Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,110
- 2,513
Sasa kuna hili ambalo nilijadili na watu wakati fulani mpaka kukaleta mabishano ya hapa na pale. Unajua tulichokuwa tunabishania ni kuhusu muda wa kuanza kutumia 'Status ya UCHUMBA'. Kulikuwa na makundi matatu:
1. Hawa wanadai UCHUMBA huanza pale unapomtambulisha mwenzi wako kwa wazazi wako na kuendelea kutambulisha kwingineko.
2. Hili linalofuatia nao wanadai kwamba, UCHUMBA huanza kwenye kipindi cha 'Maagano ya Kiroho' na kundi hili ndilo lilichochea mjadala na kuwa mrefu sana. Kuna kingine hawahawa wanadai kusomana tabia kwa wapendanao unatakiwa kufanyika ndani ya NDOA (kundi la kwanza na tatu tuliwabishania kweli hapo) , kabla ya hapo ni kusomana kijuujuu mfano elimu, familia, ndugu, jamaa, kazi, marafiki na mengineyo kama hayo.
3. Hili la mwisho wanadai eti UCHUMBA huanza pale tu Boyfriend na Girlfriend wanaporidhiana kwa asilimia 100% kwa watafunga ndoa mbele ya safari yao hata kabla ya kutambulisha kwa wazazi.
Ninyi wanajamvi mnazungumziaje kuhusu UCHUMBA huanza kutumika mara tu baada ya kutambulisha kwa Wazazi au?
Karibuni sana...!