Plato
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 420
- 94
Tangu mwaka 1973 Marekani kupitia case ya Roe Vs Wade utoaji mimba unaruhusiwa kisheria kama haki na uhuru wa mwanamke.kuna kliniki zinazotambulika kisheria zinazotoa watu mimba.daktari aweza kufungwa akikataa kumtoa mwanamke mimba.kwa sasa nchi karibia zote za ulaya zinaruhusu utoaji mimba kisheria,Marekani ya kaskazini yote na nchi nyingi za Marekani ya kusini.Kuna msukumo mkubwa sana kutaka Afrika nayo iruhusu utoaji mimba.Kupitia MAPUTO PROTOCOL.
Tanzania na nchi nyingi za africa zimeidhinisha (Ratified) mkataba huo.kipengele cha 4:2c cha protocol hii kinazitaka nchi wahusika kuruhusu haki za wanawake kutoa mimba.
Je kutoa mimba inaweza kweli kuwa haki ya mwanamke? na je kuruhusu utoaji mimba siyo kuruhusu wanawake na madaktari kuuwa watu wengine kwa sababu hao watu hawana nguvu za kujijitetea? je haki za mwanamke kuchagua zinazidi zile za mtoto kuwa na haki ya kuishi?
Nakumbuka tulivyopiga kelele kuhusu mambo ya ushoga.je kwa nini hatupigi kelele kuhusu kuambiwa turuhusu utoaji mimba? Na tujadili