Uteuzi na Utenguzi: Dkt. Kihamia ateuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa DART, Kuji awa Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA

DART inatakiwa awekwe mtu mwenye mtizamo wa kibiashara.

Hilo Shirika ni la kubinafsisha na kiufupi hata boss wake alitakiwa iwe nafasi wa wazi ya ushindani Ili watu waombe.

Hii ya kuteua Watumishi wa Umma haiwezi kuleta Tija.Just imagine Rais anateua Hadi CEO wa DART,Kuna shida mahala.

Nitashangaa Msajili wa Hazina au Mamlaka ya Uwekezaji ya Mchechu kama hajashauri kubadili muundo wa uendeshaji wa DART.
Shida ni TISS, ni ujinga ku-recycle watu wale wale kwa nafasi ambazo zinademand utaalam wa mambo ya logistics, maamuzi ya aina hii ni dharau kwa wananchi, Kihamia ni mstaafu kwa hiyo kustaafu ni kwa walimu na fani zingine tu TISS wao hawastaafu..
 
KIZIMKAZI hapo ndio anapenda mnoo kuteua na kutengua Yuko tayri kuifanyia mwaka mzima. Sukari imepanda anajifanya hajui llte kilo 4000. Na inaenda juu zaidi hapo ni January
 
Kihamia anaweza kweli hata kusimamia biashara ya daladala moja??
Sidhani kama anajua lolote kuhusiana na biashara ya usafiri au logistics.
Inavyoonekana kwa sasa kuteuliwa ni kupewa fursa kujikimu na si kutumikia watu na kuleta tija..miaka zaidi ya sitini ya uhuru serikali ina watu kwenye vetting system wanawaza kuendesha nchi kama kusimamia genge la kuuza nyanya..hakuna future hapo!
 
Mhhh MHEDE ana shida gani?mbona kila sehemu anashindwa kuperform?alikua TRA katolewa, now DART katolewa kabakisha tu uwenyekiti wa bodi ya NMB!ila Samia alitakiwa kumteua mtu mwenye vision ya biashara sio hawa kina Kihamia (wanasiasa hawa hawana jambo jipya)achomoe mtu huko ktk mabank/kampuni za simu etc!
Achomoe..huo ndio ujinga umedumaza mashirika ya umma! tangaza nafasi watu waombe hiyo kazi!
 
Kweli usiku wa manane kuna mambo mengi.


View: https://m.youtube.com/watch?v=GsXmB6Q0M84
Musa N.K Juma kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)


View attachment 2867935
View attachment 2867937

Hivi Shirika la TANAPA liliundwa kuongozwa na Wazee!!!
Kweli usiku wa manane kuna mambo mengi.


View: https://m.youtube.com/watch?v=GsXmB6Q0M84
Musa N.K Juma kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)


View attachment 2867935
View attachment 2867937
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na utenguzi wa viongozi kama ifuatavyo:

1. Amemteua Dkt. Athuman Kihamia kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART). Dkt. Kihamia aliwahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha.

Dkt. Kihamia anachukua nafasi ya Dkt. Edwin P. Mhede ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.

2. Amemteua Bw. Musa N. Kuji kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Bw. Kuji alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

View attachment 2867897
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
Tengua teua kama huyo Dr kihamia sio mtaalam wa mambo ya usafiri na uchukuzi haitasaidia. Labda kama ni mchumi ataweza kuelewa haraka jinsi ya kuendesha usafiri wa mjini. Dart inahitaji mtendaji mwenye taaluma ya usafiri sio kuchagua tu kishikaji. Pia bodi na mwenyekiti lazima wawe wajuzi na wabobezi wa usafiri na biashara. Pia huko wizarani wawepo watu vichwa sio wajinga wa mambo wasiyoweza kuelewa au kujali tumbo zao tu.
 
Ni mwendo wa kuwapa ulaji watu wa TISS hata wakivurunda.

Mhede=Kihamia=TISS

Kama Taifa tuna safari ndefu sana
 
Inakuwaje rais anateua mtendaji mkuu wa DART, kampuni ambayo ina operate ndani ya jiji ambayo kimsingi inatakiwa kuwa chini ya mandate ya Mayor wa jiji!?

Kwa kweli ukiangalia kwa jicho la tatu hizi teuzi zimekaa kisiasa zaidi na kupeana ulaji tu na siyo kulenga utendaji.
 
Mi najua ni mbinu za kivita za kuelekea Uchagizi, tangu watu waanze kulalamika ni kitambo mbona walikaa kimya.... Wanafanya saivi ivyo ili tujue eti wanatujali wakati hamna......Afya zetu zipo hatarini kutokana na uo usafiri.... Wamekaa kimya muda wote.
 
Anastahili kutolewa hata kwenye hiyo Taasisi aliyobakia kama mwenyekiti, Uchafu wake ni Mkubwa kwa Ushirika na baadhi ya Viongozi hiyo. Chunguzeni Fedha Zitokazo siku za karibuni na mengine.
 
Back
Top Bottom