Utoro wa wabunge bungeni hauna tija

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
Hatua iliyochukuliwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Anne Makinda mwishoni mwa wiki hii ya kuwadhibiti baadhi ya wabunge ambao wameonyesha utoro wa kutokuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti linaloendelea sasa bila sababu za msingi, inabidi ziungwe mkono na jamii yote ya Watanzania.

Wabunge wanawajibika kwa vikao vyote vinavyoendelea katika mkutano huo mkubwa ambao sasa unajadili Bajeti Kuu ya Serikali kwa kipindi cha mwaka mpya wa fedha wa 2012/13.

Baada ya Spika kuona utoro kwa wabunge unakithiri, amewataka kuanzia sasa wawe wanaomba kibali kabla ya kuwa nje ya Bunge huku mawaziri nao wakitakiwa kupata vibali viwili, cha Spika pamoja na kutoka kwa Waziri Mkuu.

Spika Makinda hata hivyo, akasema ipo haja ya kufanya upya mapitio kwa wabunge kuhusu kanuni na miongozo, kwani baadhi ya wabunge wamekuwa wakipoteza muda kwa kuomba miongozo au wakati mwingine kutoa taarifa kwa Spika, wakati hata yale yanayoombewa miongozo huwa hayana umuhimu.

Akitoa ufafanuzi zaidi wa kudhibiti utoro kwa wabunge, Spika Makinda alisisitiza kuwa ni lazima wabunge wote wanapokuwa nje ya Bunge, waombe kibali kwake na kuwataka pia mawaziri wafanye hivyo badala ya kuomba kibali kwa Waziri Mkuu peke yake.

Spika aliwapiga stop wabunge 50 ambao walikuwa wamedhamiria kuondoka juzi Ijumaa kwenda kwenye mpira jijini Dar es Salaam na akawataka badala yake waondoke jana Jumamosi. Alifanya hivyo ili mijadala muhimu ya Wizara ya Ujenzi ambayo ilikuwa ikiendelea ipate idadi ya wabunge inayotakiwa

kabla ya kuipitisha. Tunakubaliana kabisa na Spika Makinda kuwakumbusha wabunge wetu kuwa wakati wa kufanya maamuzi ya kupitisha bajeti, miongozo ya Bunge inataka wakati huo, angalau nusu ya wabunge wawepo ndani ya Bunge, vinginevyo utoro wao hauna tija kwa Watanzania wanaowawakilisha.

Ni hatua nzuri hasa ikizingatiwa kuwa mchezo huo umekuwepo kwa miaka mingi sasa na hivyo kuzoeleka kuwa ni jambo la kawaida kumbe kunapoteza nguvu za sauti na michango yao bungeni ambako maamuzi mazito ya mustakabali wanchi yetu hufanyika.

Kwa mfano, hakuna mantiki kabisa pale baadhi ya wabunge wanapotoka bungeni na kusafiri bila ruhusa na kutoka nje ya Dodoma bila kuwa na hofu kuwa wanaweza kupata tatizo huku taarifa za safari hizo wamezifanya kuwa ni siri. Wajiuliza; je, wakipata ajali itakuwaje? Hatuombei lakini inaweza kutokea.

Mchango wa wabunge wote pale bungeni ni muhimu sana. Wapo walioanza vizuri kama alivyosema Spika Makinda katika bunge hilo mwaka 2010, na kwamba yeye aliwaona kuwa msaada kwa Taifa na Bunge lenyewe, lakini hivi sasa wabunge hao anawaona kubadilika na kupoteza mwelekeo.

Bunge limebeba majukumu mazito yenye maslahi kwa wananchi na taifa kwa ujumla, Bungeni si mahala pa kufanyia mzaha, ni mahali panapozalisha sheria na taratibu zinazoongoza nchi, na wanaowajibika na hayo yote ni wabunge wenyewe.

Kinachotegemewa ndani ya Bunge ni mijadala ya nguvu, inayobeba hoja madhubuti kwa faida ya wapiga kura wote. Kitendo cha wabunge kuondoka ndani ya Bunge kwa sababu zozote zile lazima kiwe na ridhaa maalum ili kujenga nidhamu na heshima kwa pande zote, za ndani ya Bunge lenyewe na kwa wananchi waliowapeleka wabunge huko Bungeni.

Kinachoangaliwa hapa ni masuala makubwa mawili, Spika aliwaambia wabunge kuwa yanayotokea Bungeni baadhi yao kila wakati kuomba mwongozo na kanuni au kutoa taarifa kwa Spika, ni hali inayosababisha kupoteza muda wa kujadili mambo ya msingi yenye maslahi kwa wananchi.

Na la pili ni kujenga nidhamu ya uwajibikaji ndani ya Bunge, kwani wabunge wengi wamekuwa wakikatisha mijadala ya wachangiaji wa bajeti mbalimbali na kupisha Spika kutoa mwongozo au utaratibu, jambo ambalo Spika amelilalamikia kuwa ni kero.

Turudie kusema kuwa tunaunga mkono hatua ya Spika Makinda ya kuwadhibiti wabunge, na tunawasihi wafuate taratibu zilizopo na waheshimu mamlaka ya uongozi iliyopo ndani ya Bunge, wanapoanzisha mijadala nje ya utaratibu uliowekwa kisheria, wanapoteza muda wa kuyaweka sawa masuala ya msingi yenye manufaa kwa wananchi.

Tunayo imani kubwa kuwa mijadala ndani ya Bunge itaendeshwa kwa kufuata kanuni na taratibu zote kwani tunaamini pia kuwa wabunge ni viongozi makini wanaotetea maendeleo ya wananchi.

Muda unaotolewa kwa ajili ya majadiliano utumiwe kwa nidhamu ya hali ya juu ili hata baada ya kuahirisha kikao hicho, yote yatakayopitishwa yaweze kutekelezeka kwa ufanisi mkubwa utakaoleta maendeleo kwa taifa.Utoro kwa wabunge wetu uonekane kuwa ni jambo la aibu na lisilo na tija kwa Watanzania.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
kama cdm asaivi wanataka wazunguke mikoani na maandamano yao yasiyo na tija badala ya kutulia bungeni halafu baadaye waanze majungu yao
 
Nimeangalia mwananchi la jana kuna picha waliipiga bungen,ilikua ni viti tupu,even wakat wa mjadala wa asbuhi hakukua na wahudhuriaji kabisa,,,nadhan wabadili kanuni ,wabunge wawe wanaitwa majina as wapo class,
SPIKA:MH.JOSEPH MBILINYI
MBILINYI:NIPO MHESHIMIWA SPIKA,,,,,
KAMA HAYUPO,INAPASWA KIONGOZI WAO ASEME HAYUPO.
EVEN TO MAWAZIRI,LUKUVI NDO ANAPASWA KUSIMAMIA ZOEZ LA KUWAJIBIA MAWAZIRI WASOKUWEPO KWA NIABA YA P.M
THEN MHAGAMA J NAE AWE KWA NIABA YA WANA NYINYIEM
 
Nashauli kuwepo na daftari la majina wawe wanaitwa live mmoja mmoja kama chekechea wanavyoitwa majina.Aliyeomba ruhusa atajulikana
 
Makinda ndo kasababisha watu hawaoni haja tena hata ya kuchangia wala kuhudhuria manake she is not streight.

Amelalia upande mmoja. Akachukue tu mkopo wake wa kujenga nyumba atuachie bunge letu.:wacko:
 
tatizo bunge lenyewe linaendeshwa na mtu feki ndo mana wengi wao wanaona kama wanapoteza time tu mule ndani, ndo maana wanaenda kuspend na wake za watu mpaka wanakamatwa
 
nimeangalia mwananchi la jana kuna picha waliipiga bungen,ilikua ni viti tupu,even wakat wa mjadala wa asbuhi hakukua na wahudhuriaji kabisa,,,nadhan wabadili kanuni ,wabunge wawe wanaitwa majina as wapo class,
spika:mh.joseph mbilinyi
mbilinyi:nipo mheshimiwa spika,,,,,
kama hayupo,inapaswa kiongozi wao aseme hayupo.
Even to mawaziri,lukuvi ndo anapaswa kusimamia zoez la kuwajibia mawaziri wasokuwepo kwa niaba ya p.m
then mhagama j nae awe kwa niaba ya wana nyinyiem

wawekewe vibao jina na jimbo/mkoa/mteule; tv wapewe wapewe jukumu la kuperuzi pia notice board iwekwe majina ya wenye majukumu na ruhusa.then wadanganyika wata judge.
 
Wabunge wengi hasa ccm nadhani wanahimizwa tu kuwepo wakati wa kusema ndiooooo! then waishie na viongozi wakuu wa nserikali wanapozungumza ili wapige makofi
 
If they dont represent the tanzanians in the parliament what do they do?
 
Hilo Bunge ni ovyo kabisa. KUna kamati za bunge zipo ziarani nje ya nchi hivi sasa wakati kikao cha Bunge la Bajeti kinaendelea!

Hawakujua ratiba ya Bunge kiasi cha kupanga safari wakati huu?
 
Hata wakiwapo/wakihudhuria hakuna kinachobadilika/kilichobadilika sana ni upotevu Wa chapaa zetu tu,Bunge la upendedeo Bunge la kutukana halina maana kabisa.
 
Back
Top Bottom