UVCCM kwachafuka

Makonda aliyekuwa akizungumza kwa hisia jukwaani alisema ikiwa UVCCM wanataka kujenga taasisi yenye nguvu na inayoaminika, lazima wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaua demokrasia.
“Uchaguzi tulioufanya hatukumchagua Sadifa wala Mboni, bali tumechagua uongozi wa aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa tutarajie jumuiya hiyo…. kama sikueleweka historia itakuja kutuambia maana ya maneno haya,” alisema Makonda na kuongeza:
“Kama kuna mtoto wa maskini, mtoto wa mkulima kama mimi amechagua au kupiga kura yake kwa sababu ya rushwa, basi ajue amepanda mbegu maishani mwake.”
Baada ya Makonda kutoa kauli hizo alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja nje ya ukumbi ambako baadhi ya wapambe wake walimfuata na kuanza kulia machozi.
Baadhi yao walisikika wakisema kwamba UVCCM wameisaliti demokrasia kutokana na nguvu ya fedha. Hata hivyo, Makonda alikuwa akiwafariji kwa kuwaambia wasife moyo.
 
  • MADAI YA RUSHWA YATAWALA,
  • MALISA, SHIGELLA, BASHE, NYALANDU WATUHUMIWA,
  • MAKONDA ATOA KAULI NZITO
MATOKEO ya uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) yametangazwa jana huku kukiwa na harakati za kuyapinga kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

Kati ya mambo yaliyotajwa kupindisha taratibu za uchaguzi huo uliofanyika juzi ni kile kilichoelezwa kuwa ni kutawaliwa na vitendo vya rushwa.

Baada ya Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutangaza matokeo, baadhi ya vijana waliyapinga na kuanza kukusanya saini 340 ili kuyapinga.

Katika kuonyesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, baadhi ya wajumbe walibeba mabango yenye ujumbe wa kutokubaliana na matokeo, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein baada ya kumaliza kufunga mkutano huo.

Moja ya bango hilo lilikuwa na maneno: “Jumuiya si ya Lowassa na wafuasi wake (Benno, Bashe, Zungu, Zabein…..) hivyo jumuiya itakuwa na kambi mbili ya kwanza jukwaani na kambi ya mezani.”

Bango jingine lilisomeka: “Jumuiya imara hujengwa na uchaguzi wa haki na siyo rushwa za Bashe, Benno na Zungu.”

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ni miongoni mwa makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kambi yake imekuwa ikitajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Kwa tafsiri ya mabango hayo, Benno (Malisa) alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Bashe (Hussein) naye alikuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo ambaye amemaliza muda wake
.
Maofisa usalama na walinzi wa jumuiya hiyo ambao walikuwa wakijaribu kuwanyang’anya vijana hao mabango walishindwa, hivyo kulazimika kusubiri dakika kama tano hivi hadi msafara wa Dk Shein ulipoondoka walipowatoa nje ya eneo la ukumbi wa mkutano
.
Tukio hilo lilizua tafrani baada ya walinzi hao kuwanyanyua juujuu vijana wawili kati ya sita waliokuwa na mabango, huku wengine wakionekana kutaka kuwapiga lakini polisi waliingilia kati na kuwatoa nje.

Baadaye polisi waliondoka na vijana watatu katika tukio ambalo lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu na baadhi ya wagombea ambao walishindwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa UVCCM.

Vijana walalama

Mapema jana asubuhi, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walikutana na waandishi wa habari na kulalamika kwamba rushwa ilitawala huku wakiwatuhumu viongozi wa UVCCM na baadhi ya makada wa chama hicho kwa kuhusika na vitendo hivyo.
Waliotajwa ni pamoja Malisa, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, Bashe na mtoto wa Lowassa, Fredy.

“Kama Rais Jakaya Kikwete kweli yuko makini na kauli zake ni za dhati, basi atengue matokeo ya uchaguzi huu maana kanuni zimekiukwa na kusema kweli rushwa ilitawala. Atumie nafasi yake kurejesha hadhi ya chama, huu uchaguzi ni batili,” alisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Morogoro, Augustine Matefu.

Walidai kuwa Bashe ndiye aliyekuwa mratibu wa uingizaji wa fedha katika eneo la mkutano ambazo zilitumika kugawanywa kwa wajumbe na kwamba Malisa na Shigela waligawa Sh1 milioni kwa viongozi wa mikoa kama hatua ya kumpigia kampeni mmoja wa wagombea walioshinda.

Kada mwingine, Livamba Adinan Selemani alisema: “Vijana kweli tumempuuza Rais, kweli mtu ambaye hana hela hawezi kupata uongozi UVCCM, kwa maana nyingine nchi yetu inakwenda pabaya. Watu wachache wenye fedha wanaweza kuamua kufanya wanachotaka, hivyo ndivyo uchaguzi wetu wa vijana ulivyokuwa.”

Mjumbe mwingine, Kichanta Selemani alisema malalamiko ya viongozi wa UVCCM kuwapendelea baadhi ya wagombea yalifikishwa kwa Lukuvi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Wakati makada hao wa CCM wakizungumza na waandishi wa habari, lilitokea kundi jingine la makada wa chama hicho ambao walianza kuzozana na wenzao wakisema kuwa malalamiko yao yanatokana na kushindwa na kwamba walitaka kutumia: “Viongozi wa ngazi za juu za CCM” kuwachagulia vijana viongozi.

Kundi hilo la pili lilidai kuwa katika uchaguzi huo kundi hilo la kwanza ndilo lililohonga fedha na kumtaja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwamba alikuwa akiwashawishi wajumbe kwa fedha kumchagua mmoja wa wagombea.

Akizungumzia tuhuma hizo, Nyalandu alisema kupitia ujumbe wa simu yake ya mkononi: “Mimi siyo mjumbe wala mgombea na wala sihusiki kwa lolote. Nilikwenda ukumbini na waziri mwenzangu na baadaye tukaondoka pamoja. Hao ni waongo wakubwa na wazushi wachache wanaonunua haki.”

Hakuna mtu yeyote niliyeongea naye wala kutoa hela yoyote kwa sababu zozote zile na tulikuwa ukumbini baadaye nje wote pamoja (na waziri). Shame to them who lie (aibu kwao wanaosema uongo) na wataje majina yao tuyasikie.”

Alimtaja Waziri aliyekuwa naye kuwa ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tzeba kwa lengo la kuwasalimia vijana ambao walikuwa wakiendelea na mkutano wa uchaguzi.

Watuhumiwa wanena

Kwa nyakati tofauti, wakijibu tuhuma hizo watuhumiwa wote walikanusha kuhusika kutoa rushwa na kuwataka wanaolalamika kupeleka ushahidi wao Takukuru na kufikisha malalamiko hayo katika vikao vya ulinzi na maadili vya CCM.

Shigela kwa upande wake, akizungumza na waandishi wa habari alisema kinachotokea sasa kuhusu tuhuma hizo kilitarajiwa kwani ni kawaida watu wanaposhindwa katika uchaguzi kutoa malalamiko hata kama hawana ushahidi wa tuhuma husika.

Shigela alikanusha yeye na Malisa kutoa fedha kwa viongozi wa mikoa akisema kwa nafasi yake asingeweza kupata fursa ya kufanya hivyo kwani alikuwa mratibu mkuu wa uchaguzi kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.

“Kama kuna watu hawakuridhika kuna taratibu za chama inabidi zifuatwe, kwa mujibu wa taratibu zetu kuna siku 14 za malalamiko na hizo mtu anaweza kuzitumia kuandika malalamiko yake na yapelekwe kwa viongozi wahusika ili wachuke hatua,” alisema Shigela na kuongeza:

“Vinginevyo taratibu za chama haziruhusu kutoa au kupokea rushwa kwa namna yeyote, kwa hiyo kama mtu anadhani ana uwezo aitumikie jumuiya popote pale alipo kwa sababu wote hatuwezi kuwa viongozi kwa pamoja.”

Kwa upande wake, Malisa alisema: “Nimefanya kazi yangu na kutekeleza wajibu wangu kwa ukamilifu, kama kuna jambo lolote ambalo linahusu UVCCM, basi kamuulizeni mwenyekiti wa jumuiya maana yupo.”

Bashe alikanusha kuhusika na vitendo vya rushwa na kuwataka wanaotoa madai hayo, kama wana ushahidi waupeleke Takukuru au kufikisha suala hilo katika vikao vya chama hicho.

“Waambieni kwamba wasilete siasa za shule za sekondari UVCCM, maana kama wangeshinda ni dhahiri kwamba wasingelalamika. Ninawapa ushauri wa bure, kwanza kama wana ushahidi wa madai hayo kwamba mimi Hussein nimetoa rushwa, basi wapeleke ushahidi wao Takukuru lakini pia ndani ya chama tunayo Kamati ya Maadili na Usalama wapeleke malalamiko yao huko ili yafanyiwe kazi.”

Alisema hawezi kujihusisha na rushwa kwani hata Rais Kikwete katika hotuba ya ufunguzi alikemea vitendo hivyo.

Fredy akizungumza kwa simu alisema: “Tuhuma hizo siyo za kweli kwani mimi licha ya kwamba nilipata barua ya mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo sikuenda Dodoma kutokana na kubanwa na kazi.

“Kwanza mimi si mjumbe wa mkutano mkuu japokuwa ni Katibu wa Uhamasishaji wa Mkoa wa Arusha. Nilipata mwaliko lakini sikuweza kufika huko (Dodoma) nimetingwa na kazi nyingi,” alisema.

Matokeo ya uchaguzi

Lukuvi alimtangaza Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM baada ya kupata kura 483.

Sadifa alimshinda Rashid Simai Msaraka aliyepata kura 263, wakati mgombea mwingine Lulu Msham Abdallah licha ya kujitoa katika kinyang’anyiro hicho muda mfupi kabla ya kura kupigwa, alipata kura nane.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mboni Muhita alishinda katika duru ya pili baada ya kupata kura 489 na kumshinda, Paul Makonda aliyepata kura 241.

Katika duru ya kwanza, Mboni alikuwa amepata kura 361 na Makonda kura 206, huku mgombea mwingine Ally Salum Hapi akipata kura 179. Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya wagombea wote kutofikisha nusu ya kura kama kanuni zinavyotaka.

“Sheria kushindwa kwa heshima kuliko kushinda kwa fedheha.”

Makonda aliyekuwa akizungumza kwa hisia jukwaani alisema ikiwa UVCCM wanataka kujenga taasisi yenye nguvu na inayoaminika, lazima wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaua demokrasia.

“Uchaguzi tulioufanya hatukumchagua Sadifa wala Mboni, bali tumechagua uongozi wa aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa tutarajie jumuiya hiyo…. kama sikueleweka historia itakuja kutuambia maana ya maneno haya,” alisema Makonda na kuongeza:

“Kama kuna mtoto wa maskini, mtoto wa mkulima kama mimi amechagua au kupiga kura yake kwa sababu ya rushwa, basi ajue amepanda mbegu maishani mwake.”

Baada ya Makonda kutoa kauli hizo alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja nje ya ukumbi ambako baadhi ya wapambe wake walimfuata na kuanza kulia machozi.

Baadhi yao walisikika wakisema kwamba UVCCM wameisaliti demokrasia kutokana na nguvu ya fedha. Hata hivyo, Makonda alikuwa akiwafariji kwa kuwaambia wasife moyo.

Chanzo: Mwananchi
:target:pambafu kabisa! mafi ga ng'ombe.
 
Lowassa anautaka urais kwa gharama yoyote! Hii ni hatari sana! Viongozi wa dini mko wapi mjitokeze mkemee kwa nguvu zote EL anatumia fedha nyingi kwa faida ya nani? EL umechafuka! Kachunge ng'ombe zako huko Richimonduli!
 
baba yao kalalamika na wao eti wanajilalamisha iv wanafikili malalamiko yao nani atayashughulikia kama baba yao hadi sasa anaendelea kuachia tabasamu tu hajui cha kufanya. kwanza kama hawataki kutoka huko nyinyiem hatutaki kusikia tena utumbo wao. pambavu zao wakojoe wakalale.
 
Rushwa ndio lugha ya CCM.
Huyu Kondakta asijifanye hayajui hayo!!
 
Kwani ukipewa rushwa unalazimishwa kumchagua? mi naona ni maneno ya mkosaji tu.

Falsafa ya kwamba 'chukueni hela yao, kura msiwape' haiko sahihi kwa sababu kadhaa. Hapa nazitaja mbili tu:
1. Inaruhusu watu kutoa na kupokea rushwa, badala ya kukataza vyote kutoa na kupokea rushwa.
2. Inapuuza ukweli uliodhihirika kuwa pesa inaushawishi na nguvu ya kupumbaza mtu akaacha kufikiria vigezo sahihi na sifa za uongozi, na badala yake kuhamasisha uamuzi kufuatana na matakwa ya mtoa pesa.
Kwa kiwango cha uhitaji, umasikini na ujinga uliopo, ni wachache sana wanaoweza kuchukua hongo na wakabaki na maamuzi yao yasiyoathiriwa na hongo hiyo.

Koleo liitwe koleo. Viongozi wahubiri madhara ya rushwa na kuipinga badala ya kutoa hoja dhaifu na ya kukosa matumaini kama kusema 'pesa yao chukueni, bali msiwachague'. Waitoao hiyo hela wanaijua nguvu yake, na matunda yake-si wajinga!
 
“Vinginevyo taratibu za chama haziruhusu kutoa au kupokea rushwa kwa namna yeyote,.....”.

Chanzo: Mwananchi

Haaha , Kwa hiyo ingekuwa sio taratibu za chama yeye angetembeza mlungula siyo?
Mi nafikiri kwa maadili yake ya kama mtu binafsi hapaswi pia kutoa rushwa
 
Sasa imekuwa ni jadi chaguzi zote za CCM zinagubikwa na rushwa ya kutisha, jambo moja linalonishangaza ni pale Takukuru wanaposhindwa kumkamata hata mtu mmoja katika rushwa iliyokithiri na ya wazi kiasi hicho.
Kikwete mwenyewe ambaye anashinda angani nje ya nchi kwa kipindi kirefu ameliona tatizo la rushwa iweje Hosea & co wanaoshinda nchi kavu wanashindwa kuwabaini watoa na wapokea rushwa na kuwapeleka kunako husika.
Kwenye chaguzi za ubunge wakati wa kura za maoni walikamatwa kina Mwakalebela Mama Sitta huko Bukoba mkongwe wa siasa Luhangisa orodha ni ndefu chakushangaza baadae wote walipeta kiaina na mwisho wakagombea na kushinda bila hata chama kuwachukulia hatua zozote za kinidhamu angalau kwa ushahidi wa mazingira.
Hapa ndipo linakuja swali je kuna uhalali gani wakuwa na chombo kama Takukuru, si hilo tu je uwepo wa rais una maana gani kama anaishia kulalama tu badala ya kuchukua maamuzi stahiki au ndio sikio la kufa.
Na hili la Lowasa kuonekana anapenyeza rushwa kwa kila chaguzi za CCM chama chake na Takukuru wanalichukuliaje maanake anaonekana ndiye mweka hazina ya rushwa zote ina maana ni unbwogable au pale Hosea alipomclear na Richmond basi ikawa ni kichaa kakabidhiwa rungu, ni so powerfull mpaka chama chake kinamtetemekea kihivyo if that is a case then we are doomed. Mungu ibariki Tanzania.
 
Hakuna uchaguzi wowote ndani ya ccm ambao rushwa haitatumika labda wa mwenyekiti wa taifa kwa sababu hawamuwekei mpinzani.

Wiki chache zilizopita nilikutana na mama mmoja ambaye nilimfahamu kwa jina moja la Joyce na alikuwa anagombea u-nec wilaya ya Bukoba vijijini pamoja na akina Karamagi na nikamuuliza honestly je anadhani atashinda? akanijibu "ndio" nikamuuliza una shilling ngapi? akasema "kwa kweli sina pesa ila nategemea demokrasia ichukue mkondo wake". Nikampa za usoni kuwa kama mnategemea demokrasia ya ndani ya ccm, then, demokrasia ya kwanza itakuwa ya fedha na atakayeshinda ni mwenye fedha na mwenye fedha kati yenu ni Karamagi kwa hiyo wewe msindikize upoteze muda wako na mshindi ameshajulikana kwa sababu ya nguvu yake kifedha.

Ndivyo ilivyokuwa maana aliangukia pua! Na kilio kwa wagombea wote walikuwa wakililia rushwa..oohhh poor ccm members, poleni sana.... maana macho yenu yamekuwa short sighted! CCM ya leo imejaa rushwa na udini. Ni ukweli usio fichika na endeleeni kukimbilia huko mtakuta watoto si wenu. Najua wengi hawapendi kusikia wimbo huu lakini ninashindwa kushindwa kuuimba.

Nawashauri ccm members walio na nia ya kujiendeleza kisiasa amieni upinzani tushirikiane tuondoe monster huyu ccm rushwa na mauaji nchini!
 
Walipiana Bao ni kiasi cha Rushwa walichotoa tu otherwise UVCCM na UVMCCM wote ni wezi na watoa Rushwa
 
Back
Top Bottom