Utamjuaje Mgombea asiyefaa kuchaguliwa?

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,115
Ni mgombea muongo yule ambaye ana maneno mengi lakini yasiyo halisi mfano Kuna wimbo aliwahi kuimba Pro, Jay unaitwa ndio mzee, mgombea aliahidi wanafunzi kuwapeleka mwezi kwenda kufanya practical, ahadi kama hizo ni ahadi zinazovutia kuzisikia lakini ni ahadi za uongo zisiweza kutekelezwa.

Mgombea anayetoala hongo ili achaguliwe, au anagawa vitu kama nguo, pesa, kugawa chakula au kul8sha mikusanyiko ili achaguliwe huyo ni mgomvea asiyefaa maana hutumia hayo kama ushawishi na uwezo wake wa kuchagulika.

Mgombea ambaye anamrengo wa udini na ukabila, mfano, mgombea ambaye anasema nichagueni kwa kuwa mimi nanyi ni kabila moja, au dini moja.

Mgombea ambaye Sera anazonadi zitasaidia sehemu fulani tu ya watu na sio watu wote. Mfano, Wafanyakazi wa serikali wataongezwa mishahara, hii sera husaidia kundi la watu wachache sana, ukizingatia idadi ya watumishi wa serikali ni ndogo sana na nafasi zenyewe za kazi zimekuwa finyu sana hivyo sera za namna hii hazifai kwani zitaacha kundi kubwa bila msaada.

Watu wote watakuwa na maisha bora, au nitamaliza umasikini Sera kama hii ni sera ambayo inavutia sana hasa ukizingatia kila mtu ana kou ya kutoka kwenye lindi la umasikini, lakini Je, amekueleza ataumaliza vipi huo umasikini? Au hayo maisha bora atakupa kwa nia gani? Ukiona anatoa ahadi kama hiyo na anaishia hapo bila kukwambia njia atakazotumia kuumaliza huo umasikini, na muda atakaotumia basi jua huyo ni muongo na anatumia umasikini na kutokuwa na ufahamu kwako ili kujinufaisha yeye kwa kupata madaraka.

3.Vijana watapewa kazi Sera kama hii inavutia ila ni sera isiyotekelezeka na hata ikitekelezwa itakuwa ni kwa kundi dogo sana la watu kwani Serikali haina uwezo wa kuajiri vijana wote.

Mgombea anayesema atafanya kitu fulani bila kusema atakifanyaje, na kama kinahitaji pesa zitatika wapi, akisema kodi atatumia njia gani kukusanya hizo kodi, mgombea atayeweza kuja na suluhisho huyo ndio mgombea anayefaa na mwenye sera zenyw kuweza kusaidia jamii na kutekelezeka.

Mfano, mgombea atayesema nitahakikisha vijana wanapata ajira, nategemea aseme labda kutakuwa ba miradi nitaanzisha ambayo itatoa nafasi za kazi kwa vijana huyu amekupa na njia ambayo atatumia kuhakikisha vijana wanapata ajira na si kuongea maneno tu bila mopango.

Je, unazijua sifa nyingine za mgombea asiyefaa? Ongezea hapo
 
Mgombea yeyote wa kisiasa ni muongo tu.

Siasa asili yake ni ghilba. Maneno matamu yenye dhamira ya kumshawishi msikilizaji bila ya dhamira ya kuyatimiza.
 
Back
Top Bottom