Utambulisho wa uchumba...

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,098
2,459
Sasa kuna hili ambalo nilijadili na watu wakati fulani mpaka kukaleta mabishano ya hapa na pale. Unajua tulichokuwa tunabishania ni kuhusu muda wa kuanza kutumia 'Status ya UCHUMBA'. Kulikuwa na makundi matatu:
1. Hawa wanadai UCHUMBA huanza pale unapomtambulisha mwenzi wako kwa wazazi wako na kuendelea kutambulisha kwingineko.

2. Hili linalofuatia nao wanadai kwamba, UCHUMBA huanza kwenye kipindi cha 'Maagano ya Kiroho' na kundi hili ndilo lilichochea mjadala na kuwa mrefu sana. Kuna kingine hawahawa wanadai kusomana tabia kwa wapendanao unatakiwa kufanyika ndani ya NDOA (kundi la kwanza na tatu tuliwabishania kweli hapo) , kabla ya hapo ni kusomana kijuujuu mfano elimu, familia, ndugu, jamaa, kazi, marafiki na mengineyo kama hayo.
3. Hili la mwisho wanadai eti UCHUMBA huanza pale tu Boyfriend na Girlfriend wanaporidhiana kwa asilimia 100% kwa watafunga ndoa mbele ya safari yao hata kabla ya kutambulisha kwa wazazi.

Ninyi wanajamvi mnazungumziaje kuhusu UCHUMBA huanza kutumika mara tu baada ya kutambulisha kwa Wazazi au?

Karibuni sana...!
 
Najiuliza hii dhana ya uchumba ilianza lini na nani alianzisha?Maana kwenye vitabu suala hili sijaliona,sipingi uwepo wa uchumba nahoji uhalali wa kuwepo uchumba na uchumba ni nini?
 
Uchumba, uchumba, uchumba - ushachakachuliwa kila watu wanautafsiri kivyao na wako ''sahihi'' kwa maono yao. Kwa mimi nafikiri uchumba unazaa ndoa sasa haya mauchumba yetu ya kila kukicha kuvalishana mapete nk nk, aaaaaaah!
 
ndugu yangu uchumba mtakatifu ni ule unaotakiwa kuheshimiana na sio kuchakachuana,ukiona anakuomba mabo ful;ai huyo ana tamaa zake sio muoaji kabisa ana llke jambo tena umkimbie kama ukoma.
hata bibilia inasema ikimbieni dhambi ya zinaa, nikinukuu kwenye kitabu cha mwanzo yusufu alimkimbia mke wa bosi wake potifa, akakimbia uchi akaacha nguo zake, sasa wewe binti unakulije kirahisirashisi tu kuuchafua mwili wako kwa uzinzi? nadhani umenielewa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom