Utata wa maadhimisho ya uhuru

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
Serikali inadai kuwa tarehe 9 Dec kutakuwa na maadhimisho ya 50 ya uhuru wa Tanzania,
Maswal yenye utata ni haya:
1:Je Tanzania ilitawaliwa na nani before huo uhuru?
2:Je Tanzania ilipata lini uhuru?
3:Ni nani alileta uhuru wa Tanzania?
Katika pekuapekua zangu sijaona sehemu ambayo imeandikwa kuwa Tanzania ilipata uhuru badala yake nimeona kuwa ni Tanganyika ndo ilipata uhuru..
Wadau tujuzane ni lipi jina stahili katika kusherekea huo uhuru wa miaka 50.
Nawasilisha.
 
tanzania ilibarikiwa mwaka 1964 na kuzika tanganyika ila bado inashangaza kuiadhimisha yaa hapa kuna maswali mengi na ukitaka kuondolewa serikalini jaribu kuichambua Tanganyika na tanzania kuelekea maadhimisho ya uhuru wao
 
Wakwere kukana historia ni rahisi kabisa, noma ni pale anapowaingiza mkenge watanganyika wengine nao wanakubali. Ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.
 
Kama hatupendi kutumia jina Tanganyika basi tutumie Tanzania bara tusije tukapotosha historia.
 
tanzania ilibarikiwa mwaka 1964 na kuzika tanganyika ila bado inashangaza kuiadhimisha yaa hapa kuna maswali mengi na ukitaka kuondolewa serikalini jaribu kuichambua Tanganyika na tanzania kuelekea maadhimisho ya uhuru wao
Ahaaa! ilizikwa Tanganyika yetu,zanzibar ikaachwa,ndo mchezo wenu eeeeeeeeeeeeee!
 
Mimi napendekeza wanaoikumbuka na kuipenda Tanganyika siku hiyo tarehe 9 December sisi tukutane Jangwani uwaache wanaofikiri kuwa Tanzania ilipata uhuru tarehe 9 Dec waende uwanja wa Uhuru. Tanzania ilianzia April 26 1964. Tanganyika ilipata Uhuru Dec 9, 1961
 
tanzania ilibarikiwa mwaka 1964 na kuzika tanganyika ila bado inashangaza kuiadhimisha yaa hapa kuna maswali mengi na ukitaka kuondolewa serikalini jaribu kuichambua Tanganyika na tanzania kuelekea maadhimisho ya uhuru wao

Tanganyika ilikufa au ilifunga ndoa na Zanzibar?
kama Tanganyika ilikufa mbona Zanzibar bado ipo?
 
Tanganyika = Tanzania Bara
Zanzibar = Tanzania Visiwani

Uhuru wa Tanzania Bara! stupid!!
 
Ni ujinga usio na kifani kusherehekea kitu kisichokuwepo. Mie ninajua Tanzania itafikisha miaka 50 ifikapo 2014 na sio vinginevyo kwa sasa ninajitahidi kujiandaa na Jubilei ya Fedha ya Tanganyika huku nikiwa ninakabiliwa bado na adui ujinga, umasikini na maradhi.
 
sasa wajameni tatizo lipo kwa nani? Kwa serikali ambayo inaandaa maadhmisho au lipo kwa wananch wasiojua historia yao?
 
Back
Top Bottom