Utaratibu wa uhakiki vyeti (Vetting) Tanzania ni wa ovyo sana! Unapotezea watu muda pasipo sababu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Kusema ukweli!

Nimefuatilia nimegundua tuko nyuma sana kiakili pamoja na teknolojia! Kwa karne hii sikutegemea uhakiki wa vyeti vya masomo kwa watu (Vetting) uwe kizamani namna hii! Popote ukiomba ajira au panapohitaji uhakiki wa vyeti Tanzania bado tunatumia mbinu ya kizamani sana!

Mfano! Umeomba ajira Dodoma! Utapeleka CV yako wataipitia, then watatuma vyeti vyako chuoni kwa uhakiki kwa sanduku la posta! Mchakato wa kuvituma vyeti chuoni unachukua mwezi, hapo hujazungumzia endapo muombaji kasoma chuo zaidi ya kimoja!

Hapo kunakupotea bahasha au kufika, na endapo ikifika hadi ifunguliwe hapo chuoni kwa Uhakiki wa chuo inaweza fikisha miezi mitatu! Hapo hadi mkuu wa chuo faili limfikie mezani kwake asaini, waandae barua ya kujibu kwenda idara au kampuni husika miezi 6 inapotea!

Na majibu yake hutumwa kwa barua ambapo yanweza kufika au kupotelea njiani! Huu ndiyo utaratibu wa kuhakiki vyeti vya masomo unaotumika hadi Leo Tanzania!

Kwa wenzetu Huko duniani VETTING YA CHETI wanaichukulia serious sana, Wanaamini hayo ni maisha ya mtu, wanaipokea taarifa haraka kama vile taarifa ya msiba, kwamba haiwezi kuzidi masaa 12 kwa wenzetu email zote za VETTING Zinakuwa zimejibiwa

Hapa kwetu bongo sijui nani katuroga wallah! VETTING ya saa 12 inachukua miezi 12 kama vile mtu karudi kusoma tena!

Waziri wa ajira na kazi yupo kimya, kamishina utumishi wala hajigusi, waziri wa elimu na wasaidizi wake wala hawamwambii hilo ni tatizo!
 
A lot of shit from shithole country
Inashindikanaje taasisi ya elimu kuwa na platform moja! Waka upload huko majina ya wahitimu wao?

Kwamba ukitaka kuhakiki cheti cha mtu ukiingiza namba ya cheti kila kitu kinajibu?
Hivi kweli haya mambo ni kutumiana sanduku la posta hadi Leo?

Emaili kibao, mitandao kibao, application zipo kibao!
Tanzania hatujui tunakokwenda tuseme tu ukweli
 
Inashindikanaje taasisi ya elimu kuwa na platform moja! Waka upload huko majina ya wahitimu wao...
Mkuu hii nchi imejaa mazuzu wengi Sana inahitaji miaka 100 ili ikae sawa

Mtu upo katika harakati za kupambania ugali lakini unakutana na Upuuzi kibao , hawana Maarifa wao wanafanya vitu kwa kukalili tu
 
Ukishaona hivyo ujue ajira hupati.

Wanachukua CV wanaangalia tu vyeti kijuu juu alafu unaingia kazini.

Hizo process ni njia ya kukukatisha tamaa. Pole sana.
 
Vetting yenyewe haipo sana sana wataangalia kwenye mfumo kama wewe ni nyuki wa kijani au la
Ukiwa sio umeliwa
 
Back
Top Bottom