Utamshauri nini Mwanafunzi huyu?

STK ONE

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
627
184
Mwanafunzi wa kike amenifuata nikiwa staff leo asubuhi.
Mwanafunzi: Mwalimu Samahani. nakuomba usinichukulie vibaya na wala usinielewe tofauti na hivi ambavyo nataka kueleweka.
Mwalimu: Niambie tu usiwe na hofu. Kuna nini?
Mwnafunzi: Mwl. ****** amenitongoza.
Mwalimu: Kwa hiyo umefanya nini?
Mwanafunzi: siku mjibu, lakini tangu juma lililopita amekuwa akinipa adhabu ambazo naona kama vile ananionea.
Mwalimu: kwa nini unahisi anakuonea?
Mwanafunzi: tunafanya kosa moja na wenzangu lakini mimi ananiadhbu mara mbili au mara tatu.
Mwalimu: awali haikuwa hivyo?
Mwanafunzi: hapana, tena leo amenipa adhabu hata sifahamu kosa langu.
Mwalimu: Nenda, Jumatatu nitakuita nikupe ushauri nafikiri nitakuwa nimepata namna nzuri ya kulitatua tatizo lako.

Mimi ni Mwalimu wa kiume, vipi nikimshauri binti amfuate Mwalimu wa kike? Ungemsaidiaje binti huyu??
 
Kama unataka kweli kumsaidia basi zungumza na mwalimu mwenzio aelewe kuwa mapenzi si kulazimishana na hiyo tabia ya ufataki haina mema!
 
Sheria ipo wazi,waalimu hawaruhusiwi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi the vice versa is also true...hivyo muonye huyo mwalimu mwenzako maana anajipalia makaa.
 
duh, kama ni story ya kweli
basi hongera, hadi mwanafunzi kukufuata atakuwa anaona una 'reputation' angalau nzuri.

Afu msaidie, maana wasichana wanakuwa victims sana mashuleni, ongea na mwalimu mwenzio, lakini kuna mwalimu wa malezi unaweza mwambia aende kwa huyo.
 
huyo mwl mwenzako mpumbavu.hawa ndo wale madomo zege wanaoshindwa kutongoza wanawake wa umri wake anakuja kutuharibia kizazi chetu kijacho.mchukulie denti kama mwanao na umsaidie
 
imgekuwa mimi ningemface huyo mwalimu kujua ukweli na kumuonya au kumpeleka kwenye vyombo vya mbele zaidi/mwalimu mkuu ama hata kumpeleka polisi. na alaaniwe huyu mwalimu .if its true story
 
fanyeni mpango mumtegee mtego huyo bazazi..... ili kuwe na ushahidi kabisa . alafu keso mpelekeni mahakamani
 
Isije kuwa hako kasichana kanijitongozesha kwako ki aina aina ndo walivyo wanawake....kuna moja alikuwa anajidai cousin yangu kamtongoza....nikamwambia sasa mbona hukumkataa, akasema naona vibaya atakasirika...nikamwambia basi kama unaona vibaya atakasirika si mpe tu...akasema bora nikupe wewe kuliko yeye, mana yule kisirani sana afu hafichi siri :cool2:
 
Hivi we umesoma taaluma ya ualimu? Chukua hiyo mwalimu na mwanafunzi wapeleke kwa mwalimu mkuu basi!, unataka ushauri Wa nini wakati hayo ni mashtaka? Acheni ujinga wenu Wa ushauri kwenye mambo ya msingi, laiti ningewajua nyie ningewaweka ndani wote mnatuharibia watoto wetu makofongo nyie wakubwa msio na Haya.


Mwanafunzi wa kike amenifuata nikiwa staff leo asubuhi.
Mwanafunzi: Mwalimu Samahani. nakuomba usinichukulie vibaya na wala usinielewe tofauti na hivi ambavyo nataka kueleweka.
Mwalimu: Niambie tu usiwe na hofu. Kuna nini?
Mwnafunzi: Mwl. ****** amenitongoza.
Mwalimu: Kwa hiyo umefanya nini?
Mwanafunzi: siku mjibu, lakini tangu juma lililopita amekuwa akinipa adhabu ambazo naona kama vile ananionea.
Mwalimu: kwa nini unahisi anakuonea?
Mwanafunzi: tunafanya kosa moja na wenzangu lakini mimi ananiadhbu mara mbili au mara tatu.
Mwalimu: awali haikuwa hivyo?
Mwanafunzi: hapana, tena leo amenipa adhabu hata sifahamu kosa langu.
Mwalimu: Nenda, Jumatatu nitakuita nikupe ushauri nafikiri nitakuwa nimepata namna nzuri ya kulitatua tatizo lako.

Mimi ni Mwalimu wa kiume, vipi nikimshauri binti amfuate Mwalimu wa kike? Ungemsaidiaje binti huyu??
 
Halafu wakina Mwanaaasha wakifeli mnakuwa wa kwanza kuwalaumu kumbe chanzo kipo wazi!!Peleka malalamiko kwa mwalimu wa malezi ili hilo bazazi liwekewe kikao na lipewe onyo kali!!
 
Kama ni hadithi ya kweli:-
Kwa usiri mkubwa, fanya mpango wa kumtega Mwl., kwa huyo binti kujifanya kamkubalia Mwl. matakwa yake, ili mumkamate Mwl. kwa ushahidi wa kutosheleza kuiridhisha mahakama.
Angalizo;-
1.inaonyesha dalili kuwa huyo Mwl. ni mzoefu, kwa hiyo umakini wa kulishughulikia jambo hili unahitajika sana.
2.Iwe ni mtego tu, sio afanye kweli.
3.Ushahidi ukikamilika isianze blah blah za maelewano hatua za kisheria zichukuliwe haraka.
4.Akiadhibiwa ipasavyo itakuwa ni fundisho kwake na kwa wengine.
 
Hili suala inabidi kutumia busara ya hali ya juu, Kuangalia kwa ukaribu vitu kama huyo Mwalimu ana cheo gani na watu wake wa karibu hapo shuleni ni nani. Ukiwa nawewe ni Mwalimu wa kiume ukimfuata moja kwa moja anaweza hisi labda wewe ni Mpenzi wake na ndio maana umeingilia kati kitu ambacho chaweza leta shida zaidi. Sema sababu watotot hua wanakua ni woga na haelewi la kufanya yeye Mwenyewe.

Inategemea pia nidhamu ya hapo shuleni na hata Mwalimu mkuu yupo vipi ili kuweza wajibishwa huyo mwalimu. Kuna shule zingine wapo upande wa walimu no matter what. Binti akienda kwa mwalimu Mkuu anaweza akawa kapalia moto hadi kutaka kuhama shule. Akijaribu njia zoote it is beta akatoe taarifa kwa wazazi/walezi.

Hata hivo nashauri kama huyo binti angeweza angemfuata huyo Mwalimu na amwambie; "Baba yangu anafanya kazi HAKI ELIMU, Umenitongoza nimekataa kitu ambacho ni kosa lakini nimetunza heshima kwa kuto mwambia yeyote. Sasa naona umeanza kunionea kwa kunipa adhabu hata nisipostahili. Hili suala linanikosesha raha, na nimeona nikuombe uache hio tabia la sivo itabidi niyafikishe mbele na nina wasiwasi unaweza poteza kazi"

Inategemea Lakini ni binti wa umri gani kuweza sema hayo with confidence.
 
Mshauri kuwa Ikifika Siku ya School Baraza ateme hayo Maneno waziwazi. Na kama kweli una Moyo wa Kumsaidia utamsaidia na kusema kweli ulipata taharifa hizo ila ulikuwa ktk michakato ya kumsaidia. Huyo mwalimu mwenzio mfundishe kutongoza
 
Kutongozwa na mwalimu tu tayari ni adhabu. Katika kusolve hilo inabidi uwe makini usije ukamuweka binti katika wakati mgumu zaidi. Nafikiri ni vizuri ukampa mbinu za binti kumaliza tatizo kuliko kujiinvolve direct.
 
Isije kuwa hako kasichana kanijitongozesha kwako ki aina aina ndo walivyo wanawake....

fazaa haya mambo yanatoke sana hasa kwenye shule za wasichana tupu. Bora hata huyo mwanafunzi ameweza kumface mwalimu mwingine na kumwambia. Wengine huamua tu kutembea na mwalimu kukwepa adhabu. Wakati nasoma kuna mwanafunzi alishawahi kuwa muhanga wa hili na alijaribu kuwaambia walimu hadi mwalimu mkuu na bado hakupata msaada. Kiukweli walimu wa secondary wa kiume wengi wanaharibu madenti.
 
inaonyesha unamwoga huyo mtongozaj omba msaada kwa mwalim mwenzio usaidiwe nawe...walimu banaaaa,
 
Kila binadamu anamapungufu yake na kama stafu mwenzio yoyote yule hutataka apoteze kazi au kumharibia cha msingi hapo kama huyo mwl mtuhumiwa haupo karibu nae sana na kuna mwl mwingine ambae upo karibu naye na ni rafiki wa huy6 mwl mi naona ungemtumia ili yeye ndo amwambie huyo mwl in a friendly manner hapo utakuwa umesolve tatizo na staff yenu itaendelea kuwa organised.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom