Utengenezaji wa Sabuni za Aina Mbalimbali: Fahamu Mahitaji, Mchakato wa Uzalishaji na Masoko

Mkuu mimi sina mtaji, ila kama kuna tenda, tafadhari niajiri(DAR),

Vilevile sabuni zipo za aina nyingi hivyo utengenezaji na malighafi hutofautiana kidogo, kutokana na na aina unayohitaji!

SABUNI NGUMU
Sabuni hii inatumika kuondoa uchafu mgumu

Pima maji vipimo 5 ktk chombo cha plastik kikubwa
ongeza sodium hydroxide kipimo 1
acha mchanganyiko uchanganyike vizuri hadi uanze kupoa.
Ongeza mafuta vipimo 6 kwenye mchanganyiko wako huku ukikoroga bila kukoma hadi dakika 60.

Kabla sabuni haijawa ngumu sana, ongeza vipimo 2 vya kaolin iliyochekechwa vizuri kama kaolini haipatikani unaweza kutumia majivu ya kuni yaliyochekechwa vizuri
mimina sabuni kwenye kifyatulio(plastic) na baada ya kuganda ikate vipande kasha iweke sehemu safi ikauke taratibu hadi ndani ya wiki 12 sabuni itakuwa tayari kutumika.

Vipimo vyote ni kufuatana na idadi ya sabuni unayotaka na chombo unachopimia
Mfano unatumia kipimo cha Lt 1,
Utapima maji lt 5 sodium hydroxid lt 1 vivyohivyo kwa vipimo vikubwa!

TAHADHARI-
Sodium hydroxide {NaOH} ni hatari.
Lazima iwekwe mbali na mahali wanakofikia watoto.

*Kama mtoto atameza sodium hydroxide ni lazima apewe maziwa mengi au kikombe 1 cha mchanganyiko wa juisi ya limau/siki na vikombe 20 vya maji.
*Sodium hydroxide hushambulia ngozi, kuwa mwangalifu kila mara unapotengeneza sabuni, nawa mikono vizuri, hali ya unyevu katika hewa huibadili sodium hydroxide kuwa kimiminika hivyo ni rahisi kudhuru ngozi yako.
*Sodium hydroxide hushambulia aina zote za metali, hivyo tumia vyombo vya mfinyanzi hii itasaidia na kama vyombo vya mfinyanzi havipatikani tumia aina nyingine ya vyombo vya plastiki.
Ni lazima sodium hydroxide {NaOH} ihifadhiwe vizuri kwenye vyombo visivyopitisha hewa.

MAANA YA MANENO
Kaolin ni udongo mweupe wa mfinyanzi unaopatikana mtoni. katika Africa hutumika kupamba kuta za nyumba .
Sodium hydroxide NaOH ni kastiki.
 
naomba msaada kwa wajasimari wote, napenda sana kujifunza vitu mbalimbali na kitu kimoja ni kujua jinsi ya kutengeneza sabuni za miche, hivyo napenda sana kama naweza pata msaada wa maelezo ya jinsi ninavyoweza jifunza mwenyewe jinsi ya kutengeneza sabuni

Ngamba

ubarikiwe ni hv ili kutengeneza uahitaji yafuatayo:

caustic soda,mafuta:,mawese,nazi,nyonyo,mbosa au mise.,chumvi,glicerin,perfume na rangi.
i) JINSI YA KUTENGENEZA.
Chukua caustic soda kg1 changanya na maji lita 5 koroga kwa dk 5 acha kwa siku 7.N.B:Chombo utacho tumia kuchanganya isiwe plastic.

ii)Baada ya siku hizo saba changanya na mafuta lita 10 ikumbukwe mafuta utayotumia ni aina moja wapo kati ya hizo tajwa hapo juu hasa kwa kuzingatia ni yapi yana bei nzuri sokoni.

Mafuta hayo unayachemsha sawa sawa yahive hii unaweza kutambua kwa kutumbukiza karatas nyeupe ikitoka nyeupe yameiva so acha yapoe na baadae koroga kwenye mchanganyiko huo huo na kuweka glicerin robo lita,chumvi robo kg,rangi kijiko cha chai,na perfume kijiko cha chai.

Baada ya kukoroga utapata uji mzito ambao utapeleka kwenye "mould" hv ni vifaa maalum vyenye umbo tayari kama mche wa sabun vyaweza kuwa vya mbao au chuma.Tunatumia hivi kutokana na bei ya mashine ya sabun hz kuwa ghali mno.


Ili iitwe sabuni inatakiwa
-Ngumu kuiisha
-Yenye povu jingi
-Nyeupe
VIAMBATA VYA kutengenezea sabuni
1)Mafuta-mawese,mise,wanyana
2)Maji
3)Caustic soda(costiki soda)
VIFAA VYA KUTENGENEZEA
-Ndoo za plastiki lita 20 nne
-Diaba 1
-Mti wa kukorogea
-Mashine ya kukorogea
-Box la kugandishia
-Mhuri wa biashara
-Mzani wa saa
-Vibao vya kukatia
VIFAA VYA USALAMA
-Mask
-Groves
-Gum boots
-Goggles (miwani)
-Overall
-Ndoo ya maji au mchanga
FORMULA
-mafuta lt1+caustic soda grm135+maji mls350+sodium siligate prm100
KUCHANGANYA
pima maji ktk ndoo ya plastic kisa weka caustic soda ktk maji weka kidogokidogo huku ukikoroga mpaka itakapo yeyuka.mchanganyiko huu unaweza kuchemka na kutoa mosh usiogope. acha ipoe kuanzia masaa 8 nazaidi
KUCHANGANYA NA MAFUTA
yeyusha mafuta kwa kuyapasha joto kidogo ambapo unaweza kuyashika, tia sangi na mimina kidogo2 kuchanganya michanganyiko huku ukikoroga. mimina kwenye box la kugandishia acha igande tayari kwa kukata.Pia weka sodium siligate
 
Mkuu Ngamba hili linawezekana siku hizi kutokana na uwepo wa mafunzo mengi sana ya wajasiriamali na somo hili hufundishwa kwa ufasaha sana. Binafsi niliwahi kuhudhuria mafunzo kama hayo yaliyokuwa yakiendeshwa na kampuni moja halafu baadaye ikaibuka kwa jina la MJASIRIAMALI KWANZA ya Dr. Didas Lunyungu. Hii kampuni inaendesha mafunzo hayo na hivi karibuni wataendesha mafunzo kama hayo huko DAR LIVE. Lakini haya ya sasa ambayo yataanza tarehe 13 Agosti, 2013 ni kwa ajili ya wanawake tu. Hivyo basi ili kukidhi tamanio lako, wasikilize kwenye vipindi vyao huko WAPO RADIO utapata taarifa zote na kama uko sehemu ambayo radio hii haifiki basi sema ili nikutafutie namba zao. Fuatilia ushauri huu utajibu kiu yako. Barikiwa.
 
Wadau kwa yule anaefahamu kutengeneza sabuni ya maji atupe maujanja hapa


==============================================

JIFUNZE KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI YA KUNAIWIA MIKONO View attachment 376324

Moja kati ya mahitaji makubwa ya watu ikiwemo wafanyabiashara za mama lishe,mabucha na nyingine,ni sabuni ya kunawia.Kutokana na mahitaji makubwa waliyonayo watu na kukosekana kwa bidhaa hiyo wahitaji hujikuta wakitumia sabuni ambazo hazikutengenezwa kwa kazi hiyo kama sabuni za unga,shampoo na sabuni za vipande ambazo huwasababishia madhara bila kujijua.

Leo katika somo letu tutajifunza jinsi ya kutengeneza sabuni za kunawia mikono. Fuatana nami mwanzo mpaka mwisho.

MAHITAJI; .
Sulphonic acid .soda ash .maji yaliyochujwa vizuri .pafyum .Rangi yoyote inayovutia .sless .Chumvi

JINSI YA KUTENGENEZA.
Andaa vizuri chombo chako kwaajili ya kutengenezea sabuni yako kama ndoo au pipa pamoja na kuandaa malighafi zako huku ukizingatia usafi.

Tanguliza kumimina ssulphonic acid vijiko vitano vya chakula kwenye chombo chako. Endelea kuweka soda ash iliyochanganywa na maji vijiko vitatu vya chai.

Weka maji lita tano ukifuatiwa na sless robo lita,chukua pafyum yoyote na uweke kijiko kimoja na nusu cha chai.

Ongeza rangi kijiko kimoja cha chai na uanze kunyunyizia chumvi ambayo huleta uzito na kufanya sabuni yako isiharibike na kukaa muda mrefu.

Koroga vyote kwa pamoja kwa muda wa dakika ishirini na sabuni yako itakuwa tayari.
 
Kwa ufupi mpendwa hapo juu amesaidia sana maelezo ila mimi ningependa kama upo dsm naweza kuja kukufundisha.0717539573 ila ukipata semina ya Dr.Lunyungu ni nzuri kwani hata mimi ni zao lake.
 
Kwa ufupi mpendwa hapo juu amesaidia sana maelezo ila mimi ningependa kama upo dsm naweza kuja kukufundisha.0717539573 ila ukipata semina ya Dr.Lunyungu ni nzuri kwani hata mimi ni zao lake.

Tafadhali mpendwa ebu pata msukumo wa moyoni kutufunza wote hapa JF
 
ubarikiwe ni hv ili kutengeneza uahitaji yafuatayo:

caustic soda,mafuta:,mawese,nazi,nyonyo,mbosa au mise.,chumvi,glicerin,perfume na rangi.
i) JINSI YA KUTENGENEZA.
Chukua caustic soda kg1 changanya na maji lita 5 koroga kwa dk 5 acha kwa siku 7.N.B:Chombo utacho tumia kuchanganya isiwe plastic.
ii)Baada ya siku hizo saba changanya na mafuta lita 10 ikumbukwe mafuta utayotumia ni aina moja wapo kati ya hizo tajwa hapo juu hasa kwa kuzingatia ni yapi yana bei nzuri sokoni.Mafuta hayo unayachemsha sawa sawa yahive hii unaweza kutambua kwa kutumbukiza karatas nyeupe ikitoka nyeupe yameiva so acha yapoe na baadae koroga kwenye mchanganyiko huo huo na kuweka glicerin robo lita,chumvi robo kg,rangi kijiko cha chai,na perfume kijiko cha chai.Baada ya kukoroga utapata uji mzito ambao utapeleka kwenye "mould" hv ni vifaa maalum vyenye umbo tayari kama mche wa sabun vyaweza kuwa vya mbao au chuma.Tunatumia hivi kutokana na bei ya mashine ya sabun hz kuwa ghali mno.
 
Asante sana Buhaya Boy, umesaidia wengi. Ushauri wangu, SIDO huwa wanatoa vilevile elimu hiyo pamoja na elimu juu mambo mengi mbalimbali. SIDO ni Taasisi ya Umma na Umma ni sisi wenyewe Watanzania. Hivyo tusisite kuwasiliana nao. Wana Ofisi karibia katika kila Mkoa huku Tanzania Bara.
Ushauri wangu mwingine ni kuwa tujenge mazoea ya kufanya kazi hizi katika Umoja/Vikundi. Umoja/Kikundi sio lazima kiwe cha watu wengi - watu 2, 3, 4, 5 nk. Kuna faida lukuki kwa kuendesha shughuli za uzalishaji kwa Umoja/Vikundi!
 
MahinaVeteran nimependa busara yako ila mm nimehangaika sana hpa dsm nimekosa kundi kila mtu anawaza ajira hata kama nikufua chupi ili mradi apande Daladala aonekane anaenda kazin.Pia sido bei zao zipo juu nilienda mashine ya sabun za miche ya bei ndogo ni m.10 jambo ambalo ni changamoto kwetu.
 
Kka Nashukuru sana na kama nigekuwa nipo dar nigekutafuta na kuhudhuria mafunzo ya dr.
niko Entebbe - Uganda. so i miss a lot

usikonde wewe anza tu usisubiri watu kujiunga most of the time i copy nike slogan
JUST DO IT
 
mbona lahisi sana just pm me nd i will send u the simple way how to make it, however u need to find out where u can buy your supply material( vitu unavyohitaji kutengeneza):A S-key:
 
vp huko entebe kuna soko la vikoi vya batiki make nshawahi fika kasensero wanawake wanapenda jifunga sana vitenge nifanyie utafiti na uniPM.
 
Mkuu Ngamba, habari za Kitooro? Vijiwe kama Catch 22, Jeremiah's na Four Turkey's, Entebbe Motel, Golf Club bado vipo? Siku njema
 
mm najua vitu vingi kwa dsm niPM ili tuwe na kikundi tutengeneze vitu kibao.Make c unajua na uchaguzi unakuja taasisi nyingi tutapokelewa vizuri ili tujikwamue kwani ka kiwanda ketu lazima wanasiasa wakaneemeshe na kura hatuwapi.
 
MahinaVeteran vipo sana na vinaendelea kama kawaida na vingine vipya navyo vinazidi kushamili
 
Last edited by a moderator:
Pale Mwenge (Dar es salaam) karibu na TRA kuna duka la MJASIRIAMALI KWANZA INTERPRISES wanafundisha kutengeneza sabuni za maji na malighafi zinapatikana hapo au ufuatilie kwani wanakuwa na semina ambazo wanafundisha jinsi ya kutengeneza bidhaa nyingi sana.
 
Ila za vipande ndo zinalipa nitumie laki tano nikupe ze formular
 
mbona lahisi sana just pm me nd i will send u the simple way how to make it, however u need to find out where u can buy your supply material( vitu unavyohitaji kutengeneza):A S-key:

mm najua vitu vingi kwa dsm niPM ili tuwe na kikundi tutengeneze vitu kibao.Make c unajua na uchaguzi unakuja taasisi nyingi tutapokelewa vizuri ili tujikwamue kwani ka kiwanda ketu lazima wanasiasa wakaneemeshe na kura hatuwapi.
if you can share public do so kuliko haya masuala ya PM PM kama unauza pia just say kama tunaweza kununua huo utaalamu
 
Back
Top Bottom