Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,943
Tatizo ambalo tumelikwaa katika mijadala ya kisiasa Tanzania ni kuamini kwamba tunayemtetea tunafikiri anachafuliwa au anabolewa anapokosolewa. Tunakosea sana tunapofikiri kuwa wale tuliowapachika 'ushujaa' sio watu wanaoweza kukosea, na wakikosea basi wamenunuliwa! Na hao mashujaa wetu nao, kwa kuzoea kumwagiwa sifa, wakafikiri kila watakachokisema au kukifanya watashangiliwa, walipokosolewa wakadhani wanapigwa vita, na watu wanaowapiga vita wanatumiwa na mafisadi!
Namna ya kujitoa kwenye utumwa huu ni kuangalia hoja badala ya mtu. Ikiwa wewe upo kumtetea mtu badala ya hoja lazima utakula kwako kwa sababu huyo mtu wako ipo siku atachemka, na kwa kuwa wewe ulishaamua kuchukua upande, utaendelea kumtetea na ndipo hapo utakapoonekana kituko. Sasa katika sakata hili tulikwisha kuchemsha tangu awali kwa kufikiri kwamba chochote asemacho Mwakyembe na 'mashujaa' wenzake ni kwa maslahi ya taifa na chochote asemacho mtu kama Rostam, kwa mfano, ni kwa maslahi ya mafisadi! Kwa mtizamo huu tumekuwa tukijaribu kuhalalisha kila kitu wasemacho akina mwakyembe na kukifedhehesha chochote wasemacho watu kama akina Rostam. Japokuwa hii inatusaidia kupata furaha kisaikolojia, haitusaidii kupata ukweli wa mambo.
Tuache basi kushabikia majina ya watu, tujikite kwenye kile wanachosema. Tukifika hapa utagundua kwamba kuna siku hata Rostam na Mtikila husema kitu chenye akili, na kuna siku hata Zitto, Mwakyembe, Kilango na 'mashujaa' wetu wengine huchemsha vibaya sana, kama ilivyotokea katika hili sakata la Dowans!