Utenzi wa Tanzania - Miaka Hamsini ya Uhuru (Beti 100)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Utangulizi


Nilipata wazo la kuandika utenzi huu* kuanzia mwaka jana. Nilikuwa nimekusudia kuandika Utenzi wenye beti 1000 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Lakini katika uvivu wangu na mihangaiko ya dunia nimejikuta nimeishia kwenye hizi beti 100 za utenzi huu wa Tanzania. Maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru ni maadhimisho siyo ya mipaka ya nchi, siyo ya jina na kwa hakika kabisa siyo maadhimisho ya kupita kwa muda. Ni maadhimisho – naamini- ya utu wetu.

Kwamba, katika miaka hamsini iliyopita tumeweza kufanya kile ambacho hakikuwahi kufanywa kwa miaka 2000 iliyopita katika eneo letu. Yaani, kuwaunganisha watu watu wetu wote, chini ya mipaka ile ile, wakiwa huru na haki sawa. Katika utenzi huu nimeelezea jinsi eneo letu lilivyojulikana kama Azania katika masimulizi ya Wagiriki au kama Zenji kwa Waarabu na wakati mwingine kuhusiana na majina ya maeneo ya Kushi na Nubia katika Biblia. Kama jamii ya watu tumepitia mambo karibu yote ambayo yamepitiwa na jamii nyingine za dunia. Kuanzia maisha ya ujima, utumwa, vita, mapigano, na hatimaye uhuru.

Kumbe basi historia yetu haina tofauti sana na historia ya jamii nyingine za watu ambazo zimesimama katika pande za dunia. Unaposoma utenzi huu ni matumaini yangu utakufanya ujisikie fahari kuwa wewe kama vile mimi ni zao la historia hii. Tumefungamanishwa na historia kiasi kwamba haiwezi kufunguka. Mbele yetu wametutangulia wengi katika historia ambao nao walisimama kutambua utu wao na kuudai mbele ya watawala wa zama zao. Ni hiki ndicho tunachokifurahia kwamba leo tuko huru kuwa watu sawa na wengine – kwa kila hali.

Ni utu wetu ndio ulikuwa msingi wa kupigania uhuru wetu na unatakiwa kuwa ndio kiini cha kushangilia uhuru huo. Ni vipi tumetumia uhuru huo kuinua utu wetu hili ni swali jingine ambalo kizazi chetu kama kizazi kinachokuja kitahiji kujibu. Je, mambo tunayoyafanya na kufanyiana yanalingana na utu huo? Je, tunatendeana kama watu wenye utu katika sera, sharia, mipango, na mambo tunayoyafanya? Utenzi huu basi ni kukumbushia utu wetu.

MMM Disemba 5, 2011


SIFA KWA MUNGU!
1. Ee Mola ninakujia
Kwako ninasujudia
Sifa nakurudishia
Utukufu enzi pia



2. Ewe uliye Jalia
Mmiliki wa Dunia
Hukumu ni zako pia
Na adhabu ya Jehania



UTANGULIZI



3. Kalamu naishikia​
Naandika beti mia​
Kwa tungo nazipangia​
Zinasifu Tanzania


4. Ni tungo za historia​
Ni wapi tulianzia,​
Na wapi tumefikia,​
Lengo ni kukumbushia


5. Nataka kusimulia​
Kwa hizi tungo mia​
Huku nawahisabia​
Mpaka zitapotimia


6. Tangu walipoingia​
Wageni toka Asia​
Na wale wa Yuropia​
Makabila yalohamia


7. Ishirini na mia,​
Makabila ya Tanzania,​
Makubwa madogo pia​
Hapa nawasimulia


8. Na beti zikitimia​
Zikifika hizo mia​
Kalamu nitaachia​
Lengo nitalifikia.


9. Ujumbe nauanzia​
Wa hizi beti mia​
Kwa kina nitagusia​
Ni wapi tulianzia

...

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Disemba 5, 2011
Email: mwanakijiji@jamiiforums.com
Facebook: "mimi mwanakijiji"

Ω​
NB:* - Utenzi huu unaweza kuchapwa popote na mahali popote bila kubadilisha maneno kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Haki zote za kuunakili zimeruhusiwa bila kubadilisha jina la mtunzi au utenzi wenyewe; lazima kuweka maelezo ya mawasiliano kama yalivyo.
 

Attachments

  • utenziwatanzania.pdf
    498.1 KB · Views: 509
telek.gif
ngoja niendele kuisoma kwa umakini kabla sijaijibu
 
Awali ya yote

Thalatha inamaanisha tatu na sio thelathini
Aroba (arba) inaamisha nne na sio arobaini (arbaini)
kama ambavyo tisa inamaanisha tisa na sio tisiini

Pili, ningeomba kuelezewa huu 'utenzi', unafuata kanuni gani za uandishi wake?
 
Tanzania haijawahi kutawaliwa na haina siku ya uhuru bali ni siku ya Muungano tu, atakaepotosha ukweli huu amelaaniwa duniani mpaka mbinguni.
Nawapenda sana Tanganyika Law Society walijiondoa kwenye unafki huu tangu awali.
 
Utangulizi


Nilipata wazo la kuandika utenzi huu* kuanzia mwaka jana. Nilikuwa nimekusudia kuandika Utenzi wenye beti 1000 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.................

Nimeishia hapa. Siwezi kuendelea kusoma beti 100 za uhuru wa tanzania. Nitaweza kusoma au hata kuimba beti 10,000 za Tanganyika baada ya uhuru wa kweli tutakapoachana na Zanzibar. Anza kutunga.......
 
Beti nimemalizia
yote nimejionea
asante kwa historia
na mengi kujifunzia

hongera kwa kuyaona
makosa yalotendeka
nchi mbili kuungana
na mbili kupatikana

Tanganyika kupotea
ndilo linatusumbua
muungano twakosoa
kwani unatuumbua

Kutenda kosa si kosa
kosa kurudia kosa
tuyakosoe makosa
haki tusije ikosa
 
Aaah! amechanganya historia ya tanganyika na zanzibar huyu mie nimemwelewa hivyo! lakini ameskip! 9.december ni uhuru wa nchi ipi! mwanakijiji umenunuliwa? maana katika utenzi huu unaonyesha kuwa kwa jinsi mwingiliano wa maisha wakati wa ukoloni tulitakiwa kuwa tanzania since before sivyo? Huoni hii ni history ya kufikirika hii! ebu tengeneza utenzi kama huu specific kwa Tanganyika sawa mkuu usibadilike kaka!
 
Hivi Tanganyika ni nchi ya nani? Kwanini watu wanalilia nchi ya mkoloni?
Labda ungetusaidia kutuonesha Tanzania bara iko wapi nadhani huu utata wote utaisha. United Kingdom inaonesha kila kitu na kila kisiwa status yake,kwa nini sisi tunakuwa matapeli?
 
Hivi Tanganyika ni nchi ya nani? Kwanini watu wanalilia nchi ya mkoloni?

Kwa mara ya kwanza unisamehe ndugu......napata taabu kutamka hili.......lakini nahisi swali hili.....lakini nisamehe kwa sababu nakuheshimu....ila hata kama mkubwa hajambi......akikosea lazima tumseme.......katika hili.....UMETUMIA MASABURI KUPOST.

Tanganyika ni nchi yangu na si nchi ya mkoloni. Kama ingekuwa nchi ya mkoloni isingesubiri hadi 1964 kusilimu au kubatizwa na kuitwa Tanzania
 
Back
Top Bottom