Uteuzi wa January Makamba kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ni uamuzi mbovu sana

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,432
11,100
Nimeangalia video ya January Makamba akila kiapo cha ujumbe wa bunge la Africa mashariki, bado naona ni kiumbe Mchanga sana, kiingereza chake ulimi mzito, confidence mbovu, ni aina ya mtu asiye na exposure yoyote. Afadhari ya Bashe.

Napata shida kwenye meza ya majadiliano tutapigwa za uso Kila sehemu.

Hakika kimataifa sasa taifa linaenda kupotea.

Poleni Watanzania wote.

Ndio hivyo tena

Wadiz
 
Yuko sawa na anaweza...
Achana na wazushi...
Sina imani nae ni Mchanga mno he has not invested a lot on himself especially on language, international confidence, hana context za maana kufit hio nafasi. Tanzania imepoteza sana
 
Kama unaitaka hiyo nafasi sema basi maana upo njema kweny kingereza ,maana ishu za Tanesco sasa hamsemi tena.
 
Huyo mwenzio hafikirii perfomance..anafikiria upigaji..atakuambia zinahitajika trilioni mbili kufanya ukarabati wa balozi zetu..na bibi huwa anamsikiliza utasikia tunakupa kwanza bilioni 500..hutosikia ukarabati wala nini.

Mara ataibuka tena utasikia zinahitajika trillioni 6 ili serikali ijenge balozi zake iachane na hizi za kupanga zinaigharimu serikali..mama utasikia tumeanza ujenzi wa balozi zetu katika nchi saba utaogharimu trilioni 6 na kwa kuanza tumekopa trillioni 2..hilo naomba wizara mlisimamie.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
 
Tatizo serikali inafanya recycling ya mawaziri ni kama nchi hii haina vijana au watu wengine wenye uwezo wa kuongoza.

Yaani mtu alikuwa Wizara ya nishat amefeli ,alafu huyohuyo unampeleka wizara nyingine.

Mtu mmoja anakuwa waziri wa ulinzi,michezo,afya,kilimo huyo huyo sasa sijui kuwa wanajua kila kitu ??
 
Huyo mwenzio hafikirii perfomance..anafikiria upigaji..atakuambia zinahitajika trilioni mbili kufanya ukarabati wa balozi zetu..na bibi huwa anamsikiliza utasikia tunakupa kwanza bilioni 500..hutosikia ukarabati wala nini...
Malaika ni wao acha wale tu
 
Sina imani nae ni Mchanga mno he has not invested a lot on himself especially on language, international confidence, hana context za maana kufit hio nafasi. Tanzania imepoteza sana
Angekuwa hajakaa wizarani ungesema mchanga.
Hayo ya lugha ya kiingereza ni kasumba tu..
Akienda China au Urusi ataongea tu...
 
Tatizo serikali inafanya recycling ya mawaziri ni kama nchi hii haina vijana au watu wengine wenye uwezo wa kuongoza.

Yaani mtu alikuwa Wizara ya nishat amefeli ,alafu huyohuyo unampeleka wizara nyingine.

Mtu mmoja anakuwa waziri wa ulinzi,michezo,afya,kilimo huyo huyo sasa sijui kuwa wanajua kila kitu ??
Members wa mbuyu, msufi, na freemasons ni wachache
 
Hawaniwezi mende hao, ni mshikaji wangu ila hamna kitu hapo ulimi mzito sana na content hamna
LiTANESCO limenshinda licha ya kupewa matrillions ,Kwa kumfichia aibu ndio wakampeleka huko kusiko hitaji vitendo.

Huyo ni ktk Ile list ya mawaziri MIZIGO NA MAGOGO KWA TAIFA.
 
Back
Top Bottom