Uvamizi wa Eneo Meru na Mahojiano na Aloyce Kimaro (MB)

Mkuu,
Kwenye suala la ARDHI nawaomba sana Watanzania wenzangu, Bunge letu, Mahakama yetu, Vyombo vya habari na Serikali yetu tubaki WAJAMAA. Hili ni moja kati ya mambo mema kabisa alilotuachia MWALIMU.

Mkuu labda ulalamike ulitaka kununua ardhi ukanyimwa pasipo sababu. Hata sasa ukitaka mkuu Wilcard kumiliki ardhi haukatazwi. Kuna wengi wana nga'ang'ania kumiliki ardhi na hawaifanyii chochote. Mfano leo hii mkuu Wilcard upewe shamba ambalo halilingani na uwezo wakoo, utaweza kuliendeleza? Au utaacha tu majani yaote kwenye ardhi? Na unaupenda ujamaa sasa hivi je wakija kuchukua mali zako, hata kama ni kidogo, katika jina la ujamaa uta kubalii?
 
Hapo nilipoweka highlight ndiyo penyewe mkuu. Mimi siyo fisadi, kupitia biashara zangu na familia yangu pamoja na kazi yangu nitanunua mashamba mpaka niseme hapa basi. Mashamba nitakayoacha hapa duniani nataka yatoshe hadi kizazi cha nne maana watakapozaliwa watakuta hakuna ardhi tena ya karibu!!!! Nimeamua na hakuna wa kuniita fisadi!!! Shamba tii na title deed tiiii. Hapa sina mjadadala, sheria inaniruhusu niwe na ardhi na sheria hiyohiyo imempa Rais ku-revoke tu and not otherwise. Unajua kila binadamu huwa na hobby yake, mwingine akipata pesa nyingi anaoa wake 12 plus, leaving apart concubines!!!! Hawajui those are like parasites or eroders!!!! Invest for returns!!!!

Ardhi nayo ni mali tena ni urithi mkubwa sana kwa watoto wako na kizazi chako kijacho. Kama una pesa uliyo itolea jasho mkuu wewe miliki kiasi chochote cha ardhi uki takacho. Moja ya haki ya kuwa Mtanzania ni kumiliki ardhi. Ina bidi tukubali ukweli kuwa hata tukiondokana na ufisadi na rushwa bado kutakua na wananchi wenye nazo zaidi ya wengine. Hakuna jamii ambayo watu wote wana uwezo sawa, thats impossible and not practicle. Hayo maisha ya kila mtu kuwa sawa labda mbinguni tu. Tuwe wa kweli kuwa sisi sote tuna taka kuendelea kimaisha lakini pia sisi sote hatu wezi kuwa na hali sawa ya kimaisha hata siku moja. Tuongelee kuwa wezesha walio masikini lakini si kuwa punguzia walio tajiri. The answer is in empowering the poor not impoverishing the wealthy.
 
Kimaro ni fisadi sasa anatafuta mchawi je ni wafanyabiashara wenzake kina minja wa duty free arusha dar na nairobi aliowarusha wakati wakigawana mali pamoja na sumaye au ni kina zadock aliowatosa mara baada ya ubunge
 
Wildcard,
Hii ni changamoto kwa matajiri/wenye nacho wa nchi yetu. Pamoja na kwamba siafikiani na kitendo cha wananchi kuvamia shamba la Mhe. Kimaro bado tunapaswa kuwaangalia na kuwadadisi wenzetu 'waliobarikiwa'. Je ni kwa kiwango gani katika kujitwalia ardhi na kupata mali waliyonayo kutoka nchini mwetu wameweza kuwafikiria wananchi wenzao na kuwasaidia ipasavyo?

Kijijini kwetu enzi hizo alikuwepo Mgiriki mmoja aliyekuwa na shamba kubwaaaaaa la mkonge. Mgiriki huyo alizungukwa na wananchi wa kawaida na wale waliokuwa wafanyakazi kwenye shamba lake. Tulipopata Uhuru, wapo Wagiriki ambao hawakupenda kutawaliwa na ngozi nyeusi na ambao hawakukubaliana na siasa ya Ujamaa waliondoka kurudi makwao. Mashamba yao yalichukuliwa na Serikali. Mgiriki ninayemzungumzia hakuondoka alibaki nchini na akafia hapahapa nchini. Kwa kipindi chote alichokuwa akimiliki shamba lile alitoa ruksa kwa wananchi kulima mazao yao katikati ya mistari ya mkonge. Hatimaye hata Mameneja wa mashamba ambayo yalitaifishwa na Serikali walifuata nyayo za Mgiriki na kuwaruhusu wananchi wanaozunguka mashamba hayo kulima ndani yake. Huyo alikuwa Mgiriki mwenye utu aliyejali majirani na wafanyakazi wake!

Na sisi tunaojiita Wazalendo lakini matajiri tuliohodhi mamia ya ekari wakati wananchi wenzetu hawana hata kipande cha ardhi, hilo la kuamua kuwasaidia wenzetu kwa kuwagawia eneo la kulima bila masharti tunaliweza?

Pamoja na hayo yote, Tanzania yetu ni kubwa, ina ardhi kubwa ya kutosha. Nakumbuka enzi hizo, watu wa Kilimanjaro waliwahi kudai mbele ya Mwalimu Nyerere kwamba baadhi yao hawana ardhi. Mwalimu akawaambia Tanzania ni kubwa mno akawashauri wahame waende mikoa mingine yenye ardhi ya kutosha. Leo hii kila kona ya nchi huwezi kumkosa Mchagga aliyeridhika kuishi mkoa mwingine na kuendesha maisha yake kwa mafanikio badala ya kushawishika kwenda kumvamia Mhe. Kimaro!

Mkuu Bibi Ntilie, ni kweli kuwa wakati mwingine ni lazima tusaidiane ili tuweze kuweka usawa na kuboresha maisha yetu. Njia za kufanya hivyo ni nyingi, ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii.

Kuna wakulima wengi tu ambao hutoa fursa ya watu wanaotaka kulima kwenye mashamba yao kufanya hivyo. Nia yao kuu ni kupata nafuu ya kuyatunza mashamba hayo kwa kuhakikisha kuwa ni masafi kwa kipindi kirefu na kwa gharama nafuu. Vile vile, wengine hufanya hivyo kuepuka gharama za kuyapalilia mashamba yao na kazi hiyo kuwa imefanywa na wananchi wenye nia ya kulima mazao yao. Vyovyote iwayo huwa na win-win kwa wote wanaohusika. Ni jambo jema na lenye tija kusaidiana hivyo hata kama sababu nilizozitoa hapo juu si za msingi. Kusaidiana ndio sababu ya kuwa pamoja katika ulimwengu huu.
 
Hili shamba nalifahamu sana. Mhe. Kimaro ameuziwa ekari 50 tu kwa ajili ya Hoteli yake ya kitalii. Sehemu kubwa iliyofyekwa na hawa wavamizi ni ile iliyokuwa na migomba ya Utafiti unaoendelezwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Kanda ya Kaskazini ilioko Selian. Hii ni kama Serikali imevamiwa.
Hawa watu wanafahamu kuwa kuna eneo la ekari 25 lililotengwa kwa ajili ya kujenga shule ya Sekondari. Kwa hiyo si kweli kwamba Kata ya Singisi wamekosa mahala pa kujenga shule. Inaonekana hii ni chuki wa "wageni weusi", au ni vijana wanaodhani kila mtu mwenye fedha ni fisadi. Mhe. Kimaro anajulikana anapiga vita ufisadi Tanzania.

Jambo ambalo lingewekwa wazi na Serikali ni bei iliyolipwa na Mhe. Kimaro. Huenda "ufisadi" ukajificha katika uuzaji wa eneo hilo. Wakati Wameru wanashauriwa wahamie Wilaya ya Kilindi, Mkoani Tanga ambako wanahofia kuna malaria, huenda wakubwa kama Mhe. Kimaro wanauziwa ardhi ya hapa Meru kwa bei poa.

Mkuu Kilasara, bei ya shamba haiwezi kusababisha uhalali au kuondoa uhalali wa kumiliki shamba lenyewe. Serikali inaweza kutoa ardhi bure au kwa gharama ndogo ili nia ya uendelezaji wa ardhi hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ifikiwe. Inawezekana kabisa kuwa Mhe. Kimaro alipewa ardhi hiyo bure au hata alilipa fedha ambazo kwa maoni yako ni kidogo, ila kwa wakati aliopewa na kwa mikakati iliyokuwepo ikaonekana (kwa serikali) kuwa inatosha.
 
Its obvious and its high time tusome ALAMA ZA NYAKATI - wananchi kujichukulia sheria mkononi sio mara ya kwanza - hata MAFISADI walioiba mamilioni ya fedha wakati wananchi wanataabika itafika siku WATAPIGWA MAWE WAKIPITI NJIANI kwani TAIFA LETU LINA SHERIA ISIYOFANYA KAZI KWA WOTE - BALI WANYONGE TU - HAIWEZEKANI WANANCHI WANAOFIKIA 80 WANUNULIWE WOTE ETI WAKAHARIBU MALI YA MTU - HIYO INGEFANYWA NA FEW PEOPLE (WAHUNI) -
Mkuu Preacher, kama tunaamini kuwa kuna watu hununua shahada za kupigia kura, kwanini tudhani kuwa haiwezekani kumobilize watu 80 kufanya fujo? Kama tunaamini kuwa kwenye maandamano kuna watu hupewa pesa ili kushiriki maandamano hayo (tena pesa kidogo tu), kwanini tusiamini kuwa ni rahisi kumobilize watu 80 kufanya hivyo? Kama tunaamini ni rahisi kumshawishi mtu kuuza mwanae (zeruzeru) kwanini tusiamini kuwa ni rahisi vile vile ku-mobilize watu 80 tu kufanya fujo. Mkuu, wanaharakati za kukomoana, kufikia malengo yao wana uwezo mkubwa sana. Wana mbinu za ajabu za kufanya wayatakayo yatimie. Sitashangaa kusikia watu wanaotuhumiwa na Ufisadi kuwa kiungo katika issue hii. Sitashangaa pia kuwa hasira za kweli zilisababisha haya kutokea. All in all, these people were mobilized by a certain number of people for intentions known to themselves. Haiingii akilini ni kwa jinsi gani watu hao wanaweza kujikuta wamefika wote katika eneo la mtu na kuanza kufanya uharibifu walioufanya bila kuwa mobilized. Au wewe unadhani vipi Mkuu?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu nakuaminia lakini imekuwaje uanze kuhoji hatua ya wananchi badala ya kuhoji chanzo cha mgogoro huu. Hawa wanakijiji inawezekana wanayafuata mafundisho yako..Wamechoka kusubiri system ambayo haifuati sheria na pengine hakuna sheria iliyo juu ya Kimaro..Hivyo wanapigana na Ufisadi kwa jinsi wanayoijua wao kuwa bora...wamefikia hatua wanajua serikali haiwezi kufanya kitu..
La muhimu tuwaulize wananchi... na kama umeweza kumpata Kimaro unaweza pia kumpata mwakilishi wa kundi hili, bila shaka Kimaro atakuwa anawafahamu..pitia kwake upate kusikia pande zote mbili kabla hujahukumu..
 
Serikali ichunguze vizuri suala hilo la uvamizi wa Shamba la Kimaro kuna ajenda iliyojificha nyuma yake.
 
Penye njaa hakuna amani, viongozi wetu lazima waelewe kuwa watu wana njaa hivyo amani haiwezi kuwepo. Hao wananchi, wawe wametumwa au hawajatumwa tatizo ni njaa, nao wanahitaji shibe ambayo watawala hawaoni kuwa nao wanastahili.

Uzaji mashamba TZ hivi sasa una harufu ya ufisadi na wananchi wanafahamu. Ikumbukwe kwamba hiyo ardhi ilichukuliwa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo, serikali inaposhindwa ilipaswa kuwashirikisha wananchi wa eneo husika kuepusha migogoro.

Mzindakaya aliuziwa shamba la Nkundi kule Sumbawanga kwa milioni 30 tu, shamba ambalo lilikuwa kituo cha kilimo likiwa na ukubwa wa hekta 6,000, nyumba za watumishi, miundombinu ya umwagiliaji na ng'ombe bora. Shamba la Kapunga wilayani Mbarali kauziwa expot traders kwa shilingi bilioni 2.5 wakati uwekezaji unaelezwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni 80 za wakati ule, wananchi waliomba wauziwe na CRDB walikuwa tayari kuwakopesha hata zaidi ya shilingi bilioni tatu, wakanyimwa. Leo hii wapo wahindi pale wameshindwa kufikia uzalishaji wa wakulima wale wadogo.

Shamba la Mbarali nalo imeuziwa familia ya kina Mulla kwa bei ya kutupwa, shilingi bilioni 2.5 na kuwakatalia wananchi

Mifano iko mingi, hivyo kwa suala la Kimaro ni vema tukaliangalia kwa upana wake, kwani wakati Mzindakaya anauziwa shamba la Nkundi hata uongozi wa mkoa haukuhusishwa, jamaa alifika na nyaraka zote, na ndio maana kina Kimiti walipinga, lakini wakakutana na ukuta wa kina EL.

Katika kuhakikisha kuwa wananyamazisha kelele za kina Kimiti, EL aliongozana na kundi la wahariri kutoka DSM ambao walishuka na makala za kusifia uwekezaji wa Mzindakaya, mtindo uliotumika hata kwenye shamba la Kapunga pale ilipobainika kuwa wale wawekezaji ni feki, walichukuliwa waandishi wa habari kutoka DSM ili wasifie uwekezaji uliopo pale Kapunga.

Wa kulaumiwa ni viongozi wetu, ni walafi, wanakula bila kunawa, hao wananchi wana haki ya hiyo ardhi japokuwa wametumia njia isiyo stahili, lakini hii ni kutokana na serikali yenyewe kutowasikiliza na kuwajali wananchi wake.
 
Penye njaa hakuna amani, viongozi wetu lazima waelewe kuwa watu wana njaa hivyo amani haiwezi kuwepo. Hao wananchi, wawe wametumwa au hawajatumwa tatizo ni njaa, nao wanahitaji shibe ambayo watawala hawaoni kuwa nao wanastahili.

Uzaji mashamba TZ hivi sasa una harufu ya ufisadi na wananchi wanafahamu. Ikumbukwe kwamba hiyo ardhi ilichukuliwa kutoka kwa wananchi wa maeneo hayo, serikali inaposhindwa ilipaswa kuwashirikisha wananchi wa eneo husika kuepusha migogoro.

Mzindakaya aliuziwa shamba la Nkundi kule Sumbawanga kwa milioni 30 tu, shamba ambalo lilikuwa kituo cha kilimo likiwa na ukubwa wa hekta 6,000, nyumba za watumishi, miundombinu ya umwagiliaji na ng'ombe bora. Shamba la Kapunga wilayani Mbarali kauziwa expot traders kwa shilingi bilioni 2.5 wakati uwekezaji unaelezwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni 80 za wakati ule, wananchi waliomba wauziwe na CRDB walikuwa tayari kuwakopesha hata zaidi ya shilingi bilioni tatu, wakanyimwa. Leo hii wapo wahindi pale wameshindwa kufikia uzalishaji wa wakulima wale wadogo.

Shamba la Mbarali nalo imeuziwa familia ya kina Mulla kwa bei ya kutupwa, shilingi bilioni 2.5 na kuwakatalia wananchi

Mifano iko mingi, hivyo kwa suala la Kimaro ni vema tukaliangalia kwa upana wake, kwani wakati Mzindakaya anauziwa shamba la Nkundi hata uongozi wa mkoa haukuhusishwa, jamaa alifika na nyaraka zote, na ndio maana kina Kimiti walipinga, lakini wakakutana na ukuta wa kina EL.

Katika kuhakikisha kuwa wananyamazisha kelele za kina Kimiti, EL aliongozana na kundi la wahariri kutoka DSM ambao walishuka na makala za kusifia uwekezaji wa Mzindakaya, mtindo uliotumika hata kwenye shamba la Kapunga pale ilipobainika kuwa wale wawekezaji ni feki, walichukuliwa waandishi wa habari kutoka DSM ili wasifie uwekezaji uliopo pale Kapunga.

Wa kulaumiwa ni viongozi wetu, ni walafi, wanakula bila kunawa, hao wananchi wana haki ya hiyo ardhi japokuwa wametumia njia isiyo stahili, lakini hii ni kutokana na serikali yenyewe kutowasikiliza na kuwajali wananchi wake.
Sasa tujiulize kwa nini livamiwe la Kimaro na si za wengine,au Wameru tu ndio hawana Ardhi?EL ana ranchi huko Handeni aliyopata kwa njia hiyo hiyo Mbona haijavamiwa au Handeni hawana shida ya Ardhi?Tafakari na uchukue hatua.
 
Anatafutwa mtu wa kusingiziwa tu.
Kesho Mh. Kimaryo kama zake zitamwishia na kutangulia, basi pia atatafutwa mtu wa kusingiziwa.
 
Nsesi,
Mkuu taarifa kama hizi ndizo hujenga hoja.. shukran sana umetufunua macho wengine..
 
Mwanakijiji hayuko professional kabisa, hili swala kulichukulia kishabiki kama mancester na arsenal.
mwana kijiji anasema ameshtushwa ukimya, c'mon mwanakijiji!! ukimya gani wakati askari wameenda kuwadhibiti walioshambulia shamba na mpaka sasa zaidi ya watu 19 wamekamatwa. Mwanakijiji amesahau kuwa shamba la Shukuru Kawambwa limevamiwa just a week ago na hakuna kiongozi aliyelizungumzia hilo, wala yeye mwanakijiji hakufuatilia hilo.
Mwanakijiji anazungumzia kuwa anachojali ni ufuataji wa taratibu. Wewe mwanakijiji, hizo taratibu unataka zianze kufuatwa kuanzi hatua gani? Huu ni mgogoro, kama kufuatwa kwa taratibu ni lazima zifuatwe tangu mwanzo. Unapoanzia kwenye wanakijiji kufuata taratibu bila kufanya utafiti juu ya jinsi Mh. Kimaro alivyomilikishwa hili shamba unakuwa umechemsha na unajiabisha.
Labda mwanakijiji hajui maana ya hekari 500, hekari 500 ni sawa na viwanja 416 vya mpira. Ebu jiulize wewe Mwanakijiji kuna jinsi gani mtu anaweza kumilikishwa viwanja 416 vya mpira katika kijiji ambacho kina uhaba wa ardhi?Tena mtu huyo sio mkazi wa hicho kijiji!Tena kijiji chenyewe hakina hata uwanja wa kujenga shule.
Wewe mwanakijiji acha kwenda kama kitabu au kama kompyuta iliyowekwa kwenye program, jiruhu kuona maisha ya ukweli.
Mwanakijiji unatakiwa uipitie vizuri historia ya Meru kabla ya kuwajudge wananchi wake.Matatizo ya Ardhi Meru yapo tangu enzi za mkoloni.
Hakuna kati yetu anayependa vurugu, ila tunapoona vurugu zinatokea ni lazima tuangalie kwa mapana na marefu yake.
Hii interview yako imekaa kikabaila zaidi.
 
Yaani wewe Mwanakijiji na Mh. Kimaro ndio mnadanganyana kuwa hoteli ikijengwa inakuwa ya wanancho wa Arumeru?
Mh. Kimaro anakiri kuwa na hekari elfu 30. Look at this closely kama ana hekari elfu 30 kuna haja gani ya kugombania hekari 500 za Arumeru?
 
Yaani wewe Mwanakijiji na Mh. Kimaro ndio mnadanganyana kuwa hoteli ikijengwa inakuwa ya wanancho wa Arumeru?
Mh. Kimaro anakiri kuwa na hekari elfu 30. Look at this closely kama ana hekari elfu 30 kuna haja gani ya kugombania hekari 500 za Arumeru?

Mkuu ZeMarcopolo, ninavyojua ni kwamba, mtu anapokuwa na mali nyingi ndivyo anavyohitaji zaidi. Inawezekana kuwa Kimaro ana ekari 30K ambazo hazina thamani ya hizo 500 alizonazo hapo Arumeru. Ardhi ya Arusha ni mali mkuu.
 
Jamani lets be honest. This is so bad for the image of our country. Tanzania is not going anywhere without Investments regardless of who is investing in our country. It is important that people are sensitized and educated on the pros and cons of investments. This has become quite a trend. it damages our image abroad and for future investors. Who would want to invest such a chaotic environment. Mwanakijiji thanks a whole lot for initiating this conversation. I just pray that this was wananchi themselves taking matter on their hands and it was not an inside job. If it is then lets not be surprised when one day there would be no one interested in investing in Tanzania at all.
God bless Tanzania
 
Nsesi,
Mkuu taarifa kama hizi ndizo hujenga hoja.. shukran sana umetufunua macho wengine..

Mkuu Mkandara,

alichokisema Nsesi hapo juu ni haki kabisa,, na kwa kuongezea ni kwamba huyo mwekezaji wa KAPUNGA kule mbarali badala ya kulima mpunga, akaanza kutaka kulima mazao ya nishati (biofuels) na alikuwa na vitalu kabisa! Nasikia sirikali imempiga stop, ila kilichopo ni kwamba hakuna uzalishaji wa maana unaoendelea, jamaa ana kinu alichorithi cha kupembua mpunga unaambiwa kwa afrika vipo vichache cya ukubwa na capacity hiyo, sasa fikiria mtu kapewa shamba la ukubwa wa zaidi ya hekta 3000, ikiwemo miundombinu kama hiyo! Kule nadhani itafika siku wananchi wataamka na mishale na marungu, ni suala la muda tu...

So hapa hatuzungumzii tu sheria, kwamba mtu kapata shamba au asset kisheria, ila LEGITIMACY....sheria yoyote ili ikubaliwe lazima iwe na society's approval au legitimacy, la sivyo kuienforce inakuwa inaleta shida.....kinachoonekana hakuna uwazi na haki katika kuuziana mashamba, na wananchi wanajua ndio maana wengine wanajichukulia sheria mkononi.
 
Mbona wananchi walipojichukulia sheria kwa Ballali hamkulaani? Ndio maana wengine tunaipenda JF, rahisi kweli kweli kuona unafiki mkubwa ulioko hapa.

Kuna mtu mmoja huko nyuma naye alitolea mfano wa kitu kama hicho jibu langu kwake lilikuwa kama yeye hakufanya haina maana hakuna aliyefanya. Sasa mzee kama wewe hukulaani uvamizi wa shamba la Ballali haina maana wote hatukulaani. Rudi usome maandishi yetu. Kanuni ni kanuni tu.
 
Ni kweli wananchi hawatakiwi kujichukulia sheria mkononi na kitendo walichofanya si kizuri lakini nini chimbuko la tatizo? Inaonyesha wazi kuwa wananchi wanao zunguka eneo hilo hwana ardhi ya kutosha. Shamba limevamiwa na karibu wanakijiji 80, nadhani kuna tatizo la msingi. Lazima ifahamike kuwa ubinafsishaji wa ardhi ni tofauti sana na ubinafsishaji wa biashara nyingine.

inaonekana bado unamiss point. Eneo hilo halikutolewa kwa Kimaro tu, kuna wawekezaji wazungu wamepewa pale, kuna wawekezaji wengine wamepewa pale na wengine eneo kubwa kuliko la Kimaro katika mchakato ule ule uliompatia Kimaro eneo. Hawa walalahoi wanakerwa na eneo la Kimaro tu na yale ya wazungu ambayo mengine ni makubwa kuliko ya Kimaro hayawakeri?

Umependekeza hapo nyuma kuwa Kimaro atoe eneo lake kwa Walalahoi, anayegawa ardhi ni Kimaro toka lini? Kwanini, usitake Halmashauri itenge maeneo kwa walalahoi badala ya kumtaka mtu binafsi kufanya hivyo? Au kwanini usiseme wawekezaji wote kwenye eneo hilo la Arumeru watoe maeneo yao kwa kiwango sawa kwa walalahoi, kwanini iwe ni Kimaro tu?
 
Hamjawasikiliza WANANCHI waliovamia shamba hilo wanasemaje. Haiwezekani watu wote wale wakavamia tu bila sababu. Jamani waambieni MATAJIRI wetu hawa wafungue mashamba mapya mbali na walalahoi.

mwizi akija kukuibia utakaa chini kumsikiliza sababu ya kuja kukuibia? ili kiwe nini?
 
Back
Top Bottom