Utapeli tiGOPesa!

Tuache tabia ya kubisha kwa kila kitu ni vema kuchukua tahadhari mapema kuliko kuanza kulia baadaye bila mafanikio
 
Hii habari inaweza kuwa na ukweli ndani yake,nilitaka kununua vocha kupitia tigo pesa mnamo tarehe 24th Oct,nikaletewa msg kuwa kuna tatizo hivyo ombi langu linashughulikiwa lakini transaction katika account yangu ilikuwa imeshafanyika kwani baade nikapata msg kwamba nimefanikiwa kununua salio,nilipocheki kwenye balance yangu hakukuwa na ongezeko lolote,nilijaribu kuwasiliana na customer care lakini sikuweza kufanikiwa na kila nilipokuwa najaribu walikuwa wanakula salio ikabidi niwe mpole na kukubali imekula kwangu mazima...
 
Hata mimi ni mhanga wa tatizo hilo,leo asubuhi nimenunua airtime kwa tigopesa kwanza ilikuwa inagoma baadae ikaniletea msg kuwa transaction imefanikiwa lakini kucheki salio hakuna kilichoongezeka ha hela yangu wamekata, imenifanya hata nishindwe kutoa vijisenti vyangu nilivyohifadhi humo.
 
Kuna wakala mmoja wa tigo pesa aliniambia kuna kipindi walirushiwa pesa kimakosa kutoka tigo. Kwa maelezo yake upandishaji wa gharama za kupiga simu ulio anza kama wiki tatu hivi ulilenga kuokoa hasara iliyopatikana. Sina uhakika sana wa maelezo yake lakini inavyo onekana ni kweli tigo mfumo wa pesa haujatengamaa vizuri
 
Last week nlinunua salio la 3000 kupitia tigo pesa, ilikaa kama masaa mawili ndo wananiambia operation successfull lakini kuangalia salio, kulikuwa hawajaweka.
JANA, nimenunua tena salio la 10000 hawanipa mpaka navoandika hapa.
Nimewapigia usiku, wakanambia mtandao wao wa tigo pesa una matatizo kwa sasa ivo watanirudishia.
Lakini nkikumbuka 3000 hawakurudisha. Inanipa wasiwasi kama watanirudishia 10000 yangu.
 
Afadhali watikiswe kusudi wajiimarishe kabla hajaja serious hacker akaswafi accounts zote. Iliwahi kutokea nadhani mwaka 2004,niliweka voicha airtel na kupiga simu naambiwa sina salio.nikawaambia wakaahidi kurudisha kwani shida ilikua system. Nilikumbusha twice bila mafanikio nikaachana nao.
 
Uzushi, hakuna sababu ya kufikiri kuwa kuna hackers wameingilia mtandao, matatizo ya kiufundi tu.
 
kaka hiyo habari ni kweli tupu,
mwanzo nilinunua salio la 6,000 balance yangu ikapungua lakini airtime haikuongezeka, mara ya pili nikanunua 10,000 hadithi ikawa ile ile, ikabidi niende ofisi za tigo pale mlimani city. Nilipofika nikakuta wenye tatizo kama langu wako wengi. Hivyo tukashauriwa tuandike kwenye karatasi majina yetu na namba za simu pamoja na kiasi kilichokatwa kimakosa. Baada ya hapo nimekaa kwa wiki nzima hadi leo tarehe 27 / 10 /2011 ndio nimerudishiwa hilo salio langu kwa ujumbe uliosomeka ''your transaction has been rolled back due to system error. New balance'' ..... tigo poleni sana.
 
Umenichanganya majungu ya nani,hackers au muanzisha thread?
kaka wengine ndio hao wanakurupuka tu na kuanza kuandika ni sawa na wale wabunge wetu wakiwa mjengoni utakuta wanauchapa usingizi wakishtuliwa tu na nao hugonga meza au huitikia ndioooo imepita wakati hawajui nini kimezungumzwa
 
Last week nlinunua salio la 3000 kupitia tigo pesa, ilikaa kama masaa mawili ndo wananiambia operation successfull lakini kuangalia salio, kulikuwa hawajaweka.
JANA, nimenunua tena salio la 10000 hawanipa mpaka navoandika hapa.
Nimewapigia usiku, wakanambia mtandao wao wa tigo pesa una matatizo kwa sasa ivo watanirudishia.
Lakini nkikumbuka 3000 hawakurudisha. Inanipa wasiwasi kama watanirudishia 10000 yangu.
Usijali tigo hakuna ujanjaujanja watakurudishia pesa zako zote nawaamini sana.
 
Ni mwendelezo wa vituko na wizi ndani ya TIGO pesa leo wamekata shs 20 kwenye account za wateja , leo sio hackers bali ni wafanyakazi wa TIGO wenyewe
 
kutokana na kutokuwa na usalama wa fedha za watumiaji wengi tigo pesa ni janga lingine linalokuja , kwani jana mtandao ulivamiwa na hackers na leo kuna akount nyingi wamekata shs 20 kwenye akount za watu wengi sana, kuweni macho
 
tuelekeze jinsi ya kuwa macho! kwani kama wanakata auto unawezaje kuprevent manually.
 
Thnx Kamanda na ingekua mimi ni tume ya mawasiliano tigo ningeifuta, coz hata mawasiliano yake ni ya kihuni, Simu iko hewani ukipiga haipatikani, Tigo Hawako makini Ni mtandao wa Hovyo
 
kuna watu juzi walinunua muda wa maongezi lakini wakakatwa pesa zao bila kuongezewa salio. Binafsi walinikata sh. 1500 kwa mtindo huohuo ila walinirejeshea jana. Jamaa yangu walikomba sh. 2000 yake lakini hakurudishiwa hata senti moja.
 
Back
Top Bottom