa ndani ya chama. Ameshindwa kuona kuwa Makonda hana cha kulalamikia zaidi ya kukanya (kama kiongozi anavyotakiwa) kutokana na yanayofanywa na wanachama wengine kwa mantiki ya kuutaka uRais 2015.
Lakini kinachosikitisha zaidi ni kauli za kejeli na utovu wa nidhamu kwa kiongozi mstahafu ambae ana umri wa Baba yake, kama sio Babu yake.
Nilidhani viongozi walitakiwa kujua namna bora zaidi za kutoa kauli zao na kuthibitisha ubora wa hoja zao.
 
Tatizo Mzee Malecela anaamini watanzania wa sasa wanamsikiliza. Angefanya utafiti kidogo angeshangaa sio watu watu wengi hawamsikilizi lakini hawajui yeye ni nani?!
Sijui kama una uhakika wa unachokisema. Kauli kama hizi zinahitaji research.
 
Friends of Lowasa!!!!!!! Wapo wengi wala msishangae yetu macho na masikio. Kumbukeni mkuu wa nchi yupo kimya yeye yupo tayari kuwapa nchi wapinzani ili amani iwepo kati ya hapo CCM makundi yao ni mabaya sana.
 
Salamu Albedo aka Msando.Huonekani kwenye mikutano ya OPD hapa mo-town,
Baada ya salamu,nikujulishe kuwa hawa UVCCM moro ni vilaza,sio wasomi kama wewe na hata!
Hivi mtoa tamko si anadai kuwa Makonda sio msemaji kwa kuwa sio mwenyekiti au katibu wa chama? Mbona na yeye sio msemaji wa UVCCM moro?
Anywayz,hawana jipya na sasa mpango mzima ni M4C- OPD na tutawachapa tarehe 9 kisawasawa.
 
ngoja nitumie maneno ya watoto wa mjini "kiki"!!!
naona kila mtu sasa hata wale wasiojulikana wanatumia jina la lowasa kupata "kiki". nnachoona mimi hizo kiki zitawacost sana mambo yakienda mrama.

kiki= umaarufu
 
This is funny,

Unapinga watu kutoa matamko huku wewe ukitumia njia hiyo hiyo kutoa matamko?


Kama Makonda amekiuka kanuni,kwani wewe usipeleke kwenye vikao vya chama?Wewe umefuata katiba ipi iliyokuruhusu kumshutumu Makonda na Malecela hadharani?

Je ukiambiwa na wewe umuombe msamaha Mzee Malecela utaona umeonewa?


Yaani kada wa muda Mrefu wa UVCCM ndiyo anaweza kweli kuja hadharani kwa hoja dhaifu na za aibu namna hii?Hii ndiyo hazina ya CCM? Kweli hii chama hakiwezi kuunda serikali bila mawaziri mizigo na in the near future tutarajie the worst.

Unasema makonda kadanganya,je ukiulizwa ni lini Lowassa alistaafu U-waziri mkuu utatujibu kwa weledi na kutuondolea mashaka juu ya kauli na dhamira yako?

-Hivi,hili Tamko ni lako Binafsi kama mwenyekiti wa hilo tawi au la taasisi unayowakilisha?

Ata mimi nimesoma vitabu vyote vya historia ya nchi yetu lakini sijaona sehemu imemcot El mwaka aliostaafu uwaziri mkuu. Ila TBC1 inatangazaga waziri mstaafu.
 
huyu mamvii alistaaafu lini?

huyo ni waziri mkuu aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond aseeeh!!!!!!!!!!!!
 
[h=2]Friday, 31 January 2014[/h][h=3]UVCCM MORO WAMCHACHARUKIA MALECELA[/h]






UVCCM MORO YAMTOLEA UVIVU MALECELA
[h=3][/h]
Kutokana na malumbano yanayoendelea kati ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi hususani Jumuiya ya Umoja wa vijana (UVCCM) kutokana na matamko yanayoendelea kutolewa.

Ni jambo la kushangaza sana kumuona Mzee Mashuhuri na nguli wa Chama cha Mapinduzi Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu kumuunga mkono kijana aliyekiuka katiba ya Chama cha Mapinduzi na kanuni za Umoja wa Vijana Paul Makonda kutokana na kauli yake ya kuudanganya Umma kuwa tamko alilolitoa la kumkashifu Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa NEC ndugu Edward Lowassa kuwa ni la Umoja wa Vijana.

Vifungu vilivyo kiukwa kikanuni na kikatiba ni vifuatavyo:-


Makonda amekiuka katiba ya CCM Ibara ya 14(4) Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo “Haki ya kujitetea au kutoa maelezo mbele ya kikao cha CCM kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake.

Pamoja na haki ya kukata ya kwenda katika kikao cha juu zaidi cha CCM kama kipo endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa”


Kwa kuwa kifungu hiki kinatoa fulsa kwa Mwanachama kujitetea juu ya tuhuma zinazomkabili.


Je Chama cha Mapinduzi kiliwahi kumuita Mh. Edward Lowassa na wengineo wote wenye kashfa za rushwa na kutangaza nia ya Urais kumhoji na kumsikiliza na Chama kufanya maamuzi? Lakini kutoa matamko kupitia kofia ya Chama ni makosa makubwa yaliyofanywa na Makonda na anapaswa awajibishwe. Tunamshangaa pia Mzee Malecela kuunga mkono mtu aliyekiuka haki za mwanachama na utaratibu wa Chama. Huu ni ukweli kuwa tegemeo la Wazee wa CCM kusimamia haki na wajibu wa Chama umetoweka.


Lakini pia Mzee Malecela anamtuhumu Edward Lowassa kuchangia harambee, kugawa tisheti na kutoa misaada katika nyumba za Ibada Kanisani na Misikitini. Mbona wapo wanachama wengi wanaofanya harambee kama hizo mfano ni Benard Membe, Sumaye, Samwel Sitta na January Makamba wao pia wanatenda matendo ayatendayo Lowassa mbona hawajatolewa matamko.

Wametengeneza hadi na kalenda kama sehemu ya kujinadi mwaka 2015. Kwa nini hawakukemewa wote kwa pamoja?.Lakini pia Paul Makonda amewakashifu viongozi wetu wa dini kwa kuwafanisha na wasaka pesa kwahili tunamtaka awaombe viongozi hawa wote msamaha haraka,Vilevile ieleweka viongozi wa dini ni nguzo ya vijana wa taifa hili na uvccm inawathamini na pia tunatoa rai kwa mtanzania yoyote mwenye imani na roho ya upendo na wa dii yoyote kufanya kazi na viongozi wa dini na kujenga nchi pamoja nao,Je Mzee Malecela anaunga mkono Paulo Makonda kuwakashifu viongozi hawa wa dini?.

Tulitegemea sana Mzee kama Malecela angekemea matendo haya kwa wanachama wote lakini ameonesha chuki binafsi kwa ndugu Edward Lowassa.

Lakini hatupaswi kumshangaa maana hata Hayati Mwl Nyerere aliposema kama Mzee Malecela atagombea Urais narudisha kadi ya CCM, Hatukumuelewa Mwl Nyerere alimaanisha nini lakini kwa sasa tumepata picha kamili ni jinsi mzee huyu asivyo na busara na anaweza kukizamisha chama kwa chuki zake binafsi na maneno yake ya kupotosha watanzania.


Mzee Malecela anapaswa kuomba radhi kwa Umoja wa Vijana wa CCM kwa kumuunga mkono Paul Makonda ambaye si msemaji wa UVCCM kwa mujibu wa Kanuni za Umoja wa Vijana. Wasemaji wakuu wa Jumuiya ni Mwenyekiti na Katibu kwa ridhaa ya vikao na maadhimio yaliyofanywa katika vikao wao ndo wenye mamlaka hayo. Lakini pia Makamu mwenyekiti Mboni Mwita amekana kutolitambua tamko la Umoja wa Vijana bali ni la kwake binafsi tunashangaa Mzee Malecela kwa nini anamuunga mkono Paul Makonda.


Tunatoa wito kwa Chama cha Mapinduzi kupiga marufuku matamko yote yanayoendelea nchini na kuwachukulia hatua wale wote wanaotangaza nia ya kugombea Urais kabla ya wakati na tunamuomba Mh. Mwenyekiti wa Chama ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kukemea hali hii kwa nguvu zake zote ili kukisalimisha Chama na kuwepo kwa utii wa Kikatiba. Kuachwa kwa hali kama hii itakuza migogoro na makundi ndani ya Chama.


Imetolewa na Komredi Heri Hoza ni Kada wa muda mrefu wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya baraza la Umoja wa Vijana wa ccm Mkoa wa Morogoro. Pia ni Mwenyekiti wa CCM wa tawi jipya la Chuo Kikuu huria (Morogoro branch).
 
Hili sakata linanipa raha sana. Na hili ni trela picha kamili bado. Nasikia huyu mzee EL ameapa kuwa lazima agombee Urais ili alipe visasi asipopendekezwa na CCM atakuwa mgombea binafsi. Kazi kwenu CCM.
 
EL lazima awe rais....kuna yule wa mwandiga yeye sijui atagombea kupitia chama gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom