Utaratibu wa kupima Ukimwi bongo una maswali mengi kuliko majibu: Kuna haja ya kuboresha

Siku hizi kupima ni lazima tena siyo hiyari kama zamani,ukienda hospitali ya serikali kupima hata maralia lazima wakupime ukimwi,wakikuta signal zinasoma,unabebwa msobe msobe hadi kwenye ushauri nasaha,yaani kibabe tu!sasa wewe kaa hivyo hivyo
Ohoo basi hii hatari
 
Labda kama ananipima bila mimi Kujua lakini mbali na hapo haiwezekani
 
Unaweza kupimwa mara moja. Hichi kipimo sio cha bure. Ni shillingi laki moja. Vinapatikana kwenye hospitali kubwa za kanda.
Nenda na hela. Tatizo wengi tu apenda vya bure. Hichi kipimo ni uhakika
 
Naomba nitoe ufafanuzi japo kidogo kulingana na uelewa wangu.
Kwanza kabisa naomba nikupe taarifa kwamba kwa muongozo mpya wa NACP, muda wa kusubiri kwa ajili ya kipimo cha marudio ni mwezi mmoja na sio miezi mitatu tena.

Kwanini ufanye kipimo cha marudio?
Ugonjwa wowote, hasa magonjwa yanayoambukiza huwa yana mlolongo wake maalumu wa kuingia mwilini hadi kufikia hatua ya kuleta madhara yanayoonekana (Pathogenesis), na pia magonjwa yote yana kipindi chake maalum inachokuchukua mgonjwa tangu siku umeupata ugonjwa hadi kuanza kuonesha dalili za awali.
Kwa virusi vya Ukimwi inaweza kukuchukua kuanzia wiki mbili hadi miaka kadhaa bila kuonesha dalili.
Kwahiyo tunatakiwa kufanya kipimo cha marudio kwasababu watoa huduma wanakua na imani kwamba huenda usiku kabla ya siku ya kwenda kupima ulifanya mapenzi na mtu anaeweza kuwa muathirika ama siku kadhaa zilizopita na hivyo vile virusi bado havijafikia kwenye hatua ya kutambulika na chembe za mwili, na hivyo haiwezekani kusomeka kwenye kipimo cha kawaida kinachotumika (Bioline). Hivyo tunashauriwa kurudi tena kufanya kipimo cha uhakiki baada ya muda ili kama mwili ulikua haujatambua uwepo wa virusi basi unaweza kuwa tayari umetambua, na katika kuelezwa kuhusu kurudi nina imani unashauriwa usifanye tena ngono zembe na mtu mwingine.

Kuhusu damu kupewa mgonjwa!
Kwanza naomba nikutaarifu kwamba kwa hali ilivyo sasa, hakuna damu inayotolewa kwa mchangiaji na kupelekwa moja kwa moja kwa mhitaji (mgonjwa), damu inapotolewa inahifadhiwa kwenye mifuko maalumu, kisha sampuli ya hiyo damu inachukuliwa na kutumwa kwenye maabara maalumu ya vipimo (CPL) kwa ajili ya utafiti na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo; VVU na homa ya ini. Baada ya vipimo hivyo ndipo majibu ya sampuli hizi hurudishwa vituoni na kuruhusiwa kutumika pale tu inapokua salama.
 
Nilikataa matibabu Police Barracks kisa upuuzi huohuo, me nimekuja na matatizo yangu Dr anaanza kunibambikia kipimo kingine tena cha UKIMWI

Nisimkimbie nin hata nilichoendea sikumalizia nikabadili hospitali
hahahah duh
 
Siku hizi kupima ni lazima tena siyo hiyari kama zamani,ukienda hospitali ya serikali kupima hata maralia lazima wakupime ukimwi,wakikuta signal zinasoma,unabebwa msobe msobe hadi kwenye ushauri nasaha,yaani kibabe tu!sasa wewe kaa hivyo hivyo
mkuu ndio hari ilivyo hivyo kweli au unatania tu.
 
Naomba nitoe ufafanuzi japo kidogo kulingana na uelewa wangu.
Kwanza kabisa naomba nikupe taarifa kwamba kwa muongozo mpya wa NACP, muda wa kusubiri kwa ajili ya kipimo cha marudio ni mwezi mmoja na sio miezi mitatu tena.

Kwanini ufanye kipimo cha marudio?
Ugonjwa wowote, hasa magonjwa yanayoambukiza huwa yana mlolongo wake maalumu wa kuingia mwilini hadi kufikia hatua ya kuleta madhara yanayoonekana (Pathogenesis), na pia magonjwa yote yana kipindi chake maalum inachokuchukua mgonjwa tangu siku umeupata ugonjwa hadi kuanza kuonesha dalili za awali.
Kwa virusi vya Ukimwi inaweza kukuchukua kuanzia wiki mbili hadi miaka kadhaa bila kuonesha dalili.
Kwahiyo tunatakiwa kufanya kipimo cha marudio kwasababu watoa huduma wanakua na imani kwamba huenda usiku kabla ya siku ya kwenda kupima ulifanya mapenzi na mtu anaeweza kuwa muathirika ama siku kadhaa zilizopita na hivyo vile virusi bado havijafikia kwenye hatua ya kutambulika na chembe za mwili, na hivyo haiwezekani kusomeka kwenye kipimo cha kawaida kinachotumika (Bioline). Hivyo tunashauriwa kurudi tena kufanya kipimo cha uhakiki baada ya muda ili kama mwili ulikua haujatambua uwepo wa virusi basi unaweza kuwa tayari umetambua, na katika kuelezwa kuhusu kurudi nina imani unashauriwa usifanye tena ngono zembe na mtu mwingine.

Kuhusu damu kupewa mgonjwa!
Kwanza naomba nikutaarifu kwamba kwa hali ilivyo sasa, hakuna damu inayotolewa kwa mchangiaji na kupelekwa moja kwa moja kwa mhitaji (mgonjwa), damu inapotolewa inahifadhiwa kwenye mifuko maalumu, kisha sampuli ya hiyo damu inachukuliwa na kutumwa kwenye maabara maalumu ya vipimo (CPL) kwa ajili ya utafiti na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo; VVU na homa ya ini. Baada ya vipimo hivyo ndipo majibu ya sampuli hizi hurudishwa vituoni na kuruhusiwa kutumika pale tu inapokua salama.
hii uliyosema ni theory! lakini practical watu huko mikoani wanachangia sana damu za kumuwekea mgonjwa! tena wanakuwa specific kuomba apatikane mwenye group husika la mgonjwa! wakati mwingine damu rasm haipatikani mtu anawekewa Equivalent tu A positive kwa A negative
 
Kwanza kabisa niseme! utaratibu Wa kupima ukimwi mbali na kuwepo maswali mazito lakini pia siyo rafiki hasa kwa wanaume!

  • Sijawahi kuelewa kwanini mtu akishapimwa, bado anatakiwa ku-comfirm tena na tena after three months anapimwa second round, halafu tena after three months third round!..Kwanini miezi yote tisa jaman?
  • miezi yote hiyo tisa yakusubili kurudia kupima kiuhalisia mapenzi huyo mtu anakuwa anafanya na nani?
  • Kama kupima mara moja siyo sahihi, Je; Zile damu za kuchangia watu huwa zinapimwa Mara ngapi nakupelekewa wagonjwa pasipokusubili miezi tisa, Je damu hizo huwa siyo salama?
Naomba mwenye majibu tafadhali; Maana naona huo utaratibu siyo rafiki kwa wanaume kabisa ndiyo maana tunakimbiaga majibu
Virusi vinaanza kuonekana saa 48 mpaka miezi mitatu baada ya kuambukizwa
Nia ya kukuambia urudi ni safi tu,pengine ulivyopima umeonekana huna,lakin virusi umeambukizwa mwezi jana ila havijakomaa kiasi cha kuonekana kwenye kipimo
 
Back
Top Bottom