Hivi karibuni nikiwa nipo Tanzania kwa mapumziko mafupi,niliamua kuuza gari langu kuukuu nililoliagiza kutoka Japan miaka kadhaa iliyopita.Kwa kuwa muda wa mapumziko yangu ulikuwa mfupi sana nikaona nitafute gari mbadala kutoka kwenye "showroom" za hapo Dsm. Nikaamua kununua gari kwa "MAZRUI COMISSIONING AGENT" maeneo ya Kijitonyama.Jamaa ni WEZI,MATAPELI na WANAFIKI ingawa wanajidai ni wachamungu sana. Makubaliano yalikuwa wao wangeshughulikia mambo yote ya usajili TRA na ndani ya siku nne kila wangekuwa wameshamaliza kila kitu. Sikuamini imechukua zaidi ya mwezi gari kusajiliwa!! Hakuna sababu ya msingi wanayotoa zaidi ya porojo na uongo,cha kusikitisha ni pale usajili ulipokamilika,wakakabidhi faili lenye nyaraka zote zinazohusiana na hilo gari,kijana wangu alipokuwa anakagua nyaraka akashangaa kukuta tofauti ya mailage (kms),wakati gari inaonyesha imetembea kms.52,000,nyaraka za ukaguzi huko Japan zinaonyesha gari hiyohiyo ilikaguliwa April 2008 likiwa limetembea kms 131,000.Ina maana kuna usanii wa kuchezea mailage ili mteja uamini umenunua gari lililokwenda kms chache kumbe hali halisi ni tofauti!Nikiwa nawasiliana na mwanasheria ili niwafungulie kesi,nimeona si vibaya nikiwatahadharisha wananchi wenzangu na huu utapeli/wizi wa kimachomacho.Naomba tusambaze ujumbe huu kwa watu wengi ili wote tuwe makini.MAZRUI NI WEZI!!!
Suala la kupunguza mileage nadhani lipo hadi Japan. Wanaweza wakakudanganya kuwa gari imetembea kwa mile kadhaa kumbe si kweli. Mfano mimi mwaka juzi niliagiza Xtrail ya wife. Wao walisema imetembea km 70,000. Lakini ilipofika documents za ukaguzi zilionesha imetembea km 170,000 ingawa kwenye dashboard ilionesha hizo walizodai wao!!!
Hivi karibuni nikiwa nipo Tanzania kwa mapumziko mafupi,niliamua kuuza gari langu kuukuu nililoliagiza kutoka Japan miaka kadhaa iliyopita.Kwa kuwa muda wa mapumziko yangu ulikuwa mfupi sana nikaona nitafute gari mbadala kutoka kwenye "showroom" za hapo Dsm. Nikaamua kununua gari kwa "MAZRUI COMISSIONING AGENT" maeneo ya Kijitonyama.Jamaa ni WEZI,MATAPELI na WANAFIKI ingawa wanajidai ni wachamungu sana. Makubaliano yalikuwa wao wangeshughulikia mambo yote ya usajili TRA na ndani ya siku nne kila wangekuwa wameshamaliza kila kitu. Sikuamini imechukua zaidi ya mwezi gari kusajiliwa!! Hakuna sababu ya msingi wanayotoa zaidi ya porojo na uongo,cha kusikitisha ni pale usajili ulipokamilika,wakakabidhi faili lenye nyaraka zote zinazohusiana na hilo gari,kijana wangu alipokuwa anakagua nyaraka akashangaa kukuta tofauti ya mailage (kms),wakati gari inaonyesha imetembea kms.52,000,nyaraka za ukaguzi huko Japan zinaonyesha gari hiyohiyo ilikaguliwa April 2008 likiwa limetembea kms 131,000.Ina maana kuna usanii wa kuchezea mailage ili mteja uamini umenunua gari lililokwenda kms chache kumbe hali halisi ni tofauti!Nikiwa nawasiliana na mwanasheria ili niwafungulie kesi,nimeona si vibaya nikiwatahadharisha wananchi wenzangu na huu utapeli/wizi wa kimachomacho.Naomba tusambaze ujumbe huu kwa watu wengi ili wote tuwe makini.MAZRUI NI WEZI!!!
Kama unataka kununua gari Usipate shida ya kwenda kote huko. Nchini Uganda kuna Yard nyingi sana zinazouza magari yaliyotumika kama Dubai tena kwa gharama kama ya Dubai au tofauti kidogo tu.
Kwa wajanja waliokwisha jua huwa hawaendi tena mbali huko bali wanakwenda Uganda na unachagua gari yako na kuja kuilipia tax na duty kisha unakuja unaendesha nyumbani.
Epukana na matapeli wa Dar hao.