Wengi wanamlaumu JK juu ya kumteua Prof. Mwandosya kuwa Waziri asiye na Wizara maalum. Nadhani upembuzi huo si sahihi. Mie nadhani JK amemheshimu sana Mwandosya. Kumbukeni Mwandosya bado hajarejesha afya yake vema, na hivyo JK hajampa Wizara kamili ambayo ingehitaji nguvu nyingi. Wengi tungeishia kusema Mwandosya bado mgonjwa kwa nini apewe Wizara kubwa wakati Watanzania wengine wapo.
Alichofanya JK ni sawa na kuamua kumpumzisha Mwandosya huku bado akimweka karibu ili asiwe mbali na yanayojiri katika Baraza la Mawaziri, ikimaanisha bado anahitaji busara za Mwandosya na anaamini atapona kabisa na kuendelea na kazi. Kumbukeni kuna wakati Nyerere alimpumzisha Sokoine akiwa mgonjwa kwa karibu kipindi cha miaka miwili. Sokoine alipopona kabisa ndipo Nyerere akamrudishia Uwaziri Mkuu. JK angempumzisha Mwandosya kwa namna hiyo watu ndio mngesema hata zaidi!
In fact JK kumfanya Mwandosya Waziri asiye na Wizara maalum Mwandosya atakuwa katika ofisi ya Raisi, ikimaanisha atakuwa karibu zaidi na JK kushauriana mambo yanayohusu Wizara yeyote ile. Mie binafsi ninaheshimu sana utendaji wa Mwandosya, na kwa hili alilofanya JK kwa Mwandosya nimeona JK katumia busara sana. Fikirieni kwa makini.
Labda cha kumsihi JK ni kwamba sasa atumie busara na umakini wa Mwandosya kwa namna kubwa hata zaidi kwa kuwa wako ofisi moja; Ofisi ya Raisi.
Ndio maana tunasema serikali hii ya magamba ya kishikaji tu,rais anatoa vyeo kwa huruma? None sense!

....hahah naamini kweli umetumwaUnajuaje kwamba hakomba apumzishwe akaambiwa bado unaweza kuwa na manufaa kwa nchi? Labda uwaulize wale ambao wamekuwa mawaziri, kwamba je, Mwandosya amekuwa na mchango wowote wa busara katika vikao vya Baraza la Mawaziri? Na wakikuambia ndio, jiulize ni jinsi gani JK angeweza kuendelea kutumia busara za Mwandosya katika vikao vya Baraza la Mawaziri katika mazingira kama haya. Kumbuka hata manaibu waziri hawaingii kwenye vikao vya Baraza la Mawaziri.
Mie binafsi nimewahi kushiriki vikao ambavyo Mwandosya amekuwapo, hapa nchini na nje ya nchi. Na nakuhakikishia kwamba that man bwana ana uwezo wa kupembenua pumba akatoa mbegu kwa namna ya pekee kabisa.
Kuna waziri mmoja aliwahi kusema kuna baadhi ya mawaziri hawampendi Mwandosya kwa kuwa akitoa point zake kwenye vikao vya Baraza la mawaziri anafanya waonekane ni watupu mno!
Huyo bwana kichwa, cv yake inasoma bsc eng harafu phd, alifanya thesis ya msc wakampa phd, o lev A zote, A lev A zote!
wabongo bwana..!....hahah naamini kweli umetumwa
Kaongeza nini katika sayansi?
Kuna speech moja katoa kwao huko utumbo mtupu.
Waziri asiye na Wizara Maalum dunia ya leo? Chukulia hata anapotoka nyumban kwake anaagaje; Jaman nakwenda ofcni. Ofic ipi hata yeye hajui
Inawezekana kuna busara katika kufanya hivyo, ila usitumie mifano ambayo siyo sahihi. Nyerere hakumpuzisha Sokoine kwa ajili ya Ugonjwa bali Sokoine alikuwa akienda kusoma elimu ya juu ya utawala huko Bulgaria.