Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu katika PDF

Next level,
Kama hauna jambo la kuandika ni bora ukae kimya.Mie ninataka sababu tano na siyo mambo ya blah blaha tu.Kata ishu mkulu na siyo kuleta viroja na kama zipo sababu mia kama unavyosema ziweke hapa.

Tabia ya kumshabikia na kumuona Mwanakijiji kama Mungu wako itakuja kukuponza(mpo wengi akiwamo Ngeleja aliyemuomba Mwanakijiji afukie fukie)

Mkuu Mtanzania, Tupo Mstari mmoja!

Mwanakijiji Sham on You again na kinachoniuma ni kuwa wakati mwingine huwa unaniboa kwa kubwatuka kama mvutaji wa bangi

I have been warnging you kwa tabia yako ya kukurupuka tu kwa kumfurahisha mtu huku vitu vingine hauvijui,siyo kwamba kwa kuwa Dr. Mwakyembe ni Maanasheria wa katiba anajua kila kitu na akisema lazima tuamini hivyo,na kwavyovyote vile siyo anachosemea Mwanakijiji ni sahihi.Hell No!

Jipange sawa sawa,ila utetezi wako umejaa hoja dhaifu

Mkuu Gembe, unaonekana kukerwa sana na wanaopinga kununuliwa kwa mitambo ya DOWANS. Mimi nakuomba uelimishe jamvi hili kwa kueleza sababu za msingi unazoona zinatosha kusababisha mitambo hiyo kununuliwa na serikali hasa baada ya yote yaliyosemwa kuhusiana na mitambo hiyo.

Tafadhali toa elimu hiyo, ni mimi nitaiheshimu.
 
"Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu katika PDF."

Well, tulishasoma hoja zako. Tofauti ya kuzianzishia thread mpya ni nini, kwamba ziko kwenye PDF?

Kama unamaanisha umezikusanya pamoja, ungesema tu, Utetezi wa Mwakyembe: Hoja zangu.

PDF haiongezi uzito!

Kauli jamani, kauli.
 
kamba....
 
Mzee Mwanakijiji

Licha ya kushindwa kufungua PDF yako, lakini naungana nawe kusema kuwa Dr. Mwakyembe is innocent kwa kuto declare interest kwa sababu zifuatazo:

Kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi ya 2004, pamoja na Kanuni za msingi za utoaji wa Haki, Declaration of interest inatakiwa kutolewa katika mazingira yafuatayo:
1. Ni lazima Declarant awe na uhusiano na Mzabuni au Wahusika.
2. Ni lazima Declarant awe ni miongoni mwa walioomba hiyo zabuni.

Lakini katika suala la Mwakyembe, Kampuni yake haikuwa na Uhusiano wowote na Richmond au Waliobainika kuhusika na Sakata la Richmond.

Pia Mwakyembe hakuwa miongoni mwa walioomba hiyo Zabuni na wala hakuwa miongoni mwa Waliotuhumiwa kwa namna moja au nyingine katika sakata hilo.

Kwa hiyo, leo hii kushikia Bango kwamba Mwakyembe hakudeclare interest wakati wa kuchunguza tuhuma za Richmond ni kukosea na hii inathibitisha aina ya Media tulionayo Tanzani ambapo waandishi wetu hukurupuka kuandika bila ya kufanya Reference na ndio maana zaidi ya nakala ya MEMARTS ya Kampuni ya Mwakyembe hawakunesha any other Coroborating evidence ya madai yao.
 
Hapa Uk kuna mtu anitwa LORD SAINSBURY, Kuna kipindi alikuwa kamati ya viwanda na bishara na yeye ni mwana hisa mkubwa wa sainsbury supermarket.

Je mwakyembe kujihusisha na biashara ya nishati kumeisaidia bunge kuwa na mtaalamu wa biashara hiyo?
Je mwakyembe kujisisha na nishati kumesaida hata kujulikana hiyo mitambo inauzwa kwa kiasi gani?
Huwezi ukawa na tume nzima hamna hata mtu mmoja mwenye ujuzi wa hiyo biashara. Fikirieni advantage za mfanyabishara wa nishati kuwa kwenye tume ya nishati.

Je Masha kuwa waziri wa Mambo ya Ndani na kuwa mwanahisa wa IMMA ADVOCATES ni wrong?

Kwa maoni yangu, Masha kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na mmiliki wa IMMA Advocates ina muingiliano wa kimaslahi (Conflict of Interest). Ina muingiliano kwasababu DPP yuko chini ya Wizara yake na anayo mamlaka ya kubadilisha mwenendo wa kesi za jinai ambazo serikali ndio mshitaki. Endapo mtu yeyote akishitakiwa na serikali, na mshitaki akitumia kampuni yake kwa ajili ya huduma ya uwakili, ni rahisi kwa Masha kusababisha Mshitakiwa kutotendewa haki kikamilifu kwa kum-influence DPP kufanya maamuzi dhidi ya mshitakiwa. Maamuzi hayo si lazima yasababishe mshitakiwa kuhukumiwa na mahakama, bali yanaweza kumsababishia mshitakiwa kupata usumbufu ambao hangestahili kuupata endapo Waziri asingekuwa na maslahi katika kesi hiyo.
 
Recta hoja yako ni sahihi lakini kwa upande tofauti. DPP iko kwenye ofisi ya Mwanasheria Mkuu. Lakini Magereza na Polisi iko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati kina Mramba wamepelekwa lupango siku ya pili Waziri Masha aliweza kwenda kule gerezani kama mtu binafsi (Wakili wa IMMMA) kuwaona.

Aliweza kuingia pale kwa urahisi kwa sababu pia ni Waziri wa hiyo Magereza na kuchagua mfungwa gani anaweza kuonana naye. Anapoingia hapo anaweza kusema kuona kama wafungwa wako katika mazingira gani. Vi nzi vyetu vilivyokuwepo maoneo yale kama nilivyoripoti wakati ule vilidokeza kilichompeleka ni kutaka kuona kina Mramba kama wangetumia kampuni ya IMMMA kama watetezi wao katika kesi yao. Of course Mramba na Yona wakamtolea nje.

Pale ulikuwa ni mgongano wa maslahi ya wazi kwa sababu kuna maswali ya faida ya kifedha ambayo Masha kama partner wa IMMMA anaweza kuipata endapo kina Mramba wangeamua kuitumia IMMMA kama wakili. HIyo inaitwa conflict of interests.

Je ulisikia kuna Mbunge kasema ajiuzulu kwa sababu hiyo? Si wengine hapa tuliitwa tuna chuki na Masha?
 
Tangu nilipoanza utetezi wangu wa Dr. Harrison Mwakyembe, nimetoa majibu kwa watu wengi na kutoa hoja nyingine katika kurasa mbalimbali. Vile vile kuna mambo mengine ambayo ningeweza kuyaonesha lakini kwa kuendelea kujibizana na mtu mmoja mmoja, inanichukua muda mrefu kujenga hoja. Hivyo nimeamua kujipa jukumu hili la kutoa utetezi wangu wa wazi na usio na utata wa Dr. Harrison Mwakyembe: M. M.

utetezi.jpg

UTANGULIZI
Ndani ya siku hizi chache tumeshuhudia hoja ambazo zina hisia nyingi na ambazo naamini kwa kiasi kikubwa ni sehemu ya yale yale mapambano ya kifikra. Hoja hizi zimejengwa hasa dhidi ya Dr. Harrison Mwakyembe Mbunge wa Kyela na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mkataba wa Richmond ambayo ripoti yake Bungeni ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu kujiuzulu kufuatia kashfa ya kampuni feki ya Richmond.

Kuanzia matukio yale ya kihistoria ya mwaka jana hadi leo hii kumekuwepo na majaribio ya kila aina ya kumdhalilisha na kumbomoa Dr. Mwakyembe na ninaamini hili la sasa hivi limedhaniwa kuwa ndilo linaloweza kufanikiwa. Kuanzia suala la kukatiwa maji na DAWASCO mwezi wa nne mwaka jana. Wakati ule kama ilivyo sasa walioathirika na ripoti ya Mwakyembe Bungeni walionesha kufurahia kuwa hatimaye kumbe na Dr. Mwakyembe naye ni fisadi.

Katika jaribio jingine la sasa kuna imani ya kwamba hatimaye safari hii wamempata. Hata hivyo hilo ni kundi moja tu.

Kuna kundi la pili la wale ambao wanaamini katika maadili ya uongozi ambao wanaamini kuwa kwa jinsi walivyosoma na kutambua kuwa Dr. Mwakyembe naye ni mmiliki wa kampuni ya kufua umeme basi alitakiwa kutangaza maslahi hayo katika Kamati Teule (wakati wa kuzungumza Bungeni mwaka jana) na pia katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo yeye ni mjumbe. Hawa wanaamini Dr. Mwakyembe amevunja maadili na amekiuka miiko fulani.

Hawa naweza kusema wanaongozwa na kanuni.

Ni makusudio yangu kumtetea Dr. Mwakyembe dhidi ya makundi yote mawili na kuonesha kuwa hoja zao ni za kuvutia masikio lakini hazina msingi, ni dhaifu na tukiziangalia kwa karibu tutaona zina makosa mengi. Kwamba, makundi yote mawili yamekosea kwa hoja zao na kwa ushahidi wanaotoa. Tafadhali fuatana nami katika utetezi huu wa wazi wa Dr. Harrison Mwakyembe.

Unapofuatana nami hakikisha unaangalia sana matumizi ya maneno yangu kwani najitahidi kuchagua maneno vizuri kutaka kumaanisha kile ninachokisema na kusema ninachomaanisha. Ukikosea stepu usisite kurudi nyuma kunipata vizuri.

Kwa wale wageni na makala zangu za utetezi hii siyo makala ya kwanza au hoja ya kwanza ya utetezi. Huko nyuma nilisimama kumtetea marehemu Amina Chifupa baada ya “kunyamazishwa”, nimemtetea Waziri Sofia Simba, na nimewatetea mabinti wa Nyegezi kina Nsia Swai. Na huu utetezi hautakuwa wa mwisho kwa mtu yeyote ambaye dhamira yangu inanituma kuamini kuwa aidha anaonewa au kutokana na nguvu zaidi anawekwa mahali ambapo hawezi kushinda.

karibu....

Na pia Mengi nna zile picha za zisizo na maadili.
 
Hongera Mkuu Mwanakijiji kwa kazi uliyojipa. Hata hivyo kwa sisi tusiosomea kuzungusha maneno huwa na masuwala machache ambayo huyaona kuwa ndio kipimo cha matamshi au matendo ya mtu.
Waswahili husema anaechukua jembe na kwenda shambani anakusudia kupata mazao idadi na ubora wa mazao utategemea mazingira chungu nzima. Utetezi wako kwa DR mwakyembe naona ulibase na Fedha. Eti maslaha yanayozungumziwa ni fedha, eti wao walikuwa hawana fedha za kuleta ushindani, eti Richmond/Dowans mitambo ikitaifishwa wao ndio watakaopata hasara ya fedha. Kama nilivyosema mwanzo kuzungusha maneno hatujasomea lakini si mabwege hivyo kama mnavyodhani. Hivyo harakati zote hizo na hisa zinazomilikiwa nini lengo lake? Hivyo ndani ya Bunge kuna wakati ukaongelewa fedha physical?
Halafu hawa kina Mwakyembe ni taahira? kukaa na kuunda kitu ambacho hawana uwezo nacho? Mbona tungekuwa na makampuni sote kama nadharia ndio mtaji, nadharia ndio uzalishaji na nadharia ndio chumo la mradi. Kwa ubole wangu nahisi vitu hivyo vitatu vyote ni Fedha.
Katika utetetezi wako kwa hiyari yako unarudi na kukubali kuwa pengekuwa na mgongano kama kuondoka kwa Dowans kampuni ya mwakyembe itauza huo umeme ambao haujaanza kuzalishwa. Kwanini hii assumption? wakati unataka tuamini kuwa hakukuwa na suala la fedha? Jibu la rahisi ni kuwa huo mradi ulilenga katika Fedha.
Sawa una haki ya kumtetea shujaa wako lakini huna haki ya kuyanyamazia makosa aliyoyatenda ambayo yako nje na hili ambalo dhana yako inaona hana kosa. Hili la kuleta UKABILA nalo tuliachie hasa likiwa linatoka kinywani mwa kiongozi shujaa?. Ona madhara yake yanaanzia milangoni mwetu. Tumekuwa tukipigia kelele Ukabila humu kwenye JF lakini Bingwa wetu unalifumbia macho na tumeshaona baadhi yetu tukilish.erehesha.
Mkuu Ufisadi si rangi wala dini lakini kama tutaendelea tutaanza kuwahesabu mafisadi kwa dini zao
 
Mafisadi wajanja sana wanatafuta njia zote ili kuonyesha kuwa RICHIMOND/DOWANS ni safi!!

RICHMOND na hata DOWANS sio safi. Ni mmoja ya mfano wa MAHIRI wa tatizo la ufisadi nchini mwetu. Hata hivyo suala hapa lilikuwa ni umuhimu wa TANESCO kununua mitambo inayomilikiwa na RICHMOND na Baadaye DOWANS ambayo kuna inayosemekana ni michakavu, mikuukuu na iliyotumika kiasi. Baadae likageuka/likageuzwa kuwa suala la Zitto Vs Mwakymbe, baadaye likaja kuwa suala la Mwakymbe Vs Zitto, na sasa limeongezeka kuwa suala la VIONGOZI na MAADILI YA UONGOZI.

Tunaweza kuwa na maoni na madukuduku yetu mengi na yaliyo halali ama kwa uchungu wa kweli na nchi yetu, ushabiki wa makundi ama watu tunaowaunga mkono ama tunaowapinga na pia kuwa na imani zetu na suala zima la maadili ya kisiasa na kibinafsi.

Tukiweza kung'amua kati ya haya yote kipi ni MUHIMU zaidi kwa Tanzania yetu na kuthubutu kutilia mkazo hilo ndipo tutakuwa tunatendea haki BARAZA hili na Watanzania ambao wengi wetu tunaamini tunawaongelea hapa.

omarilyas
 
Kwa hiyo waandishi wa habari wameamua kuwa mabaamedi wa mafisadi? Nionavyo mimi ni kwamba kama ilivyo kwa baadhi ya dada zetu wanavyokubali kudhalilishwa na walevi ili wapate mlo, ndivyo baadhi ya waandishi wa habari walivyoamua kudhailisha taaluma zao ili mafisadi wajaze matumbo yao!
Wasiwasi wangu ni juu ya hao nafisadi kuwa na uraia wa nchi zaidi ya mbili. wana pa kukimbilia wakati nchi itakapoporomoka kiuchumi na kisia! Je wataondoka na hao waandishi wa habari mabaamed?

Kilemi,
Yaani hii nchi sijui tukoje. Ofcourse siungi mkono ubaguzi wa rangi lakini kusema ukweli wahindi hawana uzalendo wa kuiendeleza nchi yetu hata kama mababu wa mababu zao wamezaliwa na kufia TZ kama anavyojitetea Rostam. Watu hawa wako tayari kuagiza mawese kutoka Malaysia na Indonesia kwa wahindi wenzao wakiacha mawese ya Kigoma na Kyela yakikosa soko kwa kisingizio kuwa supply ni ndogo sana. Na watu hawa ni vinara wa madili machafu ikiwemo kuwa na uraia wa nchi kadhaa. Wako radhi kuhakikisha kuwa biashara za wazawa zinakufa wao wakishamiri huku wakikwepa hata kulipa kodi. Enyi waandishi mlionunuliwa na fisadi Rostam badilisheni nia zenu kwa maslahi ya nchi yenu.
 
Hongera Mkuu Mwanakijiji kwa kazi uliyojipa. Hata hivyo kwa sisi tusiosomea kuzungusha maneno huwa na masuwala machache ambayo huyaona kuwa ndio kipimo cha matamshi au matendo ya mtu.
Waswahili husema anaechukua jembe na kwenda shambani anakusudia kupata mazao idadi na ubora wa mazao utategemea mazingira chungu nzima. Utetezi wako kwa DR mwakyembe naona ulibase na Fedha. Eti maslaha yanayozungumziwa ni fedha, eti wao walikuwa hawana fedha za kuleta ushindani, eti Richmond/Dowans mitambo ikitaifishwa wao ndio watakaopata hasara ya fedha. Kama nilivyosema mwanzo kuzungusha maneno hatujasomea lakini si mabwege hivyo kama mnavyodhani. Hivyo harakati zote hizo na hisa zinazomilikiwa nini lengo lake? Hivyo ndani ya Bunge kuna wakati ukaongelewa fedha physical?
Halafu hawa kina Mwakyembe ni taahira? kukaa na kuunda kitu ambacho hawana uwezo nacho? Mbona tungekuwa na makampuni sote kama nadharia ndio mtaji, nadharia ndio uzalishaji na nadharia ndio chumo la mradi. Kwa ubole wangu nahisi vitu hivyo vitatu vyote ni Fedha.
Katika utetetezi wako kwa hiyari yako unarudi na kukubali kuwa pengekuwa na mgongano kama kuondoka kwa Dowans kampuni ya mwakyembe itauza huo umeme ambao haujaanza kuzalishwa. Kwanini hii assumption? wakati unataka tuamini kuwa hakukuwa na suala la fedha? Jibu la rahisi ni kuwa huo mradi ulilenga katika Fedha.
Sawa una haki ya kumtetea shujaa wako lakini huna haki ya kuyanyamazia makosa aliyoyatenda ambayo yako nje na hili ambalo dhana yako inaona hana kosa. Hili la kuleta UKABILA nalo tuliachie hasa likiwa linatoka kinywani mwa kiongozi shujaa?. Ona madhara yake yanaanzia milangoni mwetu. Tumekuwa tukipigia kelele Ukabila humu kwenye JF lakini Bingwa wetu unalifumbia macho na tumeshaona baadhi yetu tukilish.erehesha.
Mkuu Ufisadi si rangi wala dini lakini kama tutaendelea tutaanza kuwahesabu mafisadi kwa dini zao

umejitahidi... kudos na nimekusikia.
 
Mimi bado nipo na Dr Mwakyembe kwa sbabu sijaona mtu hata mmoja akitoa hoja ya maana inayoweza nishawishi niuone mgongano wa kimaslahi.

Eti tu kwa vile mmefanya tendo la ndoa basi mkiambiwa wenye watoto hawaruhusiwi kujadili hoja iliyopo mbele yenu, basi ninyi mliofanya kitendo mnahesabiwa kwamba tayari mna watoto.
Ngono inaweza kuzaa mimba na hatimaye mtoto. Je ngono ni sawa na mtoto??

Kwa mtaji huu,Tutaendelea kuuziwa mbuzi kwenye magunia hadi Yesu arudi mara ya pili.

Naona Fedha za EPA zimetulewesha Watanzania, kwa hiyo inatubidi tuwaenzi mashujaa wetu walio jitoa muhanga kuliibia taifa.

Tanzania hatuli mpaka mtu aibe.
 
Madilu na mifano yako hii.. mmh.. nimecheka.. to end my tense day. Thanks!
 
Madilu na mifano yako hii.. mmh.. nimecheka.. to end my tense day. Thanks!

Kumbe na wewe umei-notice mifano yake eeh? Yaani huyu jamaa huwaga ananiacha hoi sana. Halafu hako ka picha kake ka utotoni kanaonyesha ni jinsi gani alivyo mtu wa kufikiria....we cheki tu hiyo picha...yaani hako ka bwa mdogo kamekaa kaa kanafikiria jambo zito kweli kweli....Lol
 
Tuache ushabiki ndio maana hatufiki mahali popote tunaishia kubadilisha mvinyo toka chupa nyingine hadi nyingine kutegemeana na nani anaongea na ametokea kundi gani.

1. Did Dr do a brilliant job with his committee - YES , sana and brave
2. Did the PM resignation happen rightly or wrongly - It was right lazima he had to do that and that means we are going into a zero tolerance
3. Did Dr Mwakyembe mess kwa kutoeleza awali kabisa hizi interests zake - BIG time. Kama alieleza and all is on the record, ni sawa yeye hana kosa ila na hapa inaonyesha kuwa maswala ya maadili Bungeni yako MABOVU SANA and need URGENT action kurekebishwa and YES WABUNGE WOOOTE and viongozi woote lazima watoe ya kweli na kama wamekiuka, wapewe muda kutokana na dhana mpya za Uongozi. Kama Yesu aliposema huwezi tumikia Mabwana wawili na kama una mali mpe maskini ndo uje kwangu - all our leaders needs to be put in the same test with zero tolerance kama Watumishi wa UMMA wa Tanzania. I mean zero tolerance!! Period. Tunatafuta sababu za kuwaelewa au kutetea na ndio tunajenga misingi mobovu yenye mianya ya ajabu ajabu kila kukichwa.

4. Rostam Aziz, je ana maswali ya kujibu ? - Jibu, YES BIG time toka scandali zote zimeanza , inakuwaje ana muda wa kusambaratisha watu na nchi nzima to this level wakati sie tupo hapa tumelala usingizi!
5. Je Rostam na kambi yake wamefanikiwa kupoteza moto wa Ufisadi ? Kwangu mie ndio wanacheza mazingaombwe ila wanakulana wao kwa wao na inaonyesha jinsi mfumo mzima ulivyo mbovu, hivyo ni sawa kwani dhambi zao zinawakula. Linalotakiwa ni wewe na mimi kuwa makini kutongia kwenye zogo lao na kutokutetea uhalifu na ukosefu wa maadili kwa vile tu, eti tunampenda Dr Mwakyembe. That is and will be wrong. Two wrongs don't make a right. Mwakyembe amekosea na tusione haya kumwambia hivyo ingawa tumependezwa na ujasiri wake na bado tunatakiwa kumsupport kama bado yu nasi na ana moyo, ila hili tuseme wazi amekosea, period!

6. Dr tukiamua kama public opinion kumsamehe inabidi na yeye awe mstari wa mbele, moja aonyeshe amekomaa kisiasa - aangalie kisheria amesimama wapi, aweke sawa kisiasa na public opinon kama alivyoweka wazi juu ya record zake za BRELA kwa waandishi wa habari, ila alete siasa mpya Tanzania aseme wazi wapi amekosea kwani lazima anajua wapi amekosea; Asilete ubabe na kugawa watu kwa maneno kama eti yeye hana nchi nyingine kwani yeye Kazaliwa Tanzania na vitu kama hivyo! Tanzania ni ya Watanzania wote sio wa kuzaliwa au kuandikishwa. Tukae kwenye maadili sio tuanze kugawana kwa mafungu kwa statements kama za Uzawa.

7. Dr Mwakembe asifanye any retirement azidishie kazi kama energy bado ipo, ila kama amechoka apumzike waje wengine wenye ari ile ile kwani kazi badi saaana

La maana, tuache kuanza kusambaratika na kusahau what is the fight for. To me ni Usawa, Uongozi Bora, wa sheria na Maadili safi kama ya Azimio la Arusha Juu ya Uongozi na kuondoa ubabaishaji kwa kuwa 0 tolerant na mazingaombwe, ndio tutaweza jenga nchi na mali ndogo tulionayo tena bila kutegemea misaada kila kukicha. Angalia IPPMedia leo (21/03/2009 - kuna habari hii kwenye picha - Members of a Hadzabe family at Hilamoto Village in Iramba District, Singida Region, seated under a tree as they listen to their legislator, Mgana Msindai. Msindai urged them to store food because there is a likelihood of drought in the area.) Ningependa kujua huyu mbunge anaishi nyumba gani na hapo kijijini hawa wananchi wanakaa wapi na uwakilishi wai ukoje? These are matters that needs to concern us and our leaders sio kuchezewa who is who.
 
Ni ukweli usiopingika kwamba kuna watu wengi weusi kwa weupe waishio nchini Tanzania ambao wanasoma shule zetu bure na kudai ni Watanzania lakini wakati ukifika hao wanarudi kwao kwa mbwembwe nyingi na Kashfa.
Kuna Waarabu, Wanywarwanda, Warundi Wacongo Waganda, Wakenya Wakomoro Wamalawi Wazambia Wahindi na sasa wachina ambao wanadai kwa nguvu zao zote kwamba wao ni WaTanzania damu, lakini wakilikoroga wanaanza kwa sababu Tanzania ni kwao tu kama wanachuma kishambalabibi.
KWa hiyo kama Rostamu Aziz ametajwa kwamba yeye ni Mmesopotamia ni kazi kwake kuprove kwamba yeye ni MTZ au vinginevyo na yeye aseme DR MWakyembe ni Mzambia au Mmalawi.

Vijana wengi tulisoma nao pale Bongo na kufanya nao kazi serikalini ghafla wakaingia mitini kama wepesi wa kivuli, nimekuja hapa Marekani nakutana nao wakiwa na hati za Burundi na Rwanda.
Kibaya zaidi wanasema ovyo kwamba

WaTZ ni masikini sana Tshs 100,000 tu mtu anauza utu wake pale Uhamiaji na TRA na kudai kwamba sisi hatutakaa twende mbele kwa sababu ya ujinga wetu. Kwao Rwanda mgeni huwezi tamba ni lazima ulipe kodi yote na wakati mwingine zaidi ya mwenyeji. Wanadai kwamba Tz mtu akiongea kiswahili cha kubabaisha ni ujiko kweli kweli hasa kama una hela kidunchu za kunywesha watu bia na kuiwalipia gharama za ngono.

Samahani haya si maneno yangu ni maneno ya watu niliosoma nao sasa wanaishi hapa Marekani wakitokea Burundi na Rwanda.

Walikuweko akina Mutungirehe na akina Nyambele pale UDSM wakidai kwamba ni Wahangaza leo nasikia wako Central Bank of Rwanda na hawana kumbukumbu yeyote kwamba waliwahi kuwa Watanzania.
Maneno ya Dr MWakyembe yana ukweli mwingi ndani, nisijojua ni kuhusu huyu owner wa Rai ni kweli ana urai wa nchi mbili au tatu?
 
Hayo yote yapo sana. Mimi nilisoma na Waburundi waliokuja kukata Mkonge (Ukubwani nimkuja kujua walikuwa WaTutsi). Wengine walifika elimu za juu wengine walikuwa jeshini polisi na very succesfull, na hapo baadae nikasikia walienda Rwanda kwenye vita, some came back some sina data nao. Wengine nilisoma nao wa asili ya Kiarabu, Wahindi - wako Marekani na UK, hao Waangaza nilisoma nao, Wamalawi nilisoma nao wengine hata sasa wana madaraka makubwa nchini kwenye baadhi ya Taasisi za Umma. Wote hawa before the eyes of the law of the land, the mother of all laws, ni Watanzania. Kama wana hulka zao chafu, isiwe sabau sisi kijishusha kwenye level yao. Kumbuka ni ukosefu wa nidhamu na ukosefu wa kujua wao ni nani kwa mtu yoyote anapoangalia nani yupo kwenye chumba ndio ajiite Mtanzania au Mganda au Mrwanda. Wewe na mimi tunajijua ni Watanzania hata ukimbizwe usingizini utaitika, naam, mimi ni Mtanzania. Let us be proud of that and tuishikilie. Mwenye kutusi wakati nchio yetu ilimpa kula na kuvaa, achane nae. Ni tatizo lake sio letu. Sisi tujenge au niseme tupiganie kujenga Utawala wa sheria na tuwe makini nao.

Swala la passport mbili, hilo ni kuvunja sheria ya nchi kama ilivyo kwa sasa. Ni marufuku mtu kuwa na passport mbili Tanzania iwe moja wapo. Unatakiwa kurudisha na kukana Utanzania pindi ukichukua nyingine. ndio maana wengi wetu bado hili tunalipinga kwani twajua hawa hawa viongozi ndio wamelikalia and wanavunja sheria . Kuna uwezekano mkubwa kabisa RA awe na passport ya nchi nyingine kutokana na roots za Mababu zake. Lakini hiyo iswe ni radhia ya kufanya Watanzania wote wenye kutaka kutii sheria na kuweka hoja ya dual nationality nao wawe ovyo pia. Hapana.

La msingi swali yes lipo, ana dual passport huyo RA? Na kama ni hivyo, anawezaje kuwa Mbunge?? Kumbuka they did the same with Amir Jamal? Wapo wenzetu wengine wengu tuu wanazo hadi leo hii passport mbili. Kama sio kufundisha watanzania uharamia ni nini tena?? ALafu tanategemea tujenge utawala wa sheria?? Hata siku moja, tutajenga utawala wa uonevu, unafiki, uchoyo, uwongo na ufisadi as we can clearly see what is happening now.

Ukaburu hauna rangi ya ngozi. Ni hulka na tabia.
 
Mwanakijiji na wale wote wanaosema kuwa hakuna mgongano wa interest kwa Mwakyembe kuwa na mipango ya biashara ya umeme huku akichunguza kampuni nyingine yenye biashara hiyo hiyo na akitegemea mteja yule yule mmoja naomba mnifafanulie haya mambo mawili.

(a) Kwa vile conflict of interest inakuja tu pale ambapo kuna maslahi ya kipesa ya moja kwa moja wakati huo ni siyo huko mbeleni, je kulikuwa na lazima ya nini kwa injinia Manyanya kutakiwa kujiuzulu wadhifa wake huko TANESCO ilihali wakati huo hakuwa kwenye payroll ya TANESCO na hivyo hakukuwa na maslahi yoyote ya kipesa kwake.

(b) Kwa vile conflict of interest inakuja tu pale ambapo kuna maslahi ya kipesa ya moja kwa moja wakati huo ni siyo huko mbeleni, je kulikuwa na haja gani kumpigia kelele Mkapa kuhusu Bank M hata kama mipango ya kuanzisha benki ile ilifanywa wakati wa utawala wake lakini benki yenyewe haikuanza mpaka alipokuwa keshatoka madarakani?
 
Tuache ushabiki ndio maana hatufiki mahali popote tunaishia kubadilisha mvinyo toka chupa nyingine hadi nyingine kutegemeana na nani anaongea na ametokea kundi gani.

1. Did Dr do a brilliant job with his committee - YES , sana and brave
2. Did the PM resignation happen rightly or wrongly - It was right lazima he had to do that and that means we are going into a zero tolerance
3. Did Dr Mwakyembe mess kwa kutoeleza awali kabisa hizi interests zake - BIG time. Kama alieleza and all is on the record, ni sawa yeye hana kosa ila na hapa inaonyesha kuwa maswala ya maadili Bungeni yako MABOVU SANA and need URGENT action kurekebishwa and YES WABUNGE WOOOTE and viongozi woote lazima watoe ya kweli na kama wamekiuka, wapewe muda kutokana na dhana mpya za Uongozi. Kama Yesu aliposema huwezi tumikia Mabwana wawili na kama una mali mpe maskini ndo uje kwangu - all our leaders needs to be put in the same test with zero tolerance kama Watumishi wa UMMA wa Tanzania. I mean zero tolerance!! Period. Tunatafuta sababu za kuwaelewa au kutetea na ndio tunajenga misingi mobovu yenye mianya ya ajabu ajabu kila kukichwa.

4. Rostam Aziz, je ana maswali ya kujibu ? - Jibu, YES BIG time toka scandali zote zimeanza , inakuwaje ana muda wa kusambaratisha watu na nchi nzima to this level wakati sie tupo hapa tumelala usingizi!
5. Je Rostam na kambi yake wamefanikiwa kupoteza moto wa Ufisadi ? Kwangu mie ndio wanacheza mazingaombwe ila wanakulana wao kwa wao na inaonyesha jinsi mfumo mzima ulivyo mbovu, hivyo ni sawa kwani dhambi zao zinawakula. Linalotakiwa ni wewe na mimi kuwa makini kutongia kwenye zogo lao na kutokutetea uhalifu na ukosefu wa maadili kwa vile tu, eti tunampenda Dr Mwakyembe. That is and will be wrong. Two wrongs don't make a right. Mwakyembe amekosea na tusione haya kumwambia hivyo ingawa tumependezwa na ujasiri wake na bado tunatakiwa kumsupport kama bado yu nasi na ana moyo, ila hili tuseme wazi amekosea, period!

6. Dr tukiamua kama public opinion kumsamehe inabidi na yeye awe mstari wa mbele, moja aonyeshe amekomaa kisiasa - aangalie kisheria amesimama wapi, aweke sawa kisiasa na public opinon kama alivyoweka wazi juu ya record zake za BRELA kwa waandishi wa habari, ila alete siasa mpya Tanzania aseme wazi wapi amekosea kwani lazima anajua wapi amekosea; Asilete ubabe na kugawa watu kwa maneno kama eti yeye hana nchi nyingine kwani yeye Kazaliwa Tanzania na vitu kama hivyo! Tanzania ni ya Watanzania wote sio wa kuzaliwa au kuandikishwa. Tukae kwenye maadili sio tuanze kugawana kwa mafungu kwa statements kama za Uzawa.

7. Dr Mwakembe asifanye any retirement azidishie kazi kama energy bado ipo, ila kama amechoka apumzike waje wengine wenye ari ile ile kwani kazi badi saaana

La maana, tuache kuanza kusambaratika na kusahau what is the fight for. To me ni Usawa, Uongozi Bora, wa sheria na Maadili safi kama ya Azimio la Arusha Juu ya Uongozi na kuondoa ubabaishaji kwa kuwa 0 tolerant na mazingaombwe, ndio tutaweza jenga nchi na mali ndogo tulionayo tena bila kutegemea misaada kila kukicha. Angalia IPPMedia leo (21/03/2009 - kuna habari hii kwenye picha - Members of a Hadzabe family at Hilamoto Village in Iramba District, Singida Region, seated under a tree as they listen to their legislator, Mgana Msindai. Msindai urged them to store food because there is a likelihood of drought in the area.) Ningependa kujua huyu mbunge anaishi nyumba gani na hapo kijijini hawa wananchi wanakaa wapi na uwakilishi wai ukoje? These are matters that needs to concern us and our leaders sio kuchezewa who is who.

I like it how briliantly you put item #3 and #6; these are the angles that some us find difficult to swallow, especially due to items #1, 2, 4 and 5
 
Mwanakijiji na wale wote wanaosema kuwa hakuna mgongano wa interest kwa Mwakyembe kuwa na mipango ya biashara ya umeme huku akichunguza kampuni nyingine yenye biashara hiyo hiyo na akitegemea mteja yule yule mmoja naomba mnifafanulie haya mambo mawili.

Kichuguu, sijasema hakuna mgongano wa maslahi, nimesema kwa sheria yetu ilivyo hakuwa na mgongano wa maslahi uliomlazimu kutangaza maslahi hayo. Nje ya sheria yetu nikiangalia kutoka kwa mwanga wa corporate America and American Politics of which I'm more familiar with naweza kuorodhesha mambo mengi ambayo yana mgongano wa maslahi, siyo yeye tu bali Bunge zima.

(a) Kwa vile conflict of interest inakuja tu pale ambapo kuna maslahi ya kipesa ya moja kwa moja wakati huo ni siyo huko mbeleni, je kulikuwa na lazima ya nini kwa injinia Manyanya kutakiwa kujiuzulu wadhifa wake huko TANESCO ilihali wakati huo hakuwa kwenye payroll ya TANESCO na hivyo hakukuwa na maslahi yoyote ya kipesa kwake.

Hapana; sijasema mgongano wa maslahi unakuja TU PALE.. Mgongano wa maslahi unaweza kuwa na mambo mengi kweli kama unavyoashiria. Kwa bahati mbaya kwa kanuni ya Bungei mgongano unaotakiwa kutangazwa ni ULE..

(b) Kwa vile conflict of interest inakuja tu pale ambapo kuna maslahi ya kipesa ya moja kwa moja wakati huo ni siyo huko mbeleni, je kulikuwa na haja gani kumpigia kelele Mkapa kuhusu Bank M hata kama mipango ya kuanzisha benki ile ilifanywa wakati wa utawala wake lakini benki yenyewe haikuanza mpaka alipokuwa keshatoka madarakani?

Jibu langu la hapo juu linahusika.
 
Back
Top Bottom